Shairi: Aikael Mbowe, Freeman Mwamba wa Tanzania

Seif tutamkumbuka,kwa tabia ya uongo
Anapenda kucharuka,wakati moyoni fyongo
Siyo wa kuaminika,fitina mwenye mipango
Cheo alikitamani,kwa nadhiri ya mandevu.
 
Utampora mmoja,ila si kumi na tisa,
Walikaa kwa pomoja,wakaifanya siasa
Wakaenda kwa umoja,kujiapia vipusa
Hakuna aliyeporwa,wenyewe waliridhia
 
Seif tutamkumbuka,kwa tabia ya uongo
Anapenda kucharuka,wakati moyoni fyongo
Siyo wa kuaminika,fitina mwenye mipango
Cheo alikitamani,kwa nadhiri ya mandevu.


Huku nilikukaribisha. Hata hivyo nisiache kukupa vidonge vyako hapa pia:

Vita sasa mumo mumo, hongera bwana Hamadi,
Walidhani huna kimo, wakuchomeshe mahindi,
Itahitajika Omo, kuusafisha ushindi,
Ndani sasa yuko Sefu, pa kuficha pawe papya!
 
Hakuna haja ya vita,akae na kutulia
Atakunywa sunvita,hawezi tena fulia
Ya kwake yatamsuta,fujo alitarajia,
Katulizwa kama boli,adunde aende wapi ?

Katulizwa kama boli ,adunde aende wapi ?
Atalishwa na kacholi,tende halua na pipi
Hata akitaka mwali,mrefu hata mfupi
Ndani sasa yupo Sefu,lakini hafurukuti.
 

Kama we Mzanzibari, basi Sefu hana chake,
Vipi wewe lile gari, Dar siyo Chake chake?
Wamekupiga kabari, ulipe faini yake,
Wajifanya Mtunguja, Kumbe Matumbi wa Bara?

Kuwasemea wa Zenji, wewe nani kakutuma,
Makazi mnayafoji, Hali nyie wa Musoma!
Kuwa we si mkaaji, Mwayajengea Dodoma?
Sefu jembe la Zanziba, mmekwisha poteana

Sasa mwajifanya wao, kuwasemea wa Zenji,
Sefu ni mcheza kwao, atunzwa na wakijiji,
Sefu Yule mtu wao, Siyo wa kwenu Kimbiji,
Senzige wewe ni popo, kumbukumbu ni muhimu!

Linganisha:

Kwangu mimi ni Unguja,Nyumbani kwao Hussein
Hata bara ninakuja,kuongea ya chamani
Tunapanga yenye tija,vyote ndani ya ilani
Siraaj ng'aza siraati,tuondokwe na ghururi.


Pia hapa:

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…