Shabiki mwezangu wa Yanga unakubali Morrison kurudi Yanga?

Shabiki mwezangu wa Yanga unakubali Morrison kurudi Yanga?

Nimrkuwekea wiki umekataa, nimekuwekea miaka iliyotajwa na club yako tuhesabu tuone kama tunapata idadi hiyo ya 27 nayo pia umekaa

Unaniletea mnyakyusa ama kweli imbombo jilipo
Wiki haijazungumzia ligi ya muungano ilikuwa katika mfumo gani. Kama kuna kipengele kinaelezea basi kiweke hapa. Hoja hapa ni kwamba tumeona Zanzibar ilikuwa na ligi yao iliyotoa wakilishi kucheza ligi ya muungano je huku bara hatukuwa na ligi yetu kutoa wakilishi kombe la muungano? Hivyo lete source yako unayoiamini ituambie mfumo wa ligi ya muungano ulikuwaje maana source yangu umeipinga.
 
Wiki haijazungumzia ligi ya muungano ilikuwa katika mfumo gani. Kama kuna kipengele kinaelezea basi kiweke hapa. Hoja hapa ni kwamba tumeona Zanzibar ilikuwa na ligi yao iliyotoa wakilishi kucheza ligi ya muungano je huku bara hatukuwa na ligi yetu kutoa wakilishi kombe la muungano? Hivyo lete source yako unayoiamini ituambie mfumo wa ligi ya muungano ulikuwaje maana source yangu umeipinga.
Mwqnzo ulikuwa ume stuck kwenye ligi ya bara

Nilipokuwa na mention premier league kwenye maelezo yangu ikawa inakupa tafsiri tofauti na ukanisisitizia kuwa niwe najikita kwenye ligi kuu bara

Nikakupa maelezo na reference kuwa nipo kwenye zone hiyo hiyo

Saizi tena una switch kutoka ligi kuu mpaka ligi ya muungano

Kiukweli sina references za ligi ya muungano nikipata nitaziweka

Ila nataka uniambie kile kilichoandikwa pale kwenye website ya yanga kina relate na ukweli kimahesabu au ni fix tu?

Ile miaka ukihesabu inafika 27?

Saizi unaniletea source ya tukuyu kwa mnyakyusa Kwanini club kuanzia mashabiki mpaka idara za juu za viongozi wote mnakuwa ni wahuni?
 
Hii nimeitoa kwenye official site yao ebu nisaidie kuhesabu hapo

View attachment 2223948
Baada ya maneno TANZANIA PREMIER LEAGUE, yanafuata maneno WASHINDI MARA 27. Ukihesabu miaka unapata 22. Hiyo kanzi data inajazwa na nani?
Na ukifuatilia kwa hakika katika miaka ni kama walivyoorodhesha hapo. Napata shida kuwaamini hawa watu.
 
Mwqnzo ulikuwa ume stuck kwenye ligi ya bara

Nilipokuwa na mention premier league kwenye maelezo yangu ikawa inakupa tafsiri tofauti na ukanisisitizia kuwa niwe najikita kwenye ligi kuu bara

Nikakupa maelezo na reference kuwa nipo kwenye zone hiyo hiyo

Saizi tena una switch kutoka ligi kuu mpaka ligi ya muungano

Kiukweli sina references za ligi ya muungano nikipata nitaziweka

Ila nataka uniambie kile kilichoandikwa pale kwenye website ya yanga kina relate na ukweli kimahesabu au ni fix tu?

Ile miaka ukihesabu inafika 27?

Saizi unaniletea source ya tukuyu kwa mnyakyusa Kwanini club kuanzia mashabiki mpaka idara za juu za viongozi wote mnakuwa ni wahuni?

1) Aliye andika hiyo article ame jichanganya uwezi kusema eti Malindi alikuwa bingwa wa Tanzania bara ilihali inajulikana Malindi sio timu ya bara.

2) ukipata kujua mfumo wa ligi ya Muungano ambao ilihusisha timu za kutoka Zanzibar ndipo utajua je Tanzania bara ilikuwa na ligi inayojitegemea au lah kama iliyokuwepo utupe orodha ya waliochukua kombe.

3) kilichoandikwa na Yanga kina relate na hesabu ndio, ila kosa lao ni kutoandika Mainland (Tanzania bara) na pia mwaka 2000 unatakiwa usiwepo maana hawakuwa mabingwa wa Tanzanian bara.

4) ili tufunge mjadala huu kwa upande wako uje na source yako unayoiamini wewe, itueleze mfumo wa ligi Muungano ilikuwaje. Je kila shirikisho (bara na Shirikisho la soka Zanzibar) kila mmoja alikuwa na ligi yake iliyotoa wawakilishi wa kombe la muungano au lah.
 
Mpira ni ajira, ni urafiki na sio uadui. Mpira ni kama siasa tu usichukulie serious sana mienendo ya wahusika.

Morrison akirudi Yanga lazima awafunge makolo fc.
Utopolo na wewe FA lazima mnyama akuweke
 
Kwa sababu yanga ni wataalam wa kula matapishi yao wenyewe sitashangaa BM akirudi. Binafsi nawapongeza Simba wameonesha kuwa hakuna aliye zaidi ya Simba. Simba Sc. Ni brand kubwa yeyote anayezingua ataondoka. Kama waliweza kuachana na Manara sembuse Morison? Yes, jamaa ni fundi wa mpira lakini utovu wa nidhamu hauwezi kuvumilika. Na ngoja arudi Yanga, atafanya atakachojisikia kwa sababu ni Yanga wenyewe ndio wanaomhitaji. Yeye binafsi hana shida na Yanga, na inajulikana kuwa anaipenda Simba Sc. Safari hii Yanga mtampeleka mpaka ICC sio CAS tena kwa atakavyowapelekesha
 
Benard Morrison ni kama Ex aliyeondoka kwa dharau sana na kila tulipokutana nae alitudhihaki.

Je, unakubali kumpokea Morrison katika klabu yetu tena? Morrison anaenda kucheza nafasi ya nani?
Morrison harudi Yanga, hizi habari sijui mmemezeshwa na nani
 
Wa nini huyo we Kolo? [emoji28]

Hatuna shida naye sisi.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] Nakupa za ndani Dada yangu MORISSON anarudi Yanga deal done hilo.....Chukueni zigo lenu [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kwangu Mimi it's ok!! Tunahitaji wachezaji wengi wenye uwezo wa karba yake je tunazo pesa za kuwapata??, Jibu ni hapana kama ni hapana huyu yupo na uwezo anao. Chukua funga mkataba mgumu kwake akileta ujinga kata mshahara!!.
 
J

yale maneno ya kuwa Yanga tuna tatizo la akili naliona linaukweli aisee.

Morrison kawapotezea muda viongozi wa Yanga.

Morrison kaiaibisha klabu ya Yanga kwa kuonekana klabu inamng'ang'ania wakati yeye kawakataa.

Morrison kaipotezea Yanga pesa kwa kufungua kesi CAS
Morrison kauumbua uongozi wa Yanga kuwa ni waongo na wababaishaji.

Mbali na hiyo tabia ya Morrison inajulikana kuwa ana tabia za hovyo. Hivi Africa nzima inamaana hakuna mchezaji anayemzidi au kulingana kipaji na uwezo Morrison?
Kwakuwa hayupo kwenu utasema mabaya yake. Sisi tumechagua kuangalia mazuri yake!!
 
Benard Morrison ni kama Ex aliyeondoka kwa dharau sana na kila tulipokutana nae alitudhihaki.

Je, unakubali kumpokea Morrison katika klabu yetu tena? Morrison anaenda kucheza nafasi ya nani?

Katika sehemu hii ya mwisho ya 10 ya mfululizo wa makala za mgogoro mkubwa uliowahi kuikumba klabu ya Yanga, leo tunahitimisha na wachezaji kutimuliwa ndani ya klabu hiyo na Pan Afrika kuanzishwa... Endelea



KATIBU Mkuu wa Yanga, Mohamed Missanga alitangaza kuwafukuza wachezaji wote 21 wa klabu hiyo walioshiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kule Mombasa, Kenya. Missanga alisema uongozi wao utaendelea kuheshimu mikataba iliyoingiwa na viongozi waliopita ukiwemo ule wa Kocha Tambwe Leya.

Wachezaji waliofukuzwa ni Patrick Nyaga, Juma Pondamali ‘Mensah’, Juma Shaban, Selemani Said, Jellah Mtagwa, Leodger Tenga, Omari Kapera, Ezekel Greyson, Sunday na Kitwana Manara.

Wengine ni Gibson Sembuli, Ahmed, Muhaji Muki, Ufunguo, Ramadhani Mwinda, Sam Kampambe, Juma Matokeo, Selemani Jongo, Ali Yusuf na Boi Idd Weckens.



ADVERTISEMENT
OFISI YA TAMBWE YAVUNJWA

Kocha Msaidizi wa Yanga, Athuman Kilambo naye amesimamishwa kutokana na kudaiwa kuhusuka katika uvunjaji wa ofisi ya Kocha Tambwe Leya.

Mbali na Kilambo, wengine waliodaiwa kuhusika katika tukio hilo la Desemba 10, 1975 ni wachezaji Himid, Omari Kapera na dereva wa klabu hiyo, Sixmund Komba. Mbali na kuvunjwa kwa ofisi hiyo inadaiwa vifaa mbalimbali vya thamani viliibiwa vikiwemo medali za kocha huyo yenye thamani ya Sh 1,750 vifaa vyake binafsi na vingine vya klabu. Kesi hiyo iliachwa chini ya upelelezi wa polisi.



SABA TU WARUDI

Katibu Mkuu wa Yanga, Missanga alitangaza kuwarudisha baadhi ya wachezaji waliofukuzwa ambao ni kina Mwinda, Ezekel, Selemani Said, Twaha, Ufunguo, Selemani Jongo na Ahmad.

Pia, mchezaji Moshi Dayan pamoja na kutokuwepo katika wachezaji walishiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati naye alikubaliwa kujaza fomu na kujiunga na wachezaji hao.



TAMBWE ATIMULIWA NCHINI

Februari 1976, Serikali chini ya Waziri wa Utamaduni wa Taifa na Vijana, Mrisho Sarakikya ilitangaza kuwafukuza makocha wa kigeni wanaofundisha soka Tanzania. Pia, Waziri Sarakikya alitangaza kupiga marufuku klabu yoyote kuagiza kocha kutoka nje ya nchi. Kutokana na amri hiyo, Makocha Naby Kamara wa Simba aliyetokea Guinea na Tambwe Leya wa Yanga aliyetokea Zaire (sasa DR Congo) walilazimika kuondoka nchini.



WACHEZAJI WAOMBA RADHI

Wachezaji takribani 14 wa Yanga waliofukuzwa waliandika barua ya kuomba radhi na kutaka kurudishwa kundini kuitumikia klabu hiyo lakini uongozi wa klabu hiyo ulikataa ombi hilo.

Barua hiyo ilitiwa saini na wachezaji wote isipokuwa Nyaga na Wickens ambao tayari walishaanza kuitumikia timu ya Mseto ya Morogoro.



WAJIUNGA NA NYOTA AFRIKA

Baada ya msamaha wao kukataliwa wachezaji hao walijiunga na Nyota Afrika ya Morogoro. Kasoro wachezaji Juma Nassor ‘Mensah’, Mohamed Rishard ‘Adolf’, Jaffar Abdulrahaman, Mohammed Yahya ‘Tostao’ na Gordian Mapango ambao walijiunga na Breweries ya Dar es Salaam.

Kitendo cha Nyota Afrika kuwapokea wachezaji hao kiliingiza klabu hiyo katika mgogoro na Yanga kwa kuwa zilikuwa na uhusiano wa karibu sana. Viongozi wa Yanga waliona kama wamesalitiwa na wenzao hao.



NYOTA AFRIKA MATATANI

Baada ya kuwapokea wachezaji hao na kuwachezesha katika Ligi ya Wilaya ya Morogoro, klabu ya Nyota Afrika ilijiingiza katika matatizo makubwa. Viongozi wa soka wa Morogoro waliichukulia hatua timu hiyo baada ya kuinyanyang’anya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mapinduzi kufuatia kuwachezesha wachezaji hao. Baada ya msuguano mrefu hatimaye wachezaji hao waliruhusiwa kuitumikia timu hiyo.



PAN AFRIKA YAANZISHWA

Agosti 1976 Klabu ya Pan Afrika ilisajiliwa Wilaya ya Ilala baada ya kukubaliwa usajili. Awali kulikuwa na pingamizi la kusajiliwa kwa klabu mpya ambalo liliwekwa maalumu kwa ajili ya viongozi wa zamani wa Yanga walikuwa wakihaha kutaka kuanzisha klabu yao.

Hatimaye, viongozi hao walikwenda kuzungumza na klabu ya Zamalik (Zama za Kale) ya Upanga jijini Dar es Salaam iliyokuwa timu ya maveterani waliokuwa wakifanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya zao.

Wachezaji wa kwanza waliounda Pan Afrika ni pamoja na kipa wa zamani wa Simba, Athumani Mambosasa.

Mambosasa alijiunga na Pan akitokea Nyota Afrika kwa kuwa lengo lake la kwanza ni kutoka Simba na kujiunga na Yanga. Hivyo akaondoka na wachezaji hao kwenda nao Morogoro. Wengine ni Ali Yusuf, Boi Idd Weckens, Nondo, Mikidadi, Muhaji Muki, Omari Kapera na Kitwana Manara. Pia, walikuwepo kina Juma Matokeo, Leodger Tenga, Juma Shaban, Gibson Sembuli, Jellah Mtagwa, Sunday Manara na Mohamed Migea. Wengine ni Zakaria Digosi, Idd Said China, Kivera James, Idd Sululu na Said Juma. Pia, kina Mohamed Hussein, Michael Mapunda, Ahmed Johari, Hassan Mohamed Mwangi, Kassim Manara, Adolf, Mohamed Tostao, Gordian Mapango, Jaffar Abdulrahaman, Mohammed Mkweche, Juma Nassoro Pondamali ‘Mensah; na Haruna Hemed. Awali Pan ilihifadhiwa na Kikundi cha Taarab cha Egyptian Mtaa wa Swahili na Mkunguni na baadaye kumiliki Jengo lake Mtaa wa Swahili na Mafia Kariakoo, Dar es Salaam. Mwisho.

ADVERTISEMENT
 
Back
Top Bottom