Shairi: Aikael Mbowe, Freeman Mwamba wa Tanzania

Haujaisha na hautoisha ila Usaliti sisiemu na usaliti chadema ni vitu viwili tofauti. Hivi ni vyama viwili mbingu na ardhi, sisiemu ndio washika mpini wa kila kifaa cha kukatia.
Kweli kabisa CCM na CDM ni mbingu na ardhi, wasaliti wa CCM wakikamatwa wanapewa kesi za ML au uhujumu uchumi, kina Mdee wangekuwa CCM saa hizi wangekuwa wananyea ndoo segerea ila kwa Chadema katiba inafuatwa wako huru, that’s the big difference between the two parties.
 
Wakati ule Polepole alivyowaita wapinzani ni corona ili bonge la ishu ila sasa wenyewe kwa wenyewe wapinzani wanaitana covid 19(corona) halafu kawaida tu.
 
CCM imehangaika na CDM kuliko inavyohangaikia mambo na maduala ya chama Chao wenyewe .... hawajui chama makini ni mioyo ya wafuasi na wananchi wake ....
Tunasubiri tamko la dugai, Dpp, mwanasheri mkuu, NEC, TISs,

Sijui nani ataaza
 
Wewe mbona ccm wenu mumewahi wafutia uanchama halafu mkawarudsha kwani CDM ni dhambi wakiruhusu watu kutubu?

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Nimewaambia makamanda wenzangu kuwa tunachezeshwa kwata na ninyi (ccm) na sisi tunaingia kichwa kichwa..Hawa wadada siyowajinga wamepigania Chama na wanamchango mkubwa na watadai haki yao. Ninachokiona kwao iwe kwa msaada wa CCM au Mahakama watakuwepo Bungeni mpaka 2025. CDM yangu inapenda sana kushabikia mambo ya Kijinga na utoto
 
kumbe hata hukumwelewa vizuri, katiba ya chadema inasema"Mwanachama yeyote ambae hataridhika na maamuzi ya kuvuliwa uanachama wake ana haki ya kupinga maamuzi hayo" mbowe alinukuu kama ulifatilia alivyokuwa anaongea hakutoa mdomoni kwake.
 
Siku hizi tunaapishia gereji.
 
Unaota wakina mama wa CCM pengine CCM ilisha kufa kama una akili timamu utakuwa una lielewa hilo bila nguvu ya polisi na vyombo vya usalama CCM ilisha oza
 
Sasa Kawe ilikuwaje? Wanakaa wanaume tupu?
 
Ngoja miamba iungurume utajua ukweli huyo Simba Cha mtoto kumbuka picha ndiyo kwanza limeanza
 

Hizi naziita showing off ,Inaonekana huwalinda viongozi dhidi ya wapita njia walio vaa kiraia,Nikijivalisha magwanda ya UVCCM naweza kuondoka na kiongozi ,mfano hapo pichani,kiurahisi kabisa au nijivalishe magwanda ya kipolisi au nijidai ni usalama wa Taifa na kuonyesha vitambulisho feki,nina uhakika wa kuondoka na Mheshimiwa Mbowe mchana kweupe.
Ni mara ngapi Mbowe amechukuliwa kwenye hadhara ya watu ? Mbowe amewahi kushambuliwa,Lisu amewahi kushambuliwa na wengine wamewahi kushambuliwa na kutekwa,hakuna resistance yeyote hawa mabody-builder wanatoa au wana resist,mkuu anachukuliwa kibabebabe tu bila ya kutumia protocol za kiukamataji na wao hupigwa push wakasogezwa pembeni kama si lolote si chochote.
 
CCM imehangaika na CDM kuliko inavyohangaikia mambo na maduala ya chama Chao wenyewe .... hawajui chama makini ni mioyo ya wafuasi na wananchi wake ....
Umakini wake uko wapi? Kutoa matamko na kufanya maandamano , Chama hakina hata jengo la Ofisi kilichojenga huku kwa miaka mingi wakipata ruzuku na ndiyo maana jamaa hataki kutoka kwenye nafasi ya M/kiti ,yeye na genge lake wanakula na kutumia vibaya watu hawahoji Leo unasema Chama makini acha uhuni wewe bilashaka nawe Ni unanufaika na uhuni wa Mbowe na genge lake.Chadema ni Chama Cha kitapeli kimejaa wajanja
 
Naona umekomaa na Art pf war, hayo ni mawazo ya mtu binafsi muandishi.

Sasa kasome reality kwenye Bulshevick, go google.
 
Ni Kama ukurasa wa dhambi ndio umeanza rasmi. Nguvu za kibabe vs nguvu ya umma Sasa Ni dhahiri ligi Ni mbichi kabisa. Watawala wakitumia ubabe dhidi ya wanyonge wao . Kila upande wakijaribu kutumia kile walichonacho.
Wanyonge kweli watashinda? Swali gumu bado kwa sababu Kama Chadema walidai kuporwa ushindi Basi wababe serikali bado watahakikisha wanabana kote ili kusudi uhalali ubaki kuwa ulivyo kwa sasa
 
Akili ni nywele ila wewe unatumia vinyweleo.
Kuna watu wana influence na uwezo wakiwa upinzani ila hawana nguvu wakitoka upinzani.
Muulize Katambi,Silinde...Gekuli...Kafulila
Muulize Dkt Silaa influence yake iko wapi?
Angalia uwezo w Bulaya alivyojiunga na CDM uwezo wake ulikua mkubwa kupita kiasi .
Watapoteza mvuto kuliko unavyoamini.
 
Wahenga walisema usiku wadeni haukawii kucha. Yametimia. Ni juu ya suala la hatma ya Waliokuwa Wanachama wake 19 ambao wamefutwa kabisa uanachama kutokana na kuhujumu chama.

Maamuzi haya bila shaka yalikuwa yakisubiriwa kwa hamu sana kwa kuwa ilikuwa ni factor muhimu kuamua mwelekeo wa Chadema.

Aidha, wenye weledi walifahamu fika kuwa lengo la mradi huu ilikuwa kufanikisha mambo kadhaa kwa faida ya CCM, na Serikali ya Magufuli ikiwamo :
1. Kutengeneza mpasuko ndani ya chadema kupitia BAWACHA kwa kuhakikisha vipenzi vya wanachama wanaingia Bungeni.
2. Kuiondolea chadema na Uongozi wake uhalali wa kisiasa baada ya uchaguzi.
3. Kufifisha matumaini ya wanachama wake juu ya future ya chama chao.
4. Kufifisha dhana na madai juu ya uhalali wa uchaguzi mkuu 2020 , ukiukwaji wa haki za binadamu na mengine kadhaa yenye viashiria vya uvunjivu wa demokrasia.
5. Kuondoa uhalali wa harakati zinazoendelea katika jamii ya kimataifa kupitia watu mbalimbali. Harakati hizi zinalenga kuiadhibu Serikali ya CCM kwa njia kadhaa
6. Kutumia kete ya viti maalumu kama sehemu ya maridhiano ya kisiasa kwa kuunda Kambi rasmi ya Upinzani bungeni.
7. Kutengeneza picha kwa jamii za kimataifa kuwa hali ni shwari kwa lengo la kuvutia misaada na ruzuku zinazofuata mkondo wa inclusion democracy.

Hivyo basi kama kamati kuu ya chadema isingeweza kufanya maamuzi haya, chadema ingepata pigo kubwa kwanza kupoteza imani kwa umma, kukimbiwa na wanachama wake watiifu, kupoteza locus stand, uhalali wa kisiasa na zaidi kuipa dola nguvu ya kushughulikia wachache waliobaki.


Kwa maamuzi haya , yametuma ujumbe kuwa TOGETHER WE SHALL STAND.
VIVA Chadema, VIVA kamati kuu, VIVA Freeman Mbowe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…