Shabiby yapata ajali usiku wa kuamkia leo, mmoja afariki

Shabiby yapata ajali usiku wa kuamkia leo, mmoja afariki

Msiwe mnaandika tu JF bila kufanya utafiti,kwa Idadi ya Mabasi yanayosafirisha abiria Nchi nzima kwa siku,ufinyu na ubovu wa barabara zetu hapa nchini,uchache wa Askari Polisi mabarabarani,NI UKWELI kwamba Ajali zinazotokea ni chache sana na hilo ni jambo la kumshukuru Mungu
Duuh ajali ni chache juzi ajali ya Kibaha leo hili bus aisee na unaona sawa...
 
Unaweza kukuta hilo lori liliharibika njiani pasipo kuweka alama yoyote ya tahadhali kwa hiyo, dereva wa basi akajua gari lipo kwenye mwendo kumbe limeharibika.
 
Kwa habari zilizotufikia ni kuwa gari ya usafirishaji abiria ya kampuni ya Shabiby Line, imegonga lori la kontena kwa nyuma na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

View attachment 2931158
Hapa itakuwa aidha basi lilikuwa mwendo kasi wakati mbele ni giza taa hazina uwezo wa kumulika mbali akabamiza Lori lililosimama au walikuwa wanafukuzana karibu karibu ambao ni mtindo wa madereva wa sasa bila kuwa na akili kuwa lolote linaweza kutokea. Yote kwa yote dereva amekwepesha kwake akagongesha kwa abiria .
Madereva wa mabasi ni wahuni .
 
Alikuwa anayaendesha au kuyazuia yasipate ajali?Bado mna hangover yake.
Ole wako RTO wa mkoa husika ajari zipatikane mara kwa mara kwenye mkoa wako ni lazima utaeleza tu

Kuna mambo alikuwa anakosea lakini kuna mambo mengine alikuwa anapatia

Kwa hili alijitahidi sana

Ajari zilipungua mnooo
 
Madereva wa mabasi huwa wanafunguka utadhani mabasi yao yakichina yana assistive braking yaani ile ikiona kitu mbele gari inasimama yenyewe, Kumbe yakitokea unasikia wakiita Mamaa... Mungu atujalie mwisho ulio Mwema na aliefariki apumzike kwa amani.
 
Madereva wa mabasi huwa wanafunguka utadhani mabasi yao yakichina yana assistive braking yaani ile ikiona kitu mbele gari inasimama yenyewe, Kumbe yakitokea unasikia wakiita Mamaa... Mungu atujalie mwisho ulio Mwema na aliefariki apumzike kwa amani.
Hii fani ya udereva imevamiwa na wahuni .
Hata matajiri wa mabasi wengi ni wahuni hawajali wameajiri mtu wa aina gani muhimu waletewe ela kila siku kulipa deni la benki .
Matajiri wachache wapo makini kuhusu madereva wao.
 
Mara chache sana Shabiby bus kupata ajali…. Sio kama chinja chinja zingine hizi.

Hapo dereva ataenda kwenye mahojiano na mkurugenzi moja kwa moja.

Pole yao.
 
Malori yaliyoharibika Barabani halafu halafu hawaweki kiashiria chochote chenye kuashiria kuwa kuna Breakdown mbele kama vile matawi ya Mti na unakuta hilo Lorry halina Reflectors au zimechakaa hazina mg'ao huyo Dereva na Helper wake wafunguliwe mashtaka ya Manslaughter.

Mimi ni Dereva wa Roli ninaeongea hivyo nimeshuhudia mengi.
 
Kwakua usiku inaelekea mwandishi hajua linakoelekea, hebu tuone jua limewaka huenda ataona lilikokuwa linaelekea.
Sidhani, ni usiku but picha imepigwa vizuri kabisa, angejiongeza kuuliza route ya hilo bas, bila shaka jamii iliyokusanyika hapo, wangempa jibu.
 
Swali zuri mtoa mada kakurupuka ndio maana sijachangia chochote
. Taarifa iliyo kamilika inasaidia sana, kujua baadhi ya mambo, tuna ndugu wengi wanasifiri kila kukicha, taarifa kama hizi zinahitaji kuletwa angalau nyama imejaa kidogo... Una ndugu yupo safarini unampigia simu hapatikani then unaingia JF unakutana na Habari kama hii ipo nusu maelezo.....
 
Back
Top Bottom