Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Katika hali isiyo ya kawaida wawakilishi wa Serikali katika msiba wa Ally Mohammed Kibao uliofanyika jijini Tanga wamekumbana na zomea zomea wakati wakitoa hotuba zao.
Zomea zomea hiyo ilianzia kwa mkuu wa mkoa wa Tanga, Batilda Buriani baada ya kusema kifo cha Ally kimewahuzunisha kama Serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Batilda Buriani akitoa hotuba kwa niaba ya Serikali kwenye msiba wa Ally Mohammed Kibao
Waombolezaji walianza kupiga kelele baada ya Batilda kutaka waombolezaji waachie vyombo vya dola vije na majibu ya nani aliyehusika kwenye mauaji hayo. Batilda alitoa mfano wa kisa cha ng'ombe kilichopo kwenye sura ya Al Baqara kinachoelezea mtu aliyefariki mpaka kupatikana mhusika akisema kinafundisha ikitokea huzuni kama iliyoyotokea watu wasiwe wa kwanza kunyoosha vidole na kuacha vyombo vifanye kazi kama Rais alivyoelekeza. Wananchi walizidisha zomeazomea.
Hali ilikuwa mbaya zaidi Waziri Masauni alipopokea kipaza sauti na waombolezaji walizidisha sauti ya kumtaka waziri Masauni ajiuzulu kiasi cha kushindwa kuendelea na dua yake mpaka aliposaidiwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kutuliza hali kisha kumalizia hotuba yake.
Pia, soma=> Tafrani yazuka msibani Tanga: Waombolezaji wakataa dua ya Waziri Masauni wakimtaka ajiuzulu