SGR ikikamilika Bila Bandari ya Bagamoyo malori yatalazimika kupaki

Unalazimisha sana kuwa tutapata faida, wewe unalipwa kuipigia chapuo hiyo bandari!? Huo uhakika wa faida umeutoa wapi!?
Ajira kwa vijana,

Kukuza Uchumi,

Kuongeza idadi ya mizigo,
 
Hakuna anayelalamika kuhusu ujenzi wa bandari ya Bagamoyo. Wana siasa mkiwa na jambo lenu huwa mnalazimisha sana. Ni hivi, watu wanataka kujua vigezo na masharti za huo mradi. Hakuna anayetaka kuona nchi inakuwa mateka sababu ya maamuzi ya haraka au mabaya, wakati kuna kila sababu ya kujiridhisha na kuamua vizuri.
Ubabe na kulazimisha kumeshagharimu mambo mengi kwa walipa kodi wa nchi hii. Kuna shida gani wakitaka kujua nini kinachoendelea nyuma ya pazia?
Waswahili wanasema, mficha maradhi, kifo kitamuumbua. IPTL ni moja ya dhambi kubwa walizotendewa walipa kodi wa nchi hii, ingawa kuna watu wanaona ni sawa tu na hakuna tatizo lolote.
Yes, Bandari ya Bagamoyo..ila kwa vigezo na msharti gani???? Tukumbuke, nchi yetu ina watu mil 60 na wanaendelea kuongezeka. Udalali unafanyika ila tusisahau watanzania hawa ipo siku watawajibika sababu ya maamuzi yanayofanyika sasa na hata baadae
 
Acha porojo. Maroli lazima yapige kazi. Network ya reli ni ndogo mno. Bado usafiri wa maroli ni wa thamani sana kila siku
 
Angalia na uhalisia mkuu, bei ya kubeba gunia la mahindi kwa treni ya sasa ni balaa kama unatoa mahindi kigoma mpaka dar. Wakiweka hiyo ya umeme wataanza kuweka bei zao za ofisini na hakuna mtu atatumia hizo chuma nakwambia.

Pili biashara ya serikali ni ngumu mnoo kwa uendeshaji wake.
 
Well said, kwa kifupi kujikite kuunganisha miindo mbinu na jirani kwa kuiunganisha na reli ya SGR. mfano Rwanda, Burundi, Congo. Pia kuenga bandari kavu pale RUVU ili kupunguza msangamano wa mizigo bandarini hapo kazi kwisha Bagamoyo ni kutuongezea mzigo wa madeni usiyokuwa na tija. Rais angejikita kutafuta pesa ya kumaliza miradi ikubwa aliyoachiwa na JPM km SGR NA MWL NYERERE HYDRO POWER. kwisha.
 
Hiyo Mizigo ya Bandari ya Bagamoyo itatoka wapi?
Hiyo mizigo ya Bandari ya Bagamoyo itatoka wapi?
 
Umeongea vitu vizuri Sana
 
Ni nani amekuambia bei ya kusafirisha itakuwa ndogo kwenye SGR? Mbona mnasema ndege ni zetu lakini nauli yake ni kubwa kuliko ilivyokuwa ya fast jet? Acheni utapeli wa kijinga. Reli yenyewe hata kazi haijaanza na haifahamiki inakamilika lini.
 
No ,Mimi nimewapa tu kaufunuo kahapo baadae

Mnapopinga ujenzi wa bandari na hili mlijue linawahusu
Mku Bandari ya Bagamoyo ni nzuri wala hakuna anaepinga maendeleo. Shida ni hayo masharti tu basi. Kwanini Serikali isifikirie kujenga kwa mpango wa "PPP" yani (Public Private Partnership ) ili ikiisha tu, mwekezaji na serikali waanze kugawana mapato since day one labda kwa 70% mwekezaji na Serikali 30% au vyovyote vile mpaka mwekezaji arudishe pesa yake yote ndo waachane-mwisho wa ndoa.
Kusiwe na masharti yoyote maana wote serikali na mwekezaji wameona kuna fursa. Tuachane na masharti .
 
Malori yaende vijijini kupeleka bidhaa na kuchukua malighafi kwa ajili ya viwanda. Shida iko wapi?
 
Kama kuna kitu umenifungua macho basi ni hii logic

Kwa hesabu hii ni kweli Malori karibu yote yatapaki

Mungu mbariki Samia wetu,
Aliyekwambia mizigo yote inayopakuliwa bandari ya dar inaenda mwanza tu Nani?
 
Mizigo inayokuja bandarini dar inakwenda along the central line tu mpaka malori yapaki? Ile inayowenda Zambia, Malawi, Mbeya Iringa, Kilimanjaro Arusha, Tanga Manyara?
Mleta mada hajui kufikiria vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…