Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

We nawe ni una shida mahala, mpaka sasa hujaona thread zilizomjibu na kumuuliza huyu msukuma maswali ?? Mwite arudi jukwaani ajibu pia maswali yake maana yanazidi kupile up! Au kama una mapafu ,mjibie!!
 
Pascal

hayo maswali yote Lissu keshayajibu,

better stay quite than openly demonstrate to people kwamba now unalilia sana mkate.

Bro...this is too low to your level
 
Great thinker always anauwezo mkubwa wa kubadili text message to image or picture message. Sasa wewe ktk tukio hili la lisu umefeli kabisa
 
Great thinker always anauwezo mkubwa wa kubadili text message to image or picture message. Sasa wewe ktk tukio hili la lisu umefeli kabisa
Ok sawa.Tatizo nililogundua ni kuwa tupo tofauti kiitikadi na kifalsafa kwa hiyo tukiendelea kueleweshana katika hili hatutafika.Ila kaama unadhani Lissu alijishambulia,sawa.Na kama unaona mbowe ndo alomshambulia Lissu sawa.kama unaona kuna mtu nje ya taasisi zote 2 ndo amehusika,sawa.kama huoni mkono wa serikali pia kwako ni sawa ila kwangu naona serikali ikihusika 100%.
 
Kaka Pascal ata Mimi huwa nina mashaka na yule dereva.Maana ata ukimuangalia usoni anaonekana ana mengi kuhusu like tukio.
Mimi nahisi yule jamaa kama pandikizi Fulani maana Tundu Lissu aliisumbua sana serikali sakata la watu kufukiwa mgodini Bilyanhulu.
Tusubiri KARMA itaamua.
 
Bro...this is too low to your level
Unaangusha hiyo ID(2008)...Read Paskal between lines (his whole work while thinking critically)! For sure,....you will find out ...that He is putting on the table a serious allegation against the government regarding 'Lissu Saga'!! He has to come forward for this and explain in details.
 
Sasa si mkamkamate dereva ahukumiwe? mnangoja nini?
 
Pascal Hiyo nadharia hapo juu no. 7 wengi inatuacha na maswali mengi ya kujiuliza.Jinsi dereva alvyopona bila hata kupata mkwaruzo katikati ya mvua ya risasi.
Mkanganyiko mwingine ni pale tulipoambiwa dereva alimgeuza Lissu akalalia kiti kiasi ambacho mguu wa kulia ukaathirika zaidi, halafu ndipo dereva akateremka na kujificha.Hapa kuna wingu zito.
 
Pascal,subiri teuzi.

"Baada kuona kuna gari linawafuatilia, mlichukua hatua gani?".
Walichukuwa tahadhali,ndiyo maana wakanusurika.

"Ukiisha jiridhisha you are followed, una change direction kumpoteza maboya"
Hiyo Dodoma ina ukubwa gani hadi ukampoteza anayekufuatilia.

"Ukimuona bado yupo, then kama uko fit, unamlengesha mahali kwenye kona ambapo hawezi kuchomoka, mnamalizana!".
Wangemalizanaje wakati Lissu ana mkoba wa files za mambo ya bunge na wasiojulikana wana SMG.Hiyo mbinu yako haiwezekani kwani kwa vyovyote vile anayekufuatilia atakuwa amejiandaa.Jambo la kustukizwa unaweze kujiandaa?.

'Kama hauko fit, unamlengesha kwenye safe area ,usually sehemu open kwenye makundi ya watu na kumripoti kunakohusika'.
Hivi kuna safe area kuzidi yale makazi ya viongozi wa serikali yenye walinzi waliyosheheni silaha za kivita na CCTV camera?.Una nini wewe Mayalla.Fikiri angeenda sehemu ya wazi,unadhani wangeacha kummininia marisasi na tukaambia majambazi walitaka kupora hela.Lissu amewazidi maafira.Wchuchumae tu,wamevuliwa nguo.

"Baada ya kuona mnafuatwa, kwa nini mliendelea kuelekea nyumbani"?.
Nyumbani kwake ndiko nyumbani kwa viongozi wa serikali.Kama nyumbani kwa viongozi wa serikali zinamininwa makuni ya risasi,sina hakika eneo gani lingine wangeshindwa kufanya hivyo.


"Mlipofika mkasimama, mkawaona watu wawili wanashuka na AK 47, kitendo tuu cha kujua tuu bunduki zile ni AK 47, hii maana yake ni close proximity, kwenye shooting that close!, risasi 38!, dereva huyu amesalimikaje asipitiwe hata na moja"?.
Wangekuwa na shida na dereva naye wangemcharaza risasi.HAWAKUWA NA HAJA NAYE.

"Ametokaje kwenye gari na kujificha chini ya gari ya jirani bila kugundulika"?!.
Narudia.Wangemhitaji wangemfuata,ndiyo maana hata baada ya tukio hawakushaghulika nae hadi pale walipoona mipango imeshindikana.

"Anafichwa nini kuhojiwa?, kuna nini kinafichwa"?.
HIZO BLA BLA TU.Alikuwepo Nairobi,na sasa Ubelgiji.Lissu katoa mwongozo.Ulikuwa ni wakati muafaka kuruhusu uchunguzi HURU ili kama hawa akina Mbowe ndiyo watekelezaji wa huu unyama WASHIKISHWE ADABU maana wanatuchafulia Taifa letu.Cha ajabu wanaogopa uchunguzi huru wa kimataifa.AJABU.

MWISHO WA UBAYA NI AIBU.
 
Pascal - kama Dereva unamtilia shaka kwanini CCTV camera zilitolewa? Na kwanini zisiachwe ili kuisaidia Polisi katika upelelezi? Mkapa hakukosea kusema waandishi Makanjanja[emoji41]
Kwanini hamtaki kuwaza kama huyo dereva alishirikiana na waliotoa camera?Kuondolewa kwa camera kunamtoa vipi dereva kuhusika na tukio?
 
Na wakati huo wauaji walikua bado wanasubiri akina lusu wamalize kujificha ndo waanze kumimina risasi
 
Nukuu

ni uzito tuu wa serikali kugoma kuita wachunguzi wa nje. Ingekuwa ni inside job ya Chadema, tungeshuhudia serikali fasta ingechunguza!.

Pascal Mayalla kwa kuwa na wewe ushaonja uchungu wa Serikali ya Awamu 5 kwa aina yake.

Nakuuliza swali.
Kwa nini serikali inaogopa uchunguzi huru ikiwemo kusaidiwa na wachunguzi kutoka nje ya nchi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…