Shaka: Rais Samia kuwalipa waliofukuzwa kwa vyeti feki ni ishara ya huruma, upole na upendo kwa Watanzania

Walifanya kazi kwa moyo kuliko wenye vyeti halali.
 
Cheti ni official certification kuwa hicho kitu unakijua

Huwezi Omba kazi ya udereva leseni huna halafu unataka mwajiri akuamini tu kwa kukuangalia tu usoninkuwa wewe dereva

Halafu wewe Muongo ulaya na China vyeti huangaliwa sana mfano huwezi Tajiri daktar au mainjinia au rubani bila cheti au kuajiri Profesa bila cheti

Mnadanganyana vijiwe vya kagawa

Kuna kazi uchwara zisizohitaji vyeti hizo ndizo hupewa yeyote
 
Katiba ya ccm ya 1977 ni ya kipuuzi sana. Yaani inampa mtu mmoja mamlaka makubwa mpaka inakera.

Hakika Katiba Mpya haikwepeki.
Katiba ya CDM inakera sana haina ukomo wa madaraka ya m/kiti, na Hakuna mwanachama anayeweza kuhoji ukomo wa madaraka..na ukigusa tu hamaga chama.
 
Katiba ya CDM inakera sana haina ukomo wa madaraka ya m/kiti, na Hakuna mwanachama anayeweza kuhoji ukomo wa madaraka..na ukigusa tu hamaga chama.
Kwa bahati mbaya nchi inatawaliwa kwa kutumia Katiba ya ccm ya mwaka 1977, na siyo Katiba ya Chadema.

Kwa hiyo haya maelezo yako naweza kusema ni irrelevant!
 
Yani mtu ana vyeti fake analipwa wakati kuna vijana kibao hawana kazi na wanavyeti halali, sisi watu weusi kwakweli tuna laana flani hapa duniani si bure. 60 yrs of independence bado tupo hapa na siasa uchwara.
Kwa hili nasimama na Samia
 
Hivi hawa watu walifukuzwa na Chadema au?! Yaani Ccm huwa mna jikuna na kujitekenya wenyewe.
Ingekuwa busara mka waomba radhi mlio watimua..
 
Yani mtu ana vyeti fake analipwa wakati kuna vijana kibao hawana kazi na wanavyeti halali, sisi watu weusi kwakweli tuna laana flani hapa duniani si bure. 60 yrs of independence bado tupo hapa na siasa uchwara.

Taarifa haijasema wanaajirwa au wanarudishwa kazini. Bali wanalipwa Terminal Benefits ambazo walikwisha stahili hadi walipoachishwa kazi.

Wewe huelewi vizuri
 
Mama kwa hisani yako geuza shingo pia uwaangalie wazee EAC.Hakika hawa wazee hawakulipwa stahiki zao zinazostahili.


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kazi nzuri sana bwana Shaka,
 
Maza we wape tu, mwendazake aliwanyonga kuna watz tulipiga kelele hatari, but wewe umeshow love kwa hawa wahanga lkn kuna mitz inalalamika so Kaa ukielewa ngozi nyeusi hatunaga jema, we chapa kazi.
Nafikiri uzi huu ungeishia hapa tu.
 
Yani mtu ana vyeti fake analipwa wakati kuna vijana kibao hawana kazi na wanavyeti halali, sisi watu weusi kwakweli tuna laana flani hapa duniani si bure. 60 yrs of independence bado tupo hapa na siasa uchwara.
Nashangaa na mie hapa. Khaaah.
 
Hata Mkapa alifanya Ridandansi na kuwalipa na wengi wao waliendelea na maisha yao.
Lakini pia serikali isisite pia kufanya redandernce mana Kuna watu wengine wanastahili kulipiwa stahiki kutokana na Hali zao za kielimu kutoendana na wakati , mfano mtu aliajiriwa kwenye kumpokea simu za bosi lakini Sasa Kuna simu za mkononi Kwa kila biso au matatizo ya kiafya ili waajiriwe watu wengine wenye nguvu na ujuzi zaidi.Mtu mgonjwa Hana hata uwezo wa kwenda ofisini Kwa Nini asilipwe kiinua mgongo chake Kwa miaka 60 ili akapumzike badala ya kumwacha mpaka afe halafu familia yake ihangaike kufuatilia vihela kidogo mana itakua ni kuzungushwa TU.

Waliotumbuliwa wakati wa JPM sio wote wanastahili kulipwa kuna wengine wanatakiwa wafikishwe mahakamani ili mahakama iwasafishe au iwatie hatiani.
Atakayesafishwa na mahakama ndiye anayestahili kulipwa.

Mtu aliiba vyeti au alifoji huyo alistahili kufungwa sio kufukuzwa TU kazi Bali kuwa gerezani.

Kosa la JPM ni kuwafukuza na kuacha kuajiri wengine wenye vyeti halali.
Lakini kuwafukuza ilikua ni haki yao kabisa. Hatuwezi kuwa na Taifa la watu wezi wezi na wanaofoji foji kila kitu.

Kama Mama Samia ana pesa nyingi basi ni Bora akaanzisha Benki isiyokuwa na Riba akawakopesha Wafanyakazi au wanafunzi wa Chuo kikuu wakachulia mkopo Bila riba na wapewe mikopo wote 100% mana wanafunzi wengi wa vyuo ni watoto wa maskini hawana uwezo wa kulipa Ada za vyuo na mahitaji yote.
Hatutaki siasa nyepesi. Afute Riba kwenye mikopo ya Chuo na itolewe Kwa wote Kwa asilimia mia Moja.Hapo atakua amewakombia Watanzania lakini sio kuchukua pesa za umma na kuwapa watu waliofoji na kuliibia Taifa hili Kwa miaka hata iwe ishirini wahukuru.
Wanapaswa kutuomba msamaha Kwa kumpokea mishahara Kwa kufoji.

Bado hii nchi inahitaji kunyooshwa kabisa naona Bado watu wanapakana mafuta Kwa mgongo wa chipa huku wakilamba asali.
Nileteeni 1000 digits kwenye uchaguzi ujao.
 
Ni haki walipwe kwakuwa walikuwa wamefanyakazi.
Hoja ni hii,nani aliwaajiri watu wenye vyeti feki?
Ni utawala wa ACT wazalendo?
Kwani hawakulipwa mshahara Kwa udanganyifu wao?
Yaani mtu alipwe mshahara Kwa miaka yote Kwa udanganyifu halafu Tena alipwe na fidia. We are not serious .
Mhalifu hahitaji huruma kamwe labda akiri na kuomba msamaha kuwa walitukosea na walituibia Kodi zao na kuwaacha watu waliostahili.


Walitakiwa warejeshe pesa zote walizolipwa mshahara Kwa utapeli .Wezi wakubwa.

Nileteeni 1000 digit awanyooshe wezi wa nchi hii.
 
Sasa hapo haki yake ni ipi zaidi ya kufukuzwa Kwa udanganyifu.
Yaani miaka yote alipwe Kwa udanganyifu halafu aje alipwe na fidia badala ya kurudisha zile alizotuibia.

Wewe huoni kuwa Nchi hii inakosa maendeleo Kwa sababu ya watu wengi kuwa na vyeti feki.

Hivi unahabari kuwa hata PhD na Masters nyingi ni za Kununua bila kufanya tafiti na wakipeleka vyeti wanaongezwa mishahara mikubwa Kwa kazi Ile Ile na ujuzi ule ule waliokua nao wenye digrii Moja au wasio hata na digrii.

Kwa Sasa watu maofisini wanashindana kutafuta PhD na Masters sio Kwa ajili ya kuweka utaalam au hata kufanya mapinduzi ya kiutendaji na kiufumbuzi Bali kuongeza mishahara wakitoka jioni wakalale kwenye mabaa na Wanawake mchezo imeisha halafu utasikia wakikuambia nasoma ili nipumzike nile mshahara mkubwa.Yaani badala ya kuongeza kazi na kusaidia jamii mtu anasema anataka apande Cheo na mshahara ili apumzike.

Hivi Kwa mfano Mwalimu wa shule ya Msingi akasoma mpaka akawa na PhD halafu akabaki kufundisha shule ya Msingi atakua na manufaa Gani ?
Tunataka mtu asome kihalali na afanye kazi zaidi na ionekena sio kuwaza mshahara na vyeo Kwa kununua tafiti za watu wengine. Hawezi hata kuzielezea.

Dereva darasa la Saba alitakiwa asome QT kama wangine.Lakini wenzake walipokua wanasoma yeye anampigia simu mtu wa baraza na kumpelekea laki Tano halafu akapewa cheti adhabu yake ni kufukuzwa na kurudisha mshahara au kufungwa.
Huoni JPM aliweka hashima mpaka Baraza hawauzi vyeti na vile vya stationary haviuziki Tena.

Tafuta cheti kafanye kazi Huko kwenye kampuni binafsi lakini sio kazi ya umma inayolipa Kwa Kodi ya watu wote na nafasi zipo Kwa ajili ya wote. Ukidanganya unatupwa nje wanapewa watanzania wengine waaminifu. Wapo wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…