Shaka: Rais Samia kuwalipa waliofukuzwa kwa vyeti feki ni ishara ya huruma, upole na upendo kwa Watanzania

Shaka: Rais Samia kuwalipa waliofukuzwa kwa vyeti feki ni ishara ya huruma, upole na upendo kwa Watanzania

Hiyo ni haki. Siyo ushenzi anaohubiri ndugu Shaka. Mtu akipewa haki yake ni huruma? Acheni kumchafua Rais kwa kumbambikia mambo ya ajabu ajabu na kumlazimishia sifa za kipuuzi.
 
Anzeni na katiba za vyama vyenu Kwanzaa
Katiba ya vyama Haina impact kubwa kwa taifa na kwa wananchi kwa ujumla wake.Impact Ni ndani ya vyama vyao TU.Ndo maana Kule CUF wakati Ile Lipumba anavurugana na Maalim safe mpaka wakagawana meza na viti vya Ofisi,Hakuna sehemu au nchi iliyumba kwa changamoto Hiyo.
 
Baada ya kusikiliza hii sasa Pitia hizi nondo kwa makini,Viva Tanzania,

View attachment 2209052
View attachment 2209053
View attachment 2209054
View attachment 2209055
View attachment 2209056
View attachment 2209057
View attachment 2209058
View attachment 2209059
View attachment 2209060
View attachment 2209062
View attachment 2209063

POINT TO NOTE,

1. Hawa watu wanawatoto wanaowategemea sijui hao watoto wanahali gani hata leo!!?

2. Hawa watu wanawazazi wanaowategemea sijui wazazi wao kama leo wako hai au walikufa kwa Presha!!?

3. Hawa watu waliumizwa sana sijui leo wanahali gani,Ni Mungu pekee ndio anajua,

Asante Mama Samia, Asante sana Mama, Hakika wewe ni Mama,

Jabali,

Kazi iendelee,
 
Huruma isibague uhalifu. Hivi imefanyika Tathmini faida na hasara ya kutumia wafanyakazi hao huku wakiwa na vyeti fake kabla ya kufikia uamuzi huu?

Nadhani Kuna haja ya baadhi ya watu waelezwe kuacha kutumia nia njema na huruma ya Mama vibaya
 
Ilitakiwa aondoe wafanyakzi hewa na sio vyeti feki. Mbona waliondolewa kwa shida ya vyeti wapo sekta binafsi na wamefanya vizuri sana
 
Huruma isibague uhalifu. Hivi imefanyika Tathmini faida na hasara ya kutumia wafanyakazi hao huku wakiwa na vyeti fake kabla ya kufikia uamuzi huu?

Nadhani Kuna haja ya baadhi ya watu waelezwe kuacha kutumia nia njema na huruma ya Mama vibaya
Kinachofanya Kazi ni akili na sio vyeti,mbona majeshini awakuondolewa na Kazi zinaenda kama kawaida
 
Kabisa, nchi imetoka katika utawala wa jitu katili kabisa
 
Yani mtu ana vyeti fake analipwa wakati kuna vijana kibao hawana kazi na wanavyeti halali, sisi watu weusi kwakweli tuna laana flani hapa duniani si bure. 60 yrs of independence bado tupo hapa na siasa uchwara.
Nakupa mfano wewe unaliyejitangazia laana sababu ya weusi wako.
Kuna mtu aliajiriwa kama dereva kwa cheti cha darasa la saba halali na akatumikia kwa miaka mingi tu katika mazingira magumu.
Baadae, kwa imani kuwa akileta cheti feki cha form 4, labda kipato chake kitaongezeka kidogo. Kama kiliongezeka, basi kidogo sana na maisha ya mtu huyu yakawa duni vile vile. Maana kwenye utumishi wa umma , mtumishi siku zote analipwa pungufu kwa kile alichokifanyia kazi. Aliyemuibia mwenzake hapo utajua wewe.
Anyway, Siku ya uhakiki, cheti chake feki kilicho kwenye faili lake, kinamfuta kabisa kazi jumla jumla na kuondoka mtupu na matusi juu. Familia yake inaishia kuteseka .
Nasema hivi, hukumu wewe moyoni mwako unavyoona inafaa ila waache wale wanamuogopa kweli Mungu na sio kwa maigizo wafanye yenye Haki. Glory be to God.
 
Kuna waliostaafu na vyetu vyao halali kabisa ila wanasotea stahiki zao either hawajapata kabisa au wamelipwa advance tu.

Katika mazingira haya hata kuzungumzia hilo suala la kuwalipa watu waliofukuzwa kwa kughushi vyeti ni fedheha.

Malizaneni na hawa vyeti halali ndiyo mzungumzie hao vyeti feki.
 
Kinachofanya Kazi ni akili na sio vyeti,mbona majeshini awakuondolewa na Kazi zinaenda kama kawaida
Polisi huwezi fanya kazi bila kuwa na vyeti halali vya chuo.cha polisi Moshi au cha Jeshi kama Monduli nk

Vyeti vilivyofojiwa vingi vya uraiani

Hebu fikiria unakuwa na mwanasheria mwenye vyeti Feki ofisini hadi digrii Feki hajawahi kanyaga hata chuo.Huyo akienda kusaini mkataba wa Serikali ukiwa wa hovyo unajua uliigharimu nchi kiasi gani?

Fikiria future ya mtoto aliyefundishwa na mwalimu mwenye cheti Feki cha walimu akafeli vibaya na future yake ikaisha barabarani
Fikiria future za watu waliokuwa na vyeti halali kabisa waliokuwa ajira kisa hao vyeti Feki walibana nafasi zao.Fikiria maisha magumu waliyoishi wao na familia zao kwa kukosa ajira wakati ajira zao ulikuwepo zikachukulia na hiyo mitoto ya shetani iliyofoji vyeti

Nafikiri kilio cha wenye vyeti halali walicholia kukosa kazi kwa kuzibiwa na hao vyeti Feki Mungu alikisikia.Walilia na Mungu.

Kuwalipa wahalifu waliobana nafasi za wenye vyeti halali wakose ajira si jambo la kufurahia kwenye inayotaka kujenga uadilifu kwenye sekta ya umma .Hilo jambo litakiwa libaki hivuo ili.kujenga Jamii yenye uadilifu mkubwa kwenye ya umma
 
Yule ambaye hakuwalipa alikuwa na ishara ya udikteta, uchoyo na roho mbaya
 
Lakini huwezi foji taaluma. huwezi kuwa police bila kufanya kozi ya police, huwezi kuwa Mwalimu bila kusomea ualimu, huwezi kuwa dereva bila ujuzi,nk.
Tofautisha cheti na ufuzu au ujuzi.
Vyeti havifanyi Kazi bali brain,thus wenzetu wazungu au wachina awatazami Sana vyeti bali utendaji.
Mbona majeshini awakufukuzwa kama ishu ni vyeti,
C
 
Mlaghai anaambiwa alipwe asilimia tano za pesa alizolaghai!!! Hii kitu haiko sawa hata kwa logic ya kawaida
Sio KILA kitu ni logic,mbona mafisadi wamekwapua pesa na still wapo kazini wakiendelea na Kazi kwann wasiwe jela.
 
Back
Top Bottom