Shahidi ashindwa kumleta Tundu Lissu Mahakamani Kisutu, Kesi yaahirishwa hadi tarehe 24 Septemba 2020

Shahidi ashindwa kumleta Tundu Lissu Mahakamani Kisutu, Kesi yaahirishwa hadi tarehe 24 Septemba 2020

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam Wanajamvi,

Tundu Lissu ameshindwa kuhudhuria kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi ya uchochezi namba 236 ya mwaka 2017 na ile namba 123 ya mwaka 2017 kutokana kuchelewa kukamilisha taratibu za urejesheji fomu ya utuzi wa kugombea urais wa Tanzania.

Leo tarehe 26 Agosti 2020 Wakili wa Serikali Mkuu Simon Wankyo akisaidiwa Renatus Mkude mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mbando wameeleza kuwa mtuhumiwa hakuhudhuria mahakamani hapo leo ikiwa wakili wake Peter Kibatala aliieleza mahakama kuwa Lissu amerejea nchi kutoka kwenye matibabu na kwamba amejiweka karantine kwa siku 14 pia aliiahidi mahakama kuwa leo angemleta Lissu mahakamani hapo.

Rose Moshi mdhamini wa Lissu ameieleza mahakama hiyo Lissu ameshindwa kuhudhuria mahakamani hapo kutokana na kuchelewa kukamilisha taratibu za urejeshaji fomu ya uteuzi kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambapo mchakato huo uliisha jana saa mbili usiku.

Upande wa jamhuri haukuwa na pingamizi lolote juu ya malezo hayo Hakimu Mbando ameahilisha shauri hilo mpaka tarehe 24 Septemba mwaka huu.

Kwenye shauri hilo Lissu anatuhumiwa kwa kutoa maneno ya uchochezi .

Inadaiwa kuwa tarehe 17 Julai 2017 Kinondoni Dar es Salaam, alitoa maneno ya kujaza chuki.

Maneno hayo ni kama ifuatavyo:

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ni ya kibaguzi wa kifamilia , kikabila, kikanda na kidini . Vibali vya kazi work permit vinatolewa kwa wameshenari wa kikatoliki tu huku madhehebu mengine yakielezwa kupanga foleni uhamiaji . Viongozi wakuu wa Serikali wanachaguliwa kutoka kwenye familia kabila na ukanda ...acheni woga pazeni sauti ...kila mmoja wetu...tukawaambie wale ambao bado wanampa msaada wa pesa Magufuli na serikali yake kama tulivyowaambia wakati wa serikali ya makaburu hii serikali isusiwe na jumuiya ya kimataifa isusiwe kisiasa, kiuchumi na kidiplomasia kwa sababu ya utawala huu wa kibaguzi...yeye ni dikteta uchwara.

Wakati huo huo shauri namba 123 la mwaka 2017 lilitajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Kassian Matembele.

Wakali Peter Kibatala ameeleza mahakama hapo kuwa Lissu ameshindwa kuhudhuria kwa sababu ya kuchelewa kukamilisha taratibu za urejeshaji wa fomu ya NEC.

Shauri hilo nalo limeahirishwa hadi tarehe 24 Septemba 2020.

Lissu anakabiliwa na tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi. Inadaiwa kuwa tarehe 11 Januari akiwa Kombeni mkoani Mjini Magharibi Zanzibar kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Diman anadaiwa kutoa maneno yenye udini na yenye kuchochea.

"Kwahiyo hicho kinachoitwa uchaguzi wa marudio uharamia mtupu, haramu, haramu ...kinachoitwa uchaguzi wa marudio ni haramu tupu nyie ni Waislam sana naomba niseme uharamu wa uchaguzi wa marudio wa mwaka jana hautofautiani na kula Nguruwe kwa wala nguruwe hawa nilikuwa nazungumzia yaliyokuja baada ya wala nguruwe hawa kufanya uharamia wao...laana tullah"

Nje ya Mahakama

Viunga vya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kulikuwa na ulinzi wa jeshi la Polisi.

Hapakuwa na mfuasi au mwanachama hata mmoja wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Zaidi, soma:
Kisutu: Tundu Lissu ashindwa kutokea Mahakamani, kesi zake zaahirishwa hadi 26/08/2020


1598433085131.png
 
Kwan kwenye kurejesha form akibeba chuma Kias achoke kiasi hiko ashindwe kufika Mahakamani!
 
Kumbe NEC walimchelewesha Mh Lissu kumtengezea mazingira mazuri kwa mahakamani? Nimeanza kuamini kuwa mushachoshwa na kufanywa vikaragosi. Taabani roho zenu. Mukimuendekeza mkuu wa Kaya mutapata erectile disynfunction kwa msongo wa mawazo!
 
Leo Agosti 26, 2020 Kesi Na. 123/2017 na Na. 236/2017 zinazomkabili Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama cha Demokrasi na Maendeleo Mhe. Tundu Lissu zilizoitwa leo mbele ya mahakimu mawili tofauti wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, zimeahirishwa hadi Septemba 24, 2020. Mtuhumiwa hakuwepo kwa sababu ya mchakato wa kurejesha fomu na uteuzi Dodoma.
images%20(67).jpg
 
Huyu hawezi kuongoza nchi.. kama ni muoga hata wa kwenda mahakamani..

Muda ufike akamatwe.. ushahidi upo kwamba hata hizo siku 14 hakukaa ndani..

Mgombea hawezi kuwania uraisi.. huku ana makesi kibao.. na hataki kwenda ili ayamalize..

Toeni oda akamatwe tu.. akichenga tena.. yajayo yanafurahisha na kajitakia mwenyewe.. uwakili wote.. akili hajui kutumia..

Kwa kuchelewesha ndio kajimaliza..

Magufuli 2020 💯
 
Maneno ya kisiasa hayo. Safari hii wamekuwa wapole sana hawa wanasheria wa serikali.
Wameanza kuwaza kuwa akiwa Rais wataenda wapi?Dalili ya mvua ni mawingu,picha inayoonekana vizuri ni kwamba Mh.Lissu atakuwa Rais wa JMT 2020.Lazima awe handled with caution.

Kukomesha uonevu na hujuma hizi,kesi zifutwe kwa heshima na tuanze maisha yasiyo na kuwindana kama wanyama mwitu.Mh.TAL for Tanzanians Precidency.
 
Back
Top Bottom