Seti Mbili za Treni ya Umeme na vichwa 8 vya Umeme "Samia Express" vyawasili Nchini

Eti samia express utafikiri katoa hela zake mwenyewe kumbe ni kodi zetu na mikopo tunalipa wenyewe....Hii ni akili matope kabisa ya mwafrika.....
 
Siasa za hovyo hadi kwenye treni. Samia sio jina la kiserekali, je aliyeliweka hapo alikuwa na lengo gani hasa?
 
Alie tungisha mimba ni mwingine kabisaa! Huyu Analazimisha mtoto aonekane wake kwa mbwembe! Na madoido! Mingi!
 
howo tunaziita zuchu, hizi tunaziitaje?
 
lazima tukubali kuwa magufuli alithubutu kwa kuianza hii miradi mikubwa lakini pia mama samia naye anastahili pongezi zake kwa kuhakikisha inakamilika, tatizo la nchi zetu mara nyingi mkuu wa nchi habanwi kutekeleza ya mtangulizi wake rejea bandari ya bagamoyo.
 
Ni muhimu sasa wenzetu wa vyama vingine walionesha uzalendo wakugania taifa lao mfano Tundu Lissu, Chungaji Mtikila, Mpina n.k majina yao yawe kwenye miradi kama hizo treni n.k. haiwezekani Shule iitwe samia, treni samia, daraja magufuli, treni magufuli n.k.
 
Mods wa jf ni wapuuzi sana, yaani mada imefika ukurasa wa 4 mnakuja kuunganisha na Uzi unaoanza? Hovyo kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…