TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 14,747
- 24,250
- Thread starter
- #161
Bahati mbaya unatolea mfano eneo ambalo hulijui na hata ukijua bado unaweza kubisha.Dar Zenj tu hapo, tena umbali chini ya maili 40, nauli ni kati ya 30k hadi 100k, kwanini tunaona shida 20k kwa Morogoro kama safari itachukua saa 1.30 kweli?
Hapo baharini kuna makampuni zaidi ya mawili yanayotoa huduma ya usafirishaji abilia, zinazofahamika ni mbili tu, Azam marine na Zanzibar fast faries, sababu ndizo zilizopo.
Nauli (mimi) nilianza kulipa 15,000/- ilipanda hadi leo 30,000/- sababu ni uendeshaji na eneo hilo, hakuna ushindani ni hao wawili na hata mtetezi wa abilia hamna.
Mwaka jana wakati wa uzinduzi wa boat ya Kilimanjaro VIII, mmiliki aliomba serikali ifikilie kuwapunguzia kodi sababu ya uendeshaji ila majibu waliyopewa ni kuwa mbona hamjawahi kuacha kuangiza boat mpya kila baada ya miaka kadhaa, ina maana mnapata faida ila mwananchi hapati haueni.
So unatakiwa uelewe hakuna mfanyabiashara mwenye undugu na mteja, bado nauli ya 30,000/- ni kubwa na inawalipa sana hata ingekuwa 20,000/- ila kwa sababu hakuna namna nyingine lazima tutumie vyombo vyao, kuna meli za mizigo zinasafiri usiku kwa usiku hizi nauli ni 20-25,000 bado watu ni wengi wanazipanda.