Shaka: Watanzania watege sikio tarehe 09 Oktoba Dodoma, Rais ana jambo la kuwaambia watanzania

Shaka: Watanzania watege sikio tarehe 09 Oktoba Dodoma, Rais ana jambo la kuwaambia watanzania

Hivi ni lini araonekana Raisi mwenye maono na Falsafa? Mwl. Nyerere, Mkapa na Magufuli wote hao ulikuwa ukiwasikiliza unaona wamebeba Falsafa na maono Fulani. Hebu tusaidie maono na Falsafa yake
Falsafa ya Magufuli ilikuwa nini?
 
Anaamini katika kuwafanya wananchi kuwa na Amani.
Kujenga usawa wa kijinsia
Kugawana national cake kwa usawa
Kudumisha uhisiano na mataifa yenye nguvu kiuchumi
Yupi ambaye hakuwahi kuamini hivyo?
 
Tutayatega masikio yetu kumsikiliza mwenyekiti wa CCM na Rais wetu KIPENZI[emoji120]

ADUMU CHIFU MKUU HANGAYA
ADUMU MH.RAIS SSH
ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA MWENYEKITI MH.SSH [emoji123]

#KaziIendelee
#TunaImaniNaMh.RaisSSH
Unalipwa au unaifanya hii kazi kwa mapenzi yako?
 
Atakuwa anataka katiba mpya
Mkuu wewe kuanzia Kikwete unampinga, kaja yule dikteta pia umempinga na tulimpinga wote, Hata huyu mama nae pamoja na uungwana wake Bado mkuu wewe haumkubari!?? Ebu tuambie ni Nani angefaa hawe Rais,
Mkuu unajipa mastress ya bure aisee
 
Yeah...naona mama kaanza kampeni za 2025 kwa kasi hasa. Nini kimetokea?

Nilimsikiliza Membe juzi akisema atakuwa kampeni manager wake 2025.......nikawaza haya yote hakuna shaka hayotokei kwa bahati mbaya.

Nani anapanga au wanapanga, sijui. ...lakini muda utasema. Soon tutaanza kusikia "mitano tena"!

Madaraka matamu sana jamani....
 
Wana CCM bhanaa!!!
Shaka ni CCM.
Mh. Samia Suluhu H. ni Mwenyekiti wa CCM - Taifa, ambaye pia ni Rais wa JMT.
Kwa Uenezi wake Shaka,automatically atakuwa anamzungumzia "mwenyekiti wa CCM - Taifa.
Automatically hilo jambo lake litakuwa la CCM.
Kumuaddress SSH kama "rais" na huku yeye si msemaji wa rais, na kuhusisha jambo la chama na taasisi ya urais ni kuonyesha jinsi gani watu wa Lumumba na White House hawajui "job descriptions" zao wala mipaka ya nafasi zao.
Tatizo kubwa sana lililopo kwa Watanzania wengi.
Kuna Muunganiko mkubwa katika hizi Taasisi...Mfano unatenganishaje CCM na Serikali au dola...Yaani Kwanza hata nyie mnaosema ooh Katiba Katiba kwanza ni ngumu sana inatakiwa Kwanza Mlaumiwe nyie mliopewa Katiba na Kikwete mkaleta ujinga ooh Ukawa Ukawa sasa kiko wapi???.

Si bora mngeanza na ile Ya Mzee Kikwete baadae mdai tena.....sasa Mmekosa vyote...Na Hata huyu Mama ameshaingia Mle mle nae anawaangalia mnvyolialia...

Kingine nyie hamna agenda Kama Mbowe yuko jela hamna kitu tena....Wala hamna la maana mnafanya ....

Ingekua mnafanya utafiti mnaita media mnatoa issues zinazogusa wananchi mfano mafuta...kwann yana matozo kibao lakini Mnakaa kutukana mitandaoni...
Issue ya machinga ni bomu kubwa hatuwezi kuziba mitaro na barabara ili watu wengine watandike biashara kisingizio eti wanyonge hamna hiyo...
Nyie kila kitu mnapinga .
 
Kwa sasa Samia anafanya vizuri kuwazidi hao uliowataja. Halafu umekosea mno kumuweka na Magufuli kwenye hiyo orodha. Yule hakuwa na falsafa yoyote. Alikuwa msanii tu ambaye ametumia ujinga na ukosefu wa maadili wa watanzania kujijenga.

Raisi gani mwenye falsafa anatumia fedha za umma kama mali ya familia yake?

Raisi gani mwenye falsafa anatumia pesa za umma kununua wapinzani?
Komenti zingine zinachekesha sana yani Samia anafanya vizuri kuwazidi Mwalimu Nyerere na Mkapa duh hahahaaa inachekesha sana.
 
Akhs
Kuna Muunganiko mkubwa katika hizi Taasisi...Mfano unatenganishaje CCM na Serikali au dola...Yaani Kwanza hata nyie mnaosema ooh Katiba Katiba kwanza ni ngumu sana inatakiwa Kwanza Mlaumiwe nyie mliopewa Katiba na Kikwete mkaleta ujinga ooh Ukawa Ukawa sasa kiko wapi???.

Si bora mngeanza na ile Ya Mzee Kikwete baadae mdai tena.....sasa Mmekosa vyote...Na Hata huyu Mama ameshaingia Mle mle nae anawaangalia mnvyolialia...

Kingine nyie hamna agenda Kama Mbowe yuko jela hamna kitu tena....Wala hamna la maana mnafanya ....

Ingekua mnafanya utafiti mnaita media mnatoa issues zinazogusa wananchi mfano mafuta...kwann yana matozo kibao lakini Mnakaa kutukana mitandaoni...
Issue ya machinga ni bomu kubwa hatuwezi kuziba mitaro na barabara ili watu wengine watandike biashara kisingizio eti wanyonge hamna hiyo...
Nyie kila kitu mnapinga .
Akhsante sana kwa kututhibitishia kuwa nyinyi ni vilaza wa kutupwa.
Hapa umeandika mkorogo gani?
Umesoma mara mbili mbili na kuelewa kilichoandikwa!?
 
Bei ya mafuta mbwembwe zote zile za kutoa tozo 8 lakini imepungua sh 50 tu mama anahujumiwa!!
Nadhani una matatizo ya akili au chuki zinakusumbua.

Bila ku adjust viwango vya tozo bei ingeongeseka kwa sh.145 kwa kila Lita lakini hiyo 50 iloyopungua bado unaona si kitu.

Serikali iliweka tozo ya sh.100 kwa kila Lita kilio mlicholia Hadi mkajiharishia.
 
Falsafa gani? Kazi iendelee ni Falsafa au Haki za Wanawake kuwa sawa na wanaume? Hebu CCM Msaidieni ajue namna ya kupambanua hayo mambo. Bila Maono Kiongozi wa Nchi unakuwa huna tofauti na Diwani.
Kwako maono ni nini inaonekana hata huelewi unachoongea,kwa mfano Mwendazake alikuwa na maono gani?
 
Back
Top Bottom