SGR Mchakato wa Nauli ndiyo huu hapa, mtoto hadi Moro kulipa Tshs 12,400

SGR Mchakato wa Nauli ndiyo huu hapa, mtoto hadi Moro kulipa Tshs 12,400

ni pale serikali inapotaka kufanya biashara badala ya kutoa huduma....pole sana serikali ya JMT
 
Eleweni nyie wapumbavu treni ya abiria siku zote huwa hailipi huwa wanatoa huduma,wanajilipa kwenye tren ya mizigo na ndio lengo la ujenzi wa reli.
Ni wazi kwamba serikali yetu inaendeshwa na wendawazimu hayajielewi kwa kila yanachofanya
Hapo kuna harufu ya rushwa hakuna zaidi watu wasio na uwezo wa kufikiri wameona treni itakwamisha mabasi na malori kufanya kazi kama treni ikiwa cheap sana,
Rushwa imehusika katika hizi bei za nauli
Kuna watu ni takukuru wanalipwa ili kuhakikisha nchi haina rushwa lakini ni kama tu mabumunda

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Si walisema walitumia umeme wa laki tatu tu Dar-Moro! Bei hizo zinatoka wapi? Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kwa usafiri wa Treni kuwa ghali kuliko wa basi.
Kwa bei hizi, hata bwawa la Nyerere likizalisha umeme na ziada bei za unit itakuwa hizi hizi tu Wala hazitashuka. Hili taifa shida sana

Sent from my Infinix X6516 using JamiiForums mobile app
 
Kwa akili za wale matapeli wanaojiita manabii, "nazoom naona wafanyabiashara wa mabasi, nawaonw wameweka msisitizo nauli ya treni iwe juu kuliko mabasi"

"... kisha mbele kidogo naona mzigo kwa serikali kuendesha mradi huu utakuwa mkubwa na garama zitakuwa kubwa, hivyo naona CAG akitoa taarifa za hasara kupitia SGR, ndipo roho mchafu anayetawala sasa anasema mradi ubinafsishwe haraka sana kwa mwerarbeu"mbona walisha Sema kuwa mradi ni hasara? Kwaiyo anataka kujastifai tuuu
 
Kiuhalisia katika kufanya majaribio, wameweza kufunga mabehewa 14 yenye uwezo wa kubeba abiria 957. Sasa kama nauli ikiwa ni 10,000/ maana yake ni Tshs 9,570,000/ kwa safari moja. Na nilimsikia mkurugenzi mkuu akisema gharama ya umeme walitumia Tshs 360,000/ kwenda na kurudi Moro. Kama treni ikiweza kufanya safari kumi kwa siku, hii ni kama 9,570,000/ mara 10 ambayo ni 95,700,000/ kwa siku. Mbona watapata fedha nyingi!?
 
Wamewaletea usafiri wa haraka watu wasio na haraka🤣🤣😂
Labda waweke chakula na vinywaji iwe bure na ukitaka kubeba beba unaposhuka.
Lakini wasiweke pombe tuu,maana eeeh
Dar Zenj tu hapo, tena umbali chini ya maili 40, nauli ni kati ya 30k hadi 100k, kwanini tunaona shida 20k kwa Morogoro kama safari itachukua saa 1.30 kweli?
 
Dar Zenj tu hapo, tena umbali chini ya maili 40, nauli ni kati ya 30k hadi 100k, kwanini tunaona shida 20k kwa Morogoro kama safari itachukua saa 1.30 kweli?
Tatizo ni kwamba sisi wengi hatuna kazi maalumu zinazoenda na muda.
Mtu kwenye biashara yake hana malengo ya mwaka anafanya tuu biashara ilimradi, sasa huyu unadhani ataujua umuhimu wa treni ya express 🤔
Umasikini wa mfukoni na kichwani ni mbaya saanaa.
Atleast wangeweka dar to zenji wangeitumia wengi lakini sio wenyeji namaanisha watalii.
Maana mpemba kusafiri mke na mume plus watoto 5 mpaka 10 na lazima wabebe kuku,mihogo,samaki,ndizi na vibgine so isingewafaa
 
Serikali ikiendeshwa na wafanyabiashara neno HUDUMA huwa ni uhaini

Tutaendelea kupanda mabasi maana ndivyo TRC wanavyotaka. Nchi imejaa wapumbavu wengi kwenye nafasi za maamuzi
Na bahati mbaya hakuna mwenye uchungu na nchi kila mmoja anaamua kuchukua chake mapema, wajao waje warekebishe mapufungu watakayo yaona huko.
 
Kiuhalisia katika kufanya majaribio, wameweza kufunga mabehewa 14 yenye uwezo wa kubeba abiria 957. Sasa kama nauli ikiwa ni 10,000/ maana yake ni Tshs 9,570,000/ kwa safari moja. Na nilimsikia mkurugenzi mkuu akisema gharama ya umeme walitumia Tshs 360,000/ kwenda na kurudi Moro. Kama treni ikiweza kufanya safari kumi kwa siku, hii ni kama 9,570,000/ mara 10 ambayo ni 95,700,000/ kwa siku. Mbona watapata fedha nyingi!?
Unasahau gharama zilizotumika zinatakiwa lipwa
 
Back
Top Bottom