Serikali yatoa Tsh. Bilioni 66 Kurekebisha Miundombinu iliyoharibiwa na mvua

Ahsante kwa taarifa na inapendeza sana...


Cc: mahondaw
 
Ametoa pesa toka mfukoni mwake? Basi jambo zuri kama kajitolea. Lakini kama kaidhinisha fedha za walipakodi zikarabati miundombinu hiyo ni habari nyingine na hajatoa yeye.
 
Ametoa kwenye account yake anayoingiziwa Mshahara?
Mkuu Mjomba Magu alikuwa anasema katoa.........,mko kimya,leo Mama yetu anatoa kamili plus mnakasirika?Acha unafiki.Mlikuwa mnasifu hata nonsense issues kama Madagascar drug pammoja na kuitwa profesa aliehitimu Germany. Tanzania ni wanafiki.
Mama Piga kazi tupo nawewe.
 
Sasa ni wakati wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yenywe kutoa pesa maana ni Raisi tu ndo anatoa pesa zake....serikali kimya
 
Sema watanzania kupitia kodi zao ndio wametoa hizo pesa. Na rais anawajibika kuzisimamia zikafanye kazi iliyokusudiwa.

Rais Samia hana hiyo pesa, na hata angekuwa nayo isingeweza kuitoa.
 
Chawa utawaweza?
 

Mkuu nimeuliza maana mbatizaji amesema Rais samia atoa.

Wapo mbona watu wanatoa fedha zao kufanya ujenzi au ukarabati? Ndio maana nikauliza kwa Rais samia possible ametoa za kwake mfukoni.
 
Hizo hela ni za wananchi au za rais mbona upambe umekuwa mwingi hela ni za wananchi sio za rais
 
Tz bado kiswahili kinatubabaisha, unashindwa kusema serikali imetoa???

Nadhani siyo shida ya Kiswahili, bali upungufu akili. Ukikosa akili, huwezi kujiamini, itabidi uwe chawa na kuandika hata yasiyokuwepo.

Kule Uganda, wakati wa utawala wa Kabaka, kuna machifu waliwahi kutamka kuwa hata hewa wanayoivuta waganda ni mali ya Kabaka. Angalao hao ilikuwa miaka ya 1800, lakini sisi tunao akina Mwashambwa and the like, kwenye miaka hii!!
 
Kila kona kuna kilio cha uharibifu wa miundombinu iliyosababishwa na mvua iliyonyesha kwa takriban miezi miwili sasa. Uharibifu huu haukutarajiwa na Serikali ni mambo yasiyotarajiwa. Binafsi naipa pole Serikali yetu kwa haya yaliyotokea na hayakurajiwa. Ninaishauri Serikali kuwa ione uwezekano wa kufuta baadhi ya miradi iliyotengewa fedha kwenye bajeti na fedha zitakazopatikana zielekezwe kwenye kurekebisha miundo mbinu iliyoharibika. Mfano fedha zote za REA, miradi ya maji yote haya yafutwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…