Jumba lile la kariakoo ni la gorofa, serikali inapeleka gari la zima moto la kuzimia nyumba za walala hoi kwenda kuzima jumba la gorofa,hivi hamuoni ? Ni kweli mna macho hamuoni na mna masikio hamsikii ,yaani hata katuni inaonyesha gari za zima moto zina ngazi kwa ajili ya kuzima moto kwenye magorofa ,sasa kama kule juu kungekuwa na watu na moto unawaka kati mngefanyaje ,Serikali ya CCM jiongezeni Nchi sasa ina magorofa.
Kama haitoshi viongozi wakuu wa nchi kibao wamefika nafikiri kuona au kuangalia moto lakini sio katika juhudi za kuuzima ,kasoro Raisi tu ndio hakufika labda alikuwa mbali au na dharura.
Maneno na maelezo kibao,kuna mwananchi kasema hapahitaji siku saba siku tatu tu ,wangejua kilichopo,ametokeza kwenye Globo TV,Waziri nae amekuja na sera za kujenga soko jipya,watu wamepoteza mali unawambia tutawajengea soko jipya sijui tutaweka fire extinguisher na kuchimba visima, hivi mle sokoni hamna hizo kariakoo nzima hamna visima vya water lines interception, CCM bana mnaboa ile mbaya.
Sasa mmeunda Tume kuchunguza,ngoja tusubiri watakaotolewa kafara!