Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Embu fafanua wewe kuhusu ilo tukio lilivo tokea



Wabongo bhana kila mtu ana jikuta expert
 
Bro acha kuliaibisha jeshi la polisi kwasababu kimsingi wao ndio walipaswa wawe wakwanza kufanya uchunguzi nakuja na majibu ya nani kahusika nalile shambulio.iwe ni uyo dereva au awaye yoyote yule.sasa aya mambo ya mtaani yakumtuhumu dereva wakati vyombo husika vipo kimya vinapunguza uwezo wetu wakupambanua mambo.
 
Mkuu JokaKuu, baada ya shambulio kulikuwa hakuna plan B ya kueleza nini kimetokea kwa njia za 'fix'.
Ilitegemewa ungekuwa mwisho wa Maisha na suala zima

Kutokana na fyongo na mipango hovyo, kwanza, hakuna aliyefikiria uwepo wa Camera. Ilipogundulika zipo zikaondolewa. Camera zingeonyesha vema uhusika wa watu

Pili, swali lisilojibiwa ni kwanini siku hiyo walinzi wa eneo waliondolewa wote.

Tatu, kwanini Polisi hawafuatilii Camera wanamfuatilia 'dereva'

Mpango ulisukwa kumkamata dereva kwa mahojiano kisha kutengeneza hadhithi kwasababu dereva asingekuwa na kipaza sauti.

Unakumbuka yuele kijana wa UDSM Nondo alivyoletwa mbele ya vyombo vya habari bila yeye kupewa nafasi ya kujieleza.

Alikuwa amesimama tu ili ionekana ni mzima na anakubaliana na yaliyosemwa


Kama kuna kitu kizuri Chadema walifanya ilikuwa kumuondoa dereva.

Huyu alikuwa atumike kutengeneza uongo kama ule wa Mwangosi wa kitu chenye ncha kali kilichotupwa na mfuasi wa CDM, baada ya picha kutoka ilikuwa aibu tupu kwa Polisi

Endapo dereva angekuwa sehemu ya mpango, mbona lingekuwa jambo rahisi sana

Kwanza huenda angemaliza kazi kwa risasi moja tu kifuani au kichwani

Pili, asingemshtua bosi wake wanafuatiliwa , angetulia hadi mwisho wa sinema

Tatu, angeweza kutumika kuwekewa sumu kama yule waziri aliyechubuka mwili mzima

Hizi ni hadithi tu, inajulikana na kadri inavyozungumzwa ndivyo inaondoa shaka hata wale waliokuwa na doubt. Tusijitie upofu na wendawazimu wa kulazimisha. Hili halina mjadala
 
Na wakati huo wauaji walikua bado wanasubiri akina lusu wamalize kujificha ndo waanze kumimina risasi
Hebu msijitoe akili, kama ingekuwa hivyo gari pekee ndio ingeoga risasi na lissu akafanyiwa igizo feki la kushambuliwa kama yule mwanajeshi!!
Issue ni kwamba Lissu alioga risasi na dereva alipona, angalia lissu alikaa upande upi wa seat na dereva alikaa upande upi halafu uniambie kati ya Lissu na dereva na alikuwa na uwezekano wa kuescape kulingana na upande pyu pyu zilipotokea. Obvious uwezekano wa dereva kupona ulikuwa upo kwa yeye kwa yeye kulala uvunguni mwa gari, na haijasemwa kwamba risasi zilipigwa hadi uvunguni mwa gari.
 
Mpendwa Paskali, Kwanza kabisa inabidi kutambua kwamba kabla ya kuibua hoja katika janga hili lililomkuta Tundu Lissu
Paskali, katika ishi kama hii ya Lissu, MOTIVE ni muhimu sana. Labda kwanza ungejadili motive ya dereva kuhusika. Hapo hoja zako zingekuwa na nguvu. Kwa hoja ulizoleta, hujamtendea haki Lissu.
Katika matukio kama haya, mtuhumiwa namba moja ni yule mgomvi wa aliyeshambuliwa. Serikali ya awamu ya tano imejipambanua kutosita kutumia nguvu kubwa dhidi ya wapinzani wake. Wanaokosoa kidogo tu wanashughulikiwa vilivyo. Hapo ndio mahali pa kuanzia. Na kwa kuwa ushahidi wa kimazingira upo:
1) Kuzimwa kamera za CCTV eneo hilo
2) walinzi kuondolewa
3) mpaka sasa si Lissu wala dereva wamehojiwa
4) mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya kile kinachoendelea katika upelelezi wa Polisi, hivyo kuna uwezekano hakuna upelelezi wowote unaendelea.
5) serikali imeonesha nia ovu kwa wapinzani kwa kupambana wanaotuhumiwa wasipate dhamana hata kama sheria inaruhusu, kutafuta kuwafunga kwa njia yoyote, na kuwabambikizia mashitaka.

Kwa hiyo tungetarajia mtuhumiwa namba moja, serikali, ajitetee, au kuleta hoja zitakazotuondoa kumtuhumu, tufikie watuhumiwa wengine. Mpaka sasa hatujaona hoja zozote za kututoa hapo.
Kwa hiyo bandiko lako Mkuu Paskali, Lina mapungufu makubwa
 
Na hii ndo demokrasia sasa,kupinga,kutofautiana,kukinzana ndiyo demokrasia.Unless uwe na definition nyingine ya demokrasia
 
Wewe dereva afanyaje ili wingu likutoke?
 
Asante Mkuu!! Majibu mujarabu kabisa!!
 
Paskali,
Leo imekuwaje ukaja na maneno potofu kihivi?? Siamini, nadhani kuna mtu kakuibia Id Paskali. Njoo huku JF mambo yako si mazuri.
Ka ni wewe, wamekuahidi ka wilaya gani?? Hata mpya yaweza anzishwa hapo Pugu ukawa DC. Hivi hamuoni vibaya kuishitaki serekali kuwa wamelala hadi kina Paskali ndio waweze kuwaza vizuri?? Pathetic.
Wanasema; Serekali ina mkono mrefu wala haijawahi kushindwa na lolote. Swali la kizushi; Je, walishindwa kumkamata alipokuwa Nairobi au tuseme alikuwa kafichwa? Je, hata leo hii hawajui alipo? Mbona wewe huwasaidii kuwatonya alipo? Realy Pathetic.
 
Mkuu!
Maneno mengi ya nini? Nenda Polisi, andika statement wakupe RB uende kumkamata.
 
"The only defence ya Dereva wa Lissu has nothing to do na hiyo shooting, ni uzito tuu wa serikali kugoma kuita wachunguzi wa nje. Ingekuwa ni inside job ya Chadema, tungeshuhudia serikali fasta ingechunguza!. "
 

NI UJINGA WA KIWANGO CHA LAMI

1. Kuamini kwamba serikali ilihitaji makomandoo wengi tena wenye AK47 kumuondoa Lisu uhai. Kimsingi JASUSI mmoja tu mwenye mafunzo haba kabisa anatosha kumuondoa Tundu Lisu duniani, Tena bila mpuuzi mwingine yeyote yule kujua.

2. Kuamini kuwa pale bungeni MAJASUSI walishindwa kumuwekea sumu kwenye kiti akakalia KAMA AMBAVYO ILISEMEKANA D.R MWAKYEMBE ALIWEKEWA NA MAMVI (Na mpaka leo bado haijajulikana)

3. Kuamini kuwa wangeshindwa kumsubili barabarani wakamsukumia roli la taka ikawa ajali kama ile ililoua watalii kule Arusha

4. Kuamini kuwa Majasusi (TISS) walikosa dawa ya usingizi ya kupulizia ambayo wangeweza kwenda nyumbani kwake wakapuliza kisha wakamchomba syringe ya sumu na wakati wezi tu wa kijingajinga huku mtaani wanayo na wanatumia kuiba majumbani

5. Kuamini kuwa Majasusi (TISS) walikosa food poison ya kumuwekea dereva wa Lisu ili akilewa na kuzidiwa barabarani gari lipinduke.

6. Kuamini kuwa Majasusi (TISS) walishindwa kubuni A silent assassination method waje kumsubiri nyumbani na kupiga kelele nama AK47 ...UPUUZI.

Mimi sijawahi kwenda hata JKT lakini nina uwezo wa kubuni mbinu zaidi ya 50 za kum-eliminate MBOWE ukiachialia mbali Tundu Lisu..

TUNDU LISU hana ulinzi wa kuwapa shida watu wa TISS kama wanania ya kumuondoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…