Katika hali isiyo ya kawaida wawakilishi wa Serikali katika msiba wa Ally Mohammed Kibao wamekumbana na zomea zomea wakati wakitoa hotuba zao.
Zomea zomea hiyo ilianzia kwa mkuu wa mkoa wa Tanga, Batilda Buriani baada ya kusema kifo cha Ally kimewahuzunisha kama Serikali.
View attachment 3091388
Waombolezaji walianza kupiga kelele baada ya Batilda kutaka waombolezaji waachie vyombo vya dola vije na majibu ya nani aliyehusika kwenye mauaji hayo. Batilda alitoa mfano wa kisa cha ng'ombe kilichopo kwenye sura ya Al Baqara kinachoelezea mtu aliyefariki mpaka kupatikana mhusika akisema kinafunsha ikitokea huzuni kama iliyoyotokea watu wasiwe wa kwanza kunyoosha vidole na kuacha vyombo vifanye kazi kama Rais alivyoelekeza.
Wananchi walizidisha zomeazomea.
Hali ilikuwa mbaya zaidi Waziri Masauni alipopokea kipaza sauti na waombolezaji walizidisha sauti kiasi cha Masauni kushindwa kuendelea na hotuba yake.