Shaffih Dauda: Hatuna timu yenye uwezo wa kubeba ubingwa wa Afrika kwenye nyanja zote, huo ndio ukweli


Yaani hapo tayari keshachambua mpira!! Mimi ningetarajia atuchambulie takwimu zilizijiri katika mechi ya kwanza hapa Dar, halafu azitumie kutuambia ni kwa namna gani Orlando ni wazuri kuliko Simba.
Ukweli ni kwamba achilia matokeo baina yao kwenye mechi, takwimu za mchezo huo hazikuonesha makali yoyote ya timu hiyo hata kuipa nafasi ya kusonga mbele. Ilizidiwa karibu maeneo yote!! Kamaq itasonga mbele si kwa sababu yenyewe ni bora zaidi, bali ni matokeo tu kuwa upande wao!! Ubora wa timu huonekana kwenye btakwimu za mchezo na si vinginevyo!!
Kama Simba itasonga mbele Shafii atasema "mimi sikusema hatasonga mbele bali nilisema hatabeba ubingwa wa Confederation cup"!! Kama isiposonga mbele atasema "si nilisema, hapo hakuna kitu" Ikitokea Simba ikabeba kombe la CAF atasema " mimi nilisema hawezi kubeba ubingwa wa Africa yaani champions league". Hawa ni wambeya wa soka hitaji lao kubwa ni kuganga njaa!! Ukimpa buku anakusema vizuri nk!!
 
Huyu akili zinatokaga na kurudi. Simba ikipita na kufanikiwa atakuja na sifa nyingi. Always anaenda na upepo bila kujua wadogo wanakua na wakubwa wanazeeka
 
Kabsa. Hawa ni watu ambao hatutakiwi kuwaamini na kuwapa nafasi ya kutuaminisha upuuzi wao. Sio kila wasemacho kina ukweli. Hisia zao kwenye jambo moja wanataka zituongoze kwenye kila jambo
 
kasema ukweli,lakini kwanini anasema hayo maneno leo hii asiseme tokea kitambo?
 
Kwa hiyo Petro Atletico kawekeza kuliko Mamelod
 
😁😁 Sasa unamwita Shafii Mnafiki ,hàlafu up nasema inawezekana Kwa asilimia Ndogo🤔
 
Kwahiyo tukubali kwamba msukule na Bumbuli wanatuona sisi utopolo kwamba ni hamnazo kweli. Maana kila siku wanasema wanasuka kikosi cha kuchukua ubingwa wa Afrika mwaka ujao halafu sisi tunashangilia kama mazuzu vile huku tukijua kwamba uwezo wetu huwa ni mechi mbili tu za hatua ya awali na tunagongwa nje ndani na kuondoshwa mashindanoni
 
Record hizo umezitoa wapi?
 
[emoji16][emoji16] Sasa unamwita Shafii Mnafiki ,hàlafu up nasema inawezekana Kwa asilimia Ndogo[emoji848]
Mimi nasema aslimia ndogo, yeye anasema haiwezekani kabisa, sasa huoni kama huyo ni chizi. Kwenye mpira kwanin isiwezekane wangapi wamechukua makombe timu zao zikiwa dhohoful hali.. Wigan sijui nani sikumbuki katwaa fa huku anashuka daraja.
 
Huu ndio ukweli
 
Simba haina uwezi wa kufika Nusu fainali, wakati yanga haina uwezo wa kufika hata hatua ya Makundu. Yes ni lazima tuukubali huu ukweli.
 
Mimi nasema aslimia ndogo, yeye anasema haiwezekani kabisa, sasa huoni kama huyo ni chizi. Kwenye mpira kwanin isiwezekane wangapi wamechukua makombe timu zao zikiwa dhohoful hali.. Wigan sijui nani sikumbuki katwaa fa huku anashuka daraja.
Mimi naona mna tofautiana padogo sana ,na huyo Chizi 🤭😁😋
 
Watu wabishi halafu team bora ni ile kila mwaka wanacheza league ya mabingwa sio shirikisho. Toka lini tumesikia Alahly wanacheza shirikisho? watu bora ni wale kila mwaka wako huko league ya mabingwa na wanapigania kombe sio lazima ashinde kila mwaka ila wako huko huwezi kuwa team bora uko huku division 2. Simba miaka ya karibuni wamejitahidi lakini hawako katika level ya kuja kutawazwa mabingwa wa Africa bado sana sasa kwa Simba unaweza kusema good show kwa Yanga ndio bado sana wanasafari ndefu sana kuvuka vile viunzi vya mwanzo na kwa team hii bado watapata shida sana. Mwisho wa siku maneno yana ukweli hakuna team Tanzania kwa sasa na miaka michache ya mbele kusema tuko tayari kupigania ubingwa achilia kuingia final tu. Je bahati zipo yes zipo hata ulaya inatokea lakini msimu mmoja tu huwezi kupata kama wale kina Al Ahly na sijui Raja kubadilishana tu. Ukweli mchungu ila bado sana tena sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…