Shairi: Aikael Mbowe, Freeman Mwamba wa Tanzania

Shairi: Aikael Mbowe, Freeman Mwamba wa Tanzania

Ameunguruma Simba, Nchi imetetemeka
Manyang'au yamevimba, Aibu imewashika
Yalijiona miamba, Ile isiyovunjika
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini....
Huyo si mwamba ni kamba,ukweli wajulikana
Yote hayo anaimba,mwisho atapatikana
Samahani ataomba,mkweli kujulikana
Ni mwamba aliyeshindwa,majeruhi toka Hai.
 
Katiba ya chama ndiyo inaruhusu, kuwa mwelewa kwenye mambo madogo basi, sasa ulitaka apingane na katiba ya chama?
Chadema haijaanza kufukuza watu leo wamefukunzwa wengi tu tukianzia kina Shonza na kina Zitto haya kipindi Zitto anafukuzwa katiba ilikuwa ubeberuni? au makosa ya kusaliti na kutaka mabadiliko ya kiuongozi ndani ya chama lipi kosa kubwa?

Acheni nyinyi Mbowe ni mjanja sana kuliko mnavyodhani yule jamaa ni mfanyabiashara ktk siasa leo wangekuwa wanafanya hujuma ya kumpindua yeye nakwambia wangefukuzwa na wala wasingepewa hyo nafasi ya kuomba msamaha .
 
Hongera sana Mbowe! Wewe kweli ni kaka baba na Mtoto wa taifa hili! Wewe ni zaidi ya Nyerere! Kwani mateso yote uliyoangushiwa na awamu hii bado umesimama na democrasia! Mungu akubariki!

Umesema kweli mioyo inawauma kuwafukuza watu kama Halima Mdee-a name to reckon with! Matiko Bulaya wote hawa mliwapenda na wengine wote!

Nadhani hata wao wanalia kuacha chama ila kuna jinamizi limewadanganya! Wakiamka kwenye huo usingizi watajikuta loh! Heshima yote gone with the wind!
Poleni Chadema!
Poleni covid 19!
Siku moja sisi wananchi mtatuambia ukweli ni upi!!
Chadema Aluta Continua!
 
kumbe hata hukumwelewa vizuri, katiba ya chadema inasema"Mwanachama yeyote ambae hataridhika na maamuzi ya kuvuliwa uanachama wake ana haki ya kupinga maamuzi hayo" mbowe alinukuu kama ulifatilia alivyokuwa anaongea hakutoa mdomoni kwake.
Mkuu hv chadema wameanza kufukuza watu leo? Kipindi anafukuzwa Zitto kipengele ambacho amenukuu cha katiba kilikuwa hakipo? Chama cha siasa si kama familia mzee Chadema wako ktk wakati mgumu kuliko unavyodhani mtaji wa chama si wanachama peke yake pia na wawakilishi Bungeni ndio mtaji wa chama cha siasa ndo maana vyama kama NLD,DP na Democrasia makini unavisikia kipindi cha uchaguzi tu.

Chadema wanaitaji sana uwakilishi Bungeni kuliko kipindi chochote kile na wakiruhusu wawakilishi wao waharibikiwe kisaikologia wataside upande wa CCM na pia chama kinaitaji ruzuku coz ndo kipato pekee walichonacho kwa kuendesha shuguli za chama
 
Mbowe Mbowe Mbowe Mbowe!!!!!!!!
Ngaka12 mbona mna hangaika sana na huyo kwamba????
Wafuateni wakina Mbatia ambao leo wako na wapinzani kesho wako kwingine!
Mwamba kasema hilo halitatokea!
Nenda kunywa moja harusi moja moto!!
Mwamba wa democrasia Tz!!
Ni Mbowe na Chadema!
Mbowe tangaza namba ya simu tuanze kuwachangia muendelee kujenga chama!
Pepozzzzzzzz!
 
Yani mtu anafurahia na kumpongeza Mbowe wala hafikirii zaidi ya hapo,hivi ikiwa hadi Mdee leo hii naye anaonekana msaliti na kwamba kavuta mpunga mnono na ccm, hivi ni nani aliyebaki huko upinzani ambaye tutasema ni wa kumuamini na hanunuliki ikiwa hata Mdee kafika dau? maana kabla ya haya maamuzi watu hawakuwa na imani na hata huyo Mbowe mwenyewe.
Mbowe kanyanganywa bilicanas na mashamba lkn hajasanda, lissu kapigwa mvua ya risasi na hajasanda, mpaka hapo bado hujapata wa kumwamini cdm enh?
 
View attachment 1636567
Hizi naziita showing off ,Inaonekana huwalinda viongozi dhidi ya wapita njia walio vaa kiraia,Nikijivalisha magwanda ya UVCCM naweza kuondoka na kiongozi ,mfano hapo pichani,kiurahisi kabisa au nijivalishe magwanda ya kipolisi au nijidai ni usalama wa Taifa na kuonyesha vitambulisho feki,nina uhakika wa kuondoka na Mheshimiwa Mbowe mchana kweupe.
Ni mara ngapi Mbowe amechukuliwa kwenye hadhara ya watu ? Mbowe amewahi kushambuliwa,Lisu amewahi kushambuliwa na wengine wamewahi kushambuliwa na kutekwa,hakuna resistance yeyote hawa mabody-builder wanatoa au wana resist,mkuu anachukuliwa kibabebabe tu bila ya kutumia protocol za kiukamataji na wao hupigwa push wakasogezwa pembeni kama si lolote si chochote.
hebu tafuta panadol na maji mengi unywe alafu tafuta sehemu yenye kivuli upunge upepo wenge liishe.
 
View attachment 1636567
Hizi naziita showing off ,Inaonekana huwalinda viongozi dhidi ya wapita njia walio vaa kiraia,Nikijivalisha magwanda ya UVCCM naweza kuondoka na kiongozi ,mfano hapo pichani,kiurahisi kabisa au nijivalishe magwanda ya kipolisi au nijidai ni usalama wa Taifa na kuonyesha vitambulisho feki,nina uhakika wa kuondoka na Mheshimiwa Mbowe mchana kweupe.
Ni mara ngapi Mbowe amechukuliwa kwenye hadhara ya watu ? Mbowe amewahi kushambuliwa,Lisu amewahi kushambuliwa na wengine wamewahi kushambuliwa na kutekwa,hakuna resistance yeyote hawa mabody-builder wanatoa au wana resist,mkuu anachukuliwa kibabebabe tu bila ya kutumia protocol za kiukamataji na wao hupigwa push wakasogezwa pembeni kama si lolote si chochote.
Kamchukue basi tuone!
 
Mbowe kanyanganywa bilicanas na mashamba lkn hajasanda, lissu kapigwa mvua ya risasi na hajasanda, mpaka hapo bado hujapata wa kumwamini cdm enh?
Kwani Mdee hakuwa akipitia misukosuko yeyote? kila kitu kina muda wake na mengine yanayoendelea hatuyajui.
 
Ameunguruma Simba, Nchi imetetemeka
Manyang'au yamevimba, Aibu imewashika
Yalijiona miamba, Ile isiyovunjika
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Hawa watu waonevu, Ni watu waso na soni
Matendo yao uovu, Na ghiliba za shetani
Mipango yao mibovu, Kaivunja Freemani
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Nchi imekuwa dampo, La uchafu wa wahuni!
Mambo wayafanya simpo, Kiburi cha Firauni
Wamejifanya madompo, hawamuogopi nani!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Aibu yetu au yao?, Huu ni msala wao!
Wasaliti wana chao?, Chao ni ujinga wao!
Wameuza utu wao, Kwa uchu tamaa zao!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Wananchi tunaona, Wananchi tunajua!
Hadaa tumeziona, Inda tunaitambua!
Mambo yao konakona, Akili zao vibua
Hongera sana Mbowe, wewe ni mtu makini!

Wewe umeona wapi, Dhulma ishinde haki?
Kwenye mwanga saa ngapi, Giza likatamalaki?
Maono yao mafupi, Kama yale mafataki.
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Hima sasa wananchi, Kamanda kaweka sawa
Hila zote kazipanchi, mambo sasa sawasawa
Hadaa kapiga tochi, wamebaki kupagawa
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini!
Huyu ni mwamba wa kweli,mwamba wa kuvuta zipu,
Ili akupe kibali,nawe umpe bakuli,
Bila hivyo hakubali,ni bora umpe supu
 
Wanaenda fungua kesi mahakama itazuia kufutwa kwao sababu kesi inasikilizwa na kesi itaenda mpaka 2025 na baada ya hapo wataenda sisiemu, loser ni chadema! Mdee, bulaya, matiko wana influence kubwa sana kwa kina mama, ambao ndio wapigaji kura wakubwa..

Barafuyamoto

Katika maisha yako ya ubinadamu, omba jambo moja tu muhimu..

Omba KIBALI na KUAMINIKA mbele za Mungu muumba wako na kisha kwa wanadamu wenzako...

Mungu muumba akikuheshimisha mbele zake, basi utakubalika kwake. Baadaye atakuheshimisha mbele za wanadamu...

Kuwa na vyote duniani, Mungu akikunyang'anya KIBALI na HESHIMA, you will never experience happiness, peace and love on earth...

Bila kujikana wenyewe maisha ni taabu tupu duniani...

Kitu kikikosa uhalali, kimekosa tu haijalishi utakipaka rangi nzuri ya namna gani...

The whole world knows kwamba, Tanzania kuna uhuni umefanyika na unaendelea kufanyika..

Badala ya sisi kama nchi tutafute amani na watu wote ili kujenga kuaminika, cha kuchangaza tunaendelea kufikiria namna ya kujizamisha ktk tope la uharibifu ndani zaidi...
 
Kwani Mdee hakuwa akipitia misukosuko yeyote? kila kitu kina muda wake na mengine yanayoendelea hatuyajui.
Kapitia akiwa mbunge, so ubunge ndo ulimfanya avumilie, kukosa ubunge miezi 2 tu kasanda, akina mnyika hawakuwa hata na haja ya kugombea, lissu tangu 2017 kapokwa ubunge na hajasanda yaani wa kutumainia chadema wapo wengi mno!
 
Umwamba wake ni upi? Kuzigawa mbao za mtumbwi(hao kina halima na wenzake au)? Mi naona uongozi wa saccos ni ma losers [emoji16] [emoji23]
Ruka sarakasi zote, tembea na makalio hapa hadi Burigi, harisha ugoro wote ila Mwamba ni Mwamba.
 
Ameunguruma Simba, Nchi imetetemeka
Manyang'au yamevimba, Aibu imewashika
Yalijiona miamba, Ile isiyovunjika
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Hawa watu waonevu, Ni watu waso na soni
Matendo yao uovu, Na ghiliba za shetani
Mipango yao mibovu, Kaivunja Freemani
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Nchi imekuwa dampo, La uchafu wa wahuni!
Mambo wayafanya simpo, Kiburi cha Firauni
Wamejifanya madompo, hawamuogopi nani!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Aibu yetu au yao?, Huu ni msala wao!
Wasaliti wana chao?, Chao ni ujinga wao!
Wameuza utu wao, Kwa uchu tamaa zao!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Wananchi tunaona, Wananchi tunajua!
Hadaa tumeziona, Inda tunaitambua!
Mambo yao konakona, Akili zao vibua
Hongera sana Mbowe, wewe ni mtu makini!

Wewe umeona wapi, Dhulma ishinde haki?
Kwenye mwanga saa ngapi, Giza likatamalaki?
Maono yao mafupi, Kama yale mafataki.
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini

Hima sasa wananchi, Kamanda kaweka sawa
Hila zote kazipanchi, mambo sasa sawasawa
Hadaa kapiga tochi, wamebaki kupagawa
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini!
 
Back
Top Bottom