SGR Mchakato wa Nauli ndiyo huu hapa, mtoto hadi Moro kulipa Tshs 12,400

SGR Mchakato wa Nauli ndiyo huu hapa, mtoto hadi Moro kulipa Tshs 12,400

Usafiri wa treni ulipaswa uwe cheap kuliko bus sababu hii ni mali ya uma na kila mwananchi anamchango wake hivyo ilipaswa iwe ni biashara yenye mrengo wa huduma ili kuchochea maendeleo.
 
Eleweni nyie wapumbavu treni ya abiria siku zote huwa hailipi huwa wanatoa huduma,wanajilipa kwenye tren ya mizigo na ndio lengo la ujenzi wa reli.
Wape elimu ya bure. Watanzania ni watupu sana kwenye elimu ya msingi ya uchumi. Faida kubwa ya treni na meli hutokana na mizigo sio usafiri wa watu. Kwa usafiri wa watu ni huduma tu.

Kutokana na kutojua uchumi msingi, ndio maana watanzania wengi wanajaribu biashara kibao na wanaangukia kichwa.
 
mwisho wa siku wabinafsishe.
Na ndio lengo. Nyie watanzania mtajifunza lini kuwa serikali haifanyi biashara? Kama mwendo kasi hata hii huko mbele itabinafsishwa ili serikali ikajikite zaidi katika matibabu, elimu, maji na huduma nyingine.

Anza kujichanga ili wakati huo ukifika, uweze kununua angalau mabehewa kadhaa, badala ya kulalamika lalamika.
 
Usafiri wa treni ulipaswa uwe cheap kuliko bus sababu hii ni mali ya uma na kila mwananchi anamchango wake hivyo ilipaswa iwe ni biashara yenye mrengo wa huduma ili kuchochea maendeleo.
Kama ulikopa kupata SGR ni lazima uchangie kulipa. Maendeleo yana gharama zake. Si siri kuwa SGR imejengwa kwa mkopo.
 
Mkurugenzi mkuu wa TRC ndg Kadogosa alikuwa akiongea na kamati ya bunge walipotembelea mradi huo na kusema "Kuhusu mchakato wa nauli, sisi TRC tumemaliza sehemu yetu ambapo tumewasilisha kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA) kila kinachohitajika."

View attachment 2948956

Alisema wanaelewa kuwa LATRA tayari imeshafanya vikao na wadau wa Dar es Salaam na Dodoma.

"Tunaamini kwamba kabla ya kuanza kazi Julai mwaka huu, tutakuwa tayari tumetangaza nauli," Kadogosa aliongeza.

LATRA imepewa jukumu la kudhibiti sekta ya usafiri wa nchi kavu, haswa usafiri wa barabara, reli, na waya. Ina mamlaka ya kukagua na kuweka viwango na malipo.

Kando na hayo, pia inawaidhinisha madereva wa treni na wafanyakazi wa treni. Mwaka 2022 LATRA iliwaalika wadau wa sekta ya reli na wananchi kwenye mkutano wa kujadili mapendekezo ya nauli kwa kuzingatia nauli za abiria kwa treni ya SGR kutoka Dar es Salaam-Morogoro-Dodoma-Bahi kwa ombi la TRC.

Nauli zilizopendekezwa na TRC kutoka Dar es Salaam-Morogoro zilikuwa kwa darasa la tatu 24,794/- kwa mtu mzima, na 12,397/- kwa watoto kati ya umri wa miaka 4-12.

Kwa Daraja la Uchumi, njia hiyo hiyo ilikuwa 29,752/- kwa mtu mzima na 14,876/- kwa watoto. Kwa darasa la tatu kutoka Dar es Salaam-Dodoma 59,494/- kwa mtu mzima na 29,747/- kwa watoto kati ya umri wa miaka 4-12. Darasa la Uchumi 71,392/- kwa mtu mzima na 35,696/- kwa watoto.

Kwa njia ya Dar es Salaam-Pugu, daraja la tatu 4,694/- kwa mtu mzima na 2,347/- kwa watoto kati ya umri wa miaka 4-12. Walipendekeza 5,632/- kwa kila mtu mzima na 2,816/- kwa watoto ambao wangependelea kutumia darasa la uchumi kwa njia sawa.

Mwenyekiti wa Bodi ya TRC, Ally Karavina, alieleza kuwa ana imani na majaribio yanayoendelea na alisema treni hizo zitaanza kufanya kazi Julai mosi kama ilivyoagizwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Africa kuna shida kubwa sana.

Hii miradi imekula pesa nyingi za Wananchi lakini haitaleta nafuu yoyote kwa wananchi
 
Dunia nzima usafiri wa train ni rahisi kuliko usafiri wowote na sababu ziko wazi kwakuwa train inabeba watu wengi na mizigo mingi inapunguza gharama za uendeshaji, sasa ni lazima waweke bei chini ya usafiri wa ndege au magari hii itachochea sana wingi wa abiria na mizigo na hata parcels ndogo ndogo waweke utaratibu wa mzuri watabeba soko lote wafanye wepesi bila urasimu yaani service bora kuliko waliopo. Itasaidia kuwa na train kwa siku hata mara 4 na kila trip zikiwa nyingi gharama za operation zinashuka. Wasiliuwe shirika kama walivyofanya reli ya kati na Tazara.
Sababu nyingine ni usafiri wa uhakika matengenezo kidogo
 
tatizo sio pesa spidi na mda. ndio tatizo
Sawa Huo UMEME wanao Unajua kuna vitu vyengine havitaki kuiga vinataka uthubutu TZ tatizo letu ni Umeme na Maji ndio tataizo SUGU .Hii Treni ilitakiwa iwe ya kisasa zaidi with very high speed n wangalifanya step by step Wengeanza Dar to Moro tu kwanza halafu wakaanza na mkoa mwengine sio kukurupuka tu .tumeona Dubai jinsi gani wamejenga Metro yao hawajakurupuka tu .
 
Kiuhalisia katika kufanya majaribio, wameweza kufunga mabehewa 14 yenye uwezo wa kubeba abiria 957. Sasa kama nauli ikiwa ni 10,000/ maana yake ni Tshs 9,570,000/ kwa safari moja. Na nilimsikia mkurugenzi mkuu akisema gharama ya umeme walitumia Tshs 360,000/ kwenda na kurudi Moro. Kama treni ikiweza kufanya safari kumi kwa siku, hii ni kama 9,570,000/ mara 10 ambayo ni 95,700,000/ kwa siku. Mbona watapata fedha nyingi!?
Kwa Dar Morogoro haitajaa hata Nusu.

Watu wanapita morogoro ila sio Destination yao.
 
Dar Zenj tu hapo, tena umbali chini ya maili 40, nauli ni kati ya 30k hadi 100k, kwanini tunaona shida 20k kwa Morogoro kama safari itachukua saa 1.30 kweli?
Hata meli wanawapiga sana wazenji kwa sababu hakuma Mbadala.....ila kwa treni mbadala ni uwanja mpana ikiwemo hadi bodaboda, Guta na bajaji
 
Kiuhalisia katika kufanya majaribio, wameweza kufunga mabehewa 14 yenye uwezo wa kubeba abiria 957. Sasa kama nauli ikiwa ni 10,000/ maana yake ni Tshs 9,570,000/ kwa safari moja. Na nilimsikia mkurugenzi mkuu akisema gharama ya umeme walitumia Tshs 360,000/ kwenda na kurudi Moro. Kama treni ikiweza kufanya safari kumi kwa siku, hii ni kama 9,570,000/ mara 10 ambayo ni 95,700,000/ kwa siku. Mbona watapata fedha nyingi!?
Hilo ndio linafikirisha na kuona jinsi viongozi wetu vinavyowaza. Wanawaza kuongeza gharama za maisha ya watu wao badala ya kuwarahisishia. Treni ya dizeli ambayo uendeshaji ni ghali kwa ajili ya kutumia dizeli nauli iwe rahisi kuliko hii SGR ya umeme! Akili gani hizo?
Yaani kwa viwango vya nauli wanavyopendekeza, hii reli na treni yake zitakuwa hasara tupu. Nani aende Dar - Moro kwa shilingi 20,000/= plus? Tusishangae kila mwaka watakuwa wanatutangazia hasara.

Vv
 
Akina Abood na Shabiby wala hawana haja ya kuwa na wasiwasi kamwe 🚮🚮🚮

Screenshot_20240424_150701_WhatsApp.jpg
 
Back
Top Bottom