Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

..kwa tabia yake AK47 haina shabaha.

..But it was the right rifle kutumia kwa mazingira ya eneo walilomkuta Mh.Lissu.
Silaha kitako kikitulizwa begani na kisha kushikiliwa na mikono imara shabaha ipo na kama ikitetereka mlengaji target inakuja juu kidogo ya eneo alilolenga. Kama alilenga chini ya target, maana yake inafikia sehemu lengwa.
 
We sasa kushusha kiti kinanachukua dakika ngapi?Hapa kama huna gari huezi kuelewa.Inaonesha unadhani kushusha kiti ni sawa na kushusha sofa ghorofani
Mkuu kuvamiwa sio tukio la kucheza kombolela kwamba akili za ujifiche wapi zinakuwa active. Ushawah kutwa na jambo lolote la hatari tena ghafla?Yani mvamiwa anapata mda wa kulaza kiti na kulala kifudifudi na dereva anashuka kujificha chini ya gari hahahahah hii movie ni hatar.Msilete story za kwenye bongo movie kwenye issue serious ka hizi.Ile milio ya risasi tu ilitosha kufanya lisu apoteze faham,lkn ye anakuambia alikua anafaham zake vizur tu had anafika hospital na wakat huohuo kuna risasi ilipiga jirani na spinal cord.Nyie watu acheni mahaba ya kijinga kwenye ishu sensitive ka hizi
 
Na ww unautaka ukuu wa wilaya? Kweli Njaa mbaya na jina lako ni Manjaa mengi limeendana na hili bandiko lako braza.
 
Wee jamaa kama si mchawi basi utakuwa mjinga sana !
 
Mkuu hapo hakuna muujiza,Hilo tukio ni bongo movie. Ukiwa unapewa maelezo ya hilo tukio na ukajaribu kulitengenezea picha utaona ni uhuni tu unless thinking capacity yako iwe inaendeshwa na hisia ka unavyodai eti muujiza.Hakuna muujiza hapo.
 
Wewe ndo mjinga kabisa labda sijui kiwango chako tu cha uelewa.Unajua vitu vingine ni vitu vya kawaida sana.Kama una logic kweli kwa ccm hii iliyojaa chuki na visasi dhidi ya chadema ingeacha tukio hili lipite bila uchunguzi mujarabu?kwa nini serikali iliondoa ulinzi eneo husika?nao ni Lissu aliwatoa ?cctv je? Hivi unaelewa eneo la areaD lilivyo na mazingira yake?kweli serikali ilishindwa kama sio mkakati maalum? Serikali kwa nini isitume polisi Nairobi kwenda kumwoji Lissu na Dereva?na kama hujui dereva aliruhusiwa kwenda nchini kenya na serikali ya Tz kama angekuwa suspect no1.wasingeruhusu avuke border.Sema shida ni kwamba by that time serikali ilitaharuki baada ya kuona Lissu hajafa na kama wangetambua mapema kumzingizia dereva kosa wasingeruhusu,wangemnyang'anya passport.
 
Mimi hunisikitisha sana napowasoma hawa watu. Wagumu sana kuelewa.pascal kaandika vizuri sana. Mwenye uwezo wa ku reason ndo anaelewa.wale wa division 5 ndo wanamshambulia kwa maneno ya hovyo hovyo tu.mi nadhan kuna haja ya kuwa na mitihani kupima uwezo watu kabla hawajapewa access ya majukwaa kadhaa kama haya. Otherwise wabaki tu chit chat na MMU.

 
Nilijua utapangua hoja za hiyo movie ya dereva kushuka na kujificha kumbe unakimbilia kwenye kichaka cha CCTV hahahahaha.Tufanye CCTV zipo na kila kitu sawa, ebu niambie kwa tukio la uvamizi ukirejea maelezo uliyoniquote inawezekana vipi?
 
Nilijua utapangua hoja za hiyo movie ya dereva kushuka na kujificha kumbe unakimbilia kwenye kichaka cha CCTV hahahahaha.Tufanye CCTV zipo na kila kitu sawa, ebu niambie kwa tukio la uvamizi ukirejea maelezo uliyoniquote inawezekana vipi?
Hakuna lisiliwezekana kama watu wanaweza kuruka kwenye gari wakati ajali inatokea unashindwaje kulaza kiti ambacho ukibonyeza tu button inashuka na ukibonyeza tena kinainuka?pia lazima ujue kuwa zilizopigwa risasi ni 30+maana yake nyingi zilimkosa pia inaonesha mlengaji hakuwa mwanajeshi na mwenye uzoefu katika kutumi bunduki kubwa.kwa hiyo wakati anakoswa lazima kuna jitihada wao walijaribu kuzifanya na kumbuka dereva ndie aliemlaza Lissu so kama Lisuu angekaa kama kawaida lazima risasi nyingi hususani za kichwa zingemkuta.Hapo bado hujaelewa?
 
Bhavicha wote kichwani ziro
 
Vichwa vyenu sijui vinashida sehem,hata kujaribu kutengeneza kascene kadogo tu na kuangalia inawezekana mnashindwa?
 
Mkuu hapo hakuna muujiza,Hilo tukio ni bongo movie. Ukiwa unapewa maelezo ya hilo tukio na ukajaribu kulitengenezea picha utaona ni uhuni tu unless thinking capacity yako iwe inaendeshwa na hisia ka unavyodai eti muujiza.Hakuna muujiza hapo.
Kwahiyo hata sasa hivi hizo picha na video zote akiwa hospital ni bongo movie. Halafu unadai eti una thinking capacity kubwa. Potezea tu akili yako kisoda. Una uwezo finyu sana wa kufikir na kuchanganua mambo. Rudisha kabisa na ile avatar yako unayojiharishia.
 
Ungeweza kuchambua tukio la Makonda pale clouds ningekuona wamaana Sana.

Kwasababu camera zilikuwepo, pia Kama Tundu Lissu aliweza Kusema kuna watu wanaifatia na polisi wakashindwa Kufatilia. Je unazani ni maana?

Havyo ya camera za CCTV nitakuachia wewe uyaseme.

Ndugu nakwambia hao unaowatetea ipo siku watakungeuka?

mr mkiki
 
Vichwa vyenu sijui vinashida sehem,hata kujaribu kutengeneza kascene kadogo tu na kuangalia inawezekana mnashindwa?
Aisee kweli walimu wana kazi ngumu hivi na wewe ni great thinker?wewe utakuwa sijui mtu wa namna gani? Yaani dah!unasikitisha labda kama hujui ajali au hata uvamizi huwa hautokei wala hauwezi kufanikiwa 100%.katika kitu ambacho wasiojulikana ukiwapo na wewe wanashangaa basi ni kusalimika kwa watu hawa wawili.Ila ujue kuwa Mungu yupo na anatenda kazi maana alisha ahidi kutuokoa dhidi ya watesi wetu.Mungu yupo na alishajidhihirisha katika tukio hilo.Shetani Umeshindwa
 
Mayala Watanzania si wajinga kama unavyofikiri. Mabandiko yako ya siku za kariburi yamekuwa yakiegemea sana upande fulani wa yule bwana mkubwa.

Kibaya zaidi yamekuwa ni mabandiko ya bila fact hata moja. Jitafakari mkuu kuweka credibility yako sawasawa hasa kwenye mabandiko yako .

Uelewe umuhumi wa waandishi kama ninyi katika jamii yetu na madhara unayoweza sababisha kwa kuandika mambo ya dhahania tupu.
 
Natatizika kuamini kama bandiko hili ni kazi ya paskali kwakuwa maswali na hoja alizoweka ni za kiwango cha chini sana kuliko uwezo, weledi na uzoefu wa paskali tunaemjua.
Kama hii ni kazi take paskali, basis atakuwa ameifanya chini ya shinikizo fulani!...
Tunamtaka paskali halisi, yule wa kipindi cha kitimoto....
OVA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…