Nimekaa nikangojea angalauwatu wawili au mmoja ajiulize maswali au ajaribu kuelewa maneno kadhaa kwa hizo screenshots zinamaanisha nini, lakini imebidi nikubali tu kwamba hapa JF watu hawapendi hata kujaribu kujadili kiutaalamu, watu wanapenda kushobokea tu bila ya kuelewa ni nini haswaa wanashobokea.....
Tuanze kitu cha kwanza unafaa muelewe, hapa wanaongelea treni wala sio reli.... hapo kwa kenya wanasema Trailing load of 4,000 tonnes on each train....
Je unajua maana ya trailing load???? Hii hapa maana yake.
---------
Trailing load refers to the maximum tonnage volume that can be hauled by a freight train and it depends on the propulsion strength of the locomotive being used. Indian Railways' freight trains currently carry a maximum trailing load of 3,900 tonnes. Indian Railways operates 10,500 locomotives to haul both passenger and freight trains at present.
----------
unaelewa maana ya trailing load???? kama hujaelewa hebu fikiria ki hivi, Kenya imejenga barabara nzuri, nzito na ya kudumu, lakini imenunua malori mengi yenye uwezo wa kadri.... Tanzania inapanga kujenya barabara ya kadri (Nitakueleza badae kwanini ni kadri) lakini inapanga kununua trela nzito zenye uwezo wa kubeba mzigo mzito... Sasa hebu nikuulize, ni barbara ya nani ndo itaharibika haraka na kuhitaji marekebisho kila mara?
Kwahivyo, kani ni ukweli walivyosema hao viongozi wenu... nashuku sasa umeelewa trailing load inamaanisha nini, kwahivyo kabla hata hatujaendelea, Geuza mada, Ondoa neno SGR na uweke treni/gari la moshi.... yani mada isome " Treni ya Kenya inabeba 4,000 wakati......"
manake SGR ni technology ya reli ambayo ni kitu tofauti kabisa na uwezo wa treni!
-----
Ukiangalia India hapo, india ni nchi ya tano duniani kwa uchukuzi wa mizigo kupitia reli, treni nzito zaidi walionayo, inabeba 3,900 tonnes pekee.. hii ni kwasababu treni ikiwa pale badarini, haiwezi ikanjojea mizigo yote ya wiki ipakuliwe kwa mpigo... Mizigo kadhaa ikipakuliwa unafaa uichukue na kuipeleka.... Hii inamaanisha huko Tanzania kama mtakua na treni za kubeba 10,000 tonnes kwa mpigo mmoja, itabidi treni ingojee kama siku mbili na nusu ndo ijae mizigo ya kutosheleza, itasababisha mizigo kuxhelewa iwe hata hakuna tofauti na lori likianza kupeleka huo mzigo na lori!-----
Angalia hapa, mchina ambaye ndo anabebesha mizigo mingi zaidi duniani kupitia reli, hii ndo average trailing load yao kwa kila treni
Average freight train carrying capacity in China 2014
This statistic shows the average weight of freights carried by trains in China from 2006 to 2014. In 2007, a freight train in China carried in average a load of around 3,200 tons.
View attachment 534606
Infact, nimepitia tovuti nyingi sana kabla niandike haya na nimeona kwamba treni zinazobeba mizigo mingi kwa mpigo, 90% ni za kubeba iron ore na madini mengine mazito
Germany heaviest train -6000tonnes
France 5,410t
Nchi inayoshikilia rekodi ya dunia kwa treni yenye mzigo mzito kabisa duniani ni South Africa... ilivunja rekodi hio mwaka wa 1989!!!!
Hii hapa treni yenyewe iliokua mbele kabisa ikivuta mizigo
treni yenyewe ilikua na urefu wa 7.2KM !(ya kenya ya sasa ni 880m), na ilivita mabehewa 660 yaliyobeba 91,000tonns!
South Africa's World Record Breaking Train! | The Heritage Portal
Kwahivyo hapo juu, yanayoongelewa ni umezo wa treni bali si uwezo wa reli... treni ni jambo dogo sana ukilinganisha na ujenzi wa reli yenyewe... Pesa zilizo tumika kwa kununua treni ni 5% ya pesa zote zilizotumika kwa ujenzi wa reli.... Kumbuka hata Kenya inampango wa kuweka stima kwa reli yake by 2020 na itabidi tununue treni zengine za kutumia stima, lakini reli yenyewe inatarajiwa kufanya kazi kwa miaka zaidi ya 100... kwahivyo uwezo wa reli ndo muhimu, na ikija kwa uwezo wa reli, SGR ya Tanzania mepitwa na mbali sana na SGR ya Kenya..
comparizon ya Kenya, Uganda, Ethiopia, Tanzania SGR, ilifanywa na Ministry of Transport UG
View attachment 534611
Angalia No 16 hapo Reli ya Tz itajengwa na umezo wakubeba maximum of 18 Million tonnes per year au ukitaka 18m/365days = 49,315 tonnes per day -Kwahivyo mkitaka, mnaeza nunua hata treni mbili tu za uwezo wa kubeba 20,000 tonnes each... ama ukipenda zaidi, muwe na treni moja tu yenye uwezo wa 50,000 tonnes ibebe mizigo yote kwa mpigo mmoja! lakini jambo la muhimu la kuangalia ni msipitishe zadi ya avg 49,315 tonnes kwa siku au 18Million kwa mwaka manake mkipitisha hapo, reli itakaribika kwa mda mfupi.....
Ukiangalia reli ya Kenya, design ya reli ni nzito, inaeza kubeba hadi maximum of 35Million tonnes kwa mwaka! au ukipenda 95,890 tonnes kwa siku, kwahivyo hata tukipenda tunaweza kununua reli ya urefu wa 7km na mabehewa 700 ya kubeba mizigo yote kwa mpigo mmoja..
Kwahivyo muache kelele nyingi bila vitendo,, mdomo mkubwa hata hamjaanza ujenzi, tulizeni boli kwanza... Wakuu wenu wameshaanza propaganda za kujilinganisha na reli ya Kenya, watanzania wenyewe hata hamjui kuchambua, mazombie kazi kushikilia chochote mnachoambiwa kana kwamba biblia/quran... Baada ya miaka 20 hivi wakati uchumi wenu utakua umekua hako ka reli kenu ka 18m tonnes/year katakua hakawezi kuwatosheleza mahitaji yenu tena, itabidi muengeze reli ya pili yenye uwezo sawa ndo mjitosheleze, wakati Kenya reli hio hio moja ya max 35m tonnes/year itakua bado iko na capacity ya kuongeza usafirishaji wa mizigo bila kuhitaji reli nyengine kujengwa