View attachment 2322973
Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema hakuna shaka Rais Samia Suluhu Hassan ataendelea kuwavusha watanzania hadi 2030 kutoka na uwezo mkubwa uliounesha katika uongozi na utendaji uliotukuka.
Akizungumza katika kongamano maalum la kumpongea Rais Samia huko Unguja hii leo, Shaka amesema Rais Samia pamoja na Rais Dkt. Hussein Mwinyi ni viongozi shupavu walioonesha ari kubwa kuwatumikia watanzania.
Shaka amesisitiza kutokana na kazi nzuri ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 inatoa uhalali kwao kuendelea kuiongoza nchi yetu panapo kudra za Mwenyezi Mungu mpaka 2030 ikiwa pia ni utii wa katiba ya CCM, kanuni na utamaduni tuliojiwekea.
Aidha, Shaka amesema wale wenye ndoto ya Urais 2025 kwa bara na visiwani wasahau kwakuwa CCM inamila, katiba,desturi ,Utaratibu na miongozo mbalimbali zinazotawala muda wa Rais kudhaminiwa na Chama cha Mapinduzi.
===