Pole kwa kwa kuuguliwa. Lakini nimpinge 'kuhamia' Simba, kwa sababu ni kitu kisichowezekana. Ni kama kutangaza kwamba sasa umehama kabila, hakuna atakayekuelewa. Mimi kuna timu inanitesa sana, kuna kazee kameng'ang'ania ukocha kwa zaid ya miaka 20, tunapigwa bao kama watoto yatima, lakin bado nipo nayo tu. Kila nikijifanya 'nahama' najikuta nimehama akili lakin moyo bado uko palepale.
Ushauri kwa Manara, aache kutumia shida za watu kujipatia umaarufu na mashabiki. Kuna clip anamwambia shabiki wa Yanga avue jezi ili ampe elfu 10. Ukitaka kupata thawabu kwa kumsaidia mtu, usimpe masharti. La sivyo itakuwa sawa na wale kina dada wanaopewa hela na wao kutoa tiba ya matamanio. Kama shida ni PR, fanyeni kama Mbeya City FC, chukua wachezaji kachangie damu wagonjwa hospitalini, kaoneni watoto yatima, kafagien masoko, tembelea shule kipindi cha michezo, nk