Nakupa mfano wewe unaliyejitangazia laana sababu ya weusi wako.
Kuna mtu aliajiriwa kama dereva kwa cheti cha darasa la saba halali na akatumikia kwa miaka mingi tu katika mazingira magumu.
Baadae, kwa imani kuwa akileta cheti feki cha form 4, labda kipato chake kitaongezeka kidogo. Kama kiliongezeka, basi kidogo sana na maisha ya mtu huyu yakawa duni vile vile. Maana kwenye utumishi wa umma , mtumishi siku zote analipwa pungufu kwa kile alichokifanyia kazi. Aliyemuibia mwenzake hapo utajua wewe.
Anyway, Siku ya uhakiki, cheti chake feki kilicho kwenye faili lake, kinamfuta kabisa kazi jumla jumla na kuondoka mtupu na matusi juu. Familia yake inaishia kuteseka .
Nasema hivi, hukumu wewe moyoni mwako unavyoona inafaa ila waache wale wanamuogopa kweli Mungu na sio kwa maigizo wafanye yenye Haki. Glory be to God.