Shahidi wa pili kesi ya Mbowe, Bw. Kaaya afunga akaunti ya facebook baada ukweli kuhusu uachama wake wa CCM kuwekwa wazi mitandaoni

Shahidi wa pili kesi ya Mbowe, Bw. Kaaya afunga akaunti ya facebook baada ukweli kuhusu uachama wake wa CCM kuwekwa wazi mitandaoni

Huyu shahidi namba 2, kuna mengi sana nyuma yake na asipokuwa makini kwenye utetezi kuna viashiria vingi vya kumtia matatani pia
 
sile sms zinaweza kutengenezwa tu toka mtandao husika, sauti inaweza kuchongwa vile vile kama ile ya Mbowe eti kumtaka wema enzi zile...Ila Mbowe kweli Ukubwa jalala, kapitia mengi sana huyu MWAMBA.

Kwa mtu laini laini tayari kashanyoosha mikono juu mwendo wa mateka moja kwa moja Lumumba kusajiliwa... lakini ngoma IMEGOMA katu katu... huu ndiyo UANAUME.

Siyo unabinywa kidogo, kesho yake IKULU kuomba msamaha kwa machozi.
ebu kuwa serious kidogo.
 
You are the idiot one....Hujui hata tofauti ya mwanachama na shabiki!! Umeweka ushabiki wa kijinga mbele
Kosa lako ni moja tu!Kati ya Haki na Unafiki wewe umechagua Unafiki.So Tz huipendi.Najua ukiwa pekeako hapo unaujua ukweli ambao ata sisi tunaujua Ila ukija kwenye keyboard kusaka malipo unajitia uchizi, sometimes usijitie upofu kumbuka Kuna kifo na Kuna hukumu kwa Mungu.
 
We mfuasi wa kampuni ya Mbowe acha kuangaika usiku...mbowe atafungwa tu ni guide yule...mnakosea mnapo tafsiri hili swala la mbowe kisiasa...mbona ushahidi upo wazi sana kuliko hata zile kesi za Sabaya za kuunga unga ushahidi
Upumbavu mwingine bwana...tofautisha basi gaidi na guide!! Usiwe kama huyu fulishi

Polish: tulimkuta na bastola
M/sheria: mlimwuliza alipoitoa?
Fulishi: hapana
Fulishi: tulimkuta na madawa
M/sheria: alipotoa mmehoji?
Fulishi: hapana

Mytake - Kimsingi ninyi mnajua mlipotoa ndomana hamhoji!!

Fulishi: walitaka kulipua petrol station
M/sheria: mlimkuta na vilipuzi?
Fulishi: hapana
Fulishi: walitaka mdhuru jambazi 7baya kwa kemikali
M/sheria: mlimkuta nakemikali hizo?
Fulishi: hapana
My take - hahahahhhahhha
 
Kwa pointi yako ni kwamba Mtu wa karibu wa Mbowe (e.g. Mukya), hawezi kuwa shahidi wa utetezi? Sababu tu amekuwa karibu sana na Mbowe kwa muda mrefu? Unajua kwamba kuna kuapa mahakamani kabla ya kutoa ushahidi? Unajua kitu kinaitwa "Perjury"?
Wewe unajua mambo sana, hadi ‘Perjury’ unaijua, lakini ujinga wa kutunga kama hii kesi ambayo hata mtoto ndogo anajua, Wewe hujui!
 
Hii inaitwa kukurupuka na kukosa watu walio serious kwenye uandaaji na utetezi wa kesi ya jinai. Kwa mahakama zilizo huru na ambazo zinajitegemea kilichofanywa na shahidi wa pili kinatosha kumfunga au kutaka Chama cha mapinduzi kinachotuhumiwa kutumia Polisi na wanachama wa chama hicho kuidanganya mahakama kufika mahakamani kujieleza kuhusu utata uliojitokeza juu ya ushahidi unaoendelea.

Katika ushahidi uliotolewa shahidi huyu wa pili amekana kutokuwa na affiliation na chama cha siasa. Lakini jamii au public ambayo inamjua shahidi imesambaza Taarifa zake zinazothibitisha kuwa alikuwa kada wa CCM.

Jambo la pili shahidi huyu imethibitika kwamba alikuwa mwajiriwa wa Sabaya lakini walihitilafiana kisha akakamatwa na kubambikiwa kesi ambayo baadaye ilifutwa. Leo anasimama mahakamani kusema kwamba alishirikishwa na Mbowe kumdhuru Sabaya. Huu ni ukakasi wa pili kuhusu credibility ya mahakama kumruhusu mtu Kama huyu kusimama mbele ya Jaji akajitungia. Story.

Lakini kwa kiburi baada ya kuona ushahidi wake unakinzana na ukweli wa akaunti yake ya Facebook amedelete akaunti hiyo. Je, hao waliompanga walishindwa kupitia hata account zake za mitandao ya kijamii kuona zinavyoweza kuathiri kesi jhii hadi anafika kutoa ushahidi? Huu uzembe mkubwa hivi unaashiria nn kuhusu umakini wa vyombo vya dola?

Lakini pia huyu bwana aliajiriwa kuwa msaidizi wa katibu wa CCM longido na hata alipohitilafiana na Sabaya alirejea huko, je huko alikoajiriwa mwajiri alimwajiri mtu aliyekinyume na itikadi ya chama ?

Ila pia uhusika wa Pole pole, Bashiru, Gambo na Dagaro unamtenganisha vipi na chama Tawala?

Kitu chakushangaza wakati anakamatwa alikutwa na dola zakutosha na tshs zakutosha ambazo anadai alitoka kuuza mbogamboga lakini mtu huyo anayetembea na zaidi ya milioni mbili mfukoni anasema alikuwa akipewa shs elfu hamsini na Mbowe.......huu ugaidi huu

Hii Ni fedhea nyingine kwa mahakama na Serikali ,tengenezeni mambo yenye logic siyo watu wa aina hii ambao wamekaririshwa.
shida ni kwamba hata majaji na mahakimu wetu wanaendeshwa na wanafanya kazi yao kwa uoga sana. Huyu shahidi alipaswa awekwe custody mpaka kesi iishe au ahukumiwe on the spot kwa kitendo hicho. Lakini hiyo yote inategemea weledi na usimamizi wa haki wa jaji anayehusika.
 
Kosa lako ni moja tu!Kati ya Haki na Unafiki wewe umechagua Unafiki.So Tz huipendi.Najua ukiwa pekeako hapo unaujua ukweli ambao ata sisi tunaujua Ila ukija kwenye keyboard kusaka malipo unajitia uchizi, sometimes usijitie upofu kumbuka Kuna kifo na Kuna hukumu kwa Mungu.
Sorry kama umekwazika, problem watu wanajitia upofu kisa ushabiki!! Shahidi kasema yeye siyo mwanachama, hajasema yeye siyo shabiki! Ni nini hapo kigumu kueleweka?? Mwanachama anakuwa na kadi, yupo kwenye database ya chama, analipia michango, anashiriki vikao vya chama, na anauwezo wa kugombea nafasi yeyote ya uongozi ndani ya chama but anyone anaweza kuwa shabiki na hakuna popote pa kudhibitisha!! Ni kazi ya akina Kibatala kudhibitisha kama jamaa ni mwanachama or hapana, wakiweza kudhibitisha hilo ushahidi wa jamaa unakuwa void kwa sababu anakuwa kadanganya mahakama chini ya kiapo!! Mahaba kwa Mbowe yasiwatoe kwenye reasoning
 
Sioni haja ya wafuasi wa gaidi Mbowe kulialia humu,yule hatoboi,ambieni ndugu zake waanze matanga
Kauli zenu kwamba hatoboi kwenye hii kesi hazitofautiani sana na zile za kusema hashindi ubunge! Mnaonekana mna uhakika fulani wa jambo lenu! Na kwa mnavyo sisitiza hata mimi naanza kuwaamini!
Kitu kimoja tu ambacho inawezekana kwenye hi combination mtakuwa mmesahau, baada ya Mbowe kushindwa uchaguzi, March iliyo fuata kuna mbuyu uling’ooka!
 
Hii kesi imetengenezwa maalum kupoteza upepo wa kudai katiba mpya, ni kazi maalum ya TISs maana moto aliokuwa nao Mbowe kwenye kudai katiba ulikuwa hatar, kwahiyo wanachofanya sasa hivi ni kuwapotezea muda kina Mbowe na kuvuta attention ya raia kutoka kudai katiba kwenda kwenye kuguatilia kesi ya Mbowe na mwisho watawaachia watuhumiwa watakapoona upepo wa katiba mpya umepoa
 
Sasa hivi kila mwanachadema ni mwanasheria, duh!
Tulieni mahakama ifanye kazi yake.
Shahidi kuifunga akaunti yake ni hiari yake na haiingiliani wala kuathiri mwenendo wa kesi ya Mbowe.
 
Sasa hivi kila mwanachadema ni mwanasheria, duh!
Tulieni mahakama ifanye kazi yake.
Shahidi kuifunga akaunti yake ni hiari yake na haiingiliani wala kuathiri mwenendo wa kesi ya Mbowe.
Mwenye macho haambiwi tazama
 
Back
Top Bottom