Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

U
Uhuru wake wa kueleza unalindwa lakini wakati huo huo hoja aliyotoa ni ya kinafiki, huku akijua kuwa hadi hii leo hakana mtu hata mmoja aliyehojiwa kuhusiana na tukio hili, vyombo vya mabavu vipo kimya, havisemi neno, havijishitukii kwani ni jukumu lao kufanya hivyo.

Mawali ya Paskali ni ya hovyo na hayana nguvu yoyote kisheria na hata kiuandishi wa habari, akajipange upya, au afanye hata investigaTIVE Journalism atapata majibu sahaihi juu ya tukio hili baya amabalowachunguzi wamelichunia kana kwamba aliyeshambuliwa ni kuku. SAD!
 
FACT [emoji115] [emoji115] [emoji115] [emoji115]
 
kwa nini dereva afichwe?Mara ya mwisho tuliambiwa anatibiwa saikolojia ila hatujawahi kupewa updates zake.
 
Witness alienda Nairobi kwa sababu zipi?
 
Halafu CCTV cameras tuliambiwa zilikuwa kwa Kalemani ambaye Ni jirani yake Leo tumeambiwa zilikuwa kwa Lisu mwenyewe. Mpimeni na akili jamaa yenu au aanze matibabu ya kisaikolojia kama dereva.
Walikuwa wanamtaka dereva waende kumminya kwa vitu ambavyo havijui.
Wao walitakiwa wakamate watu kadhaa.na magari Nissan nyeupe ambazo wanazihisi.
Baadae ndo wamuuite dereva.aende kuwatambua wale watu au Yale magari.
Sasa wao wanamtaka tu dereva.atawasaidia nini?
Zaidi ya kwenda kumpa mateso.
 

Mkuu GENTAMYCINE kwanza nikupongeze kwa uandishi wako makini na kuandika mambo yenye mashiko. Uko sahihi sana ww na Paskali kwa kuliangalia hili jambo kwa jicho la 3D, hiyo ni haki yako na mengi ya uliyoandika yanafikirisha. Ila mjue sisi ni watu wazima tuna uwezo wa kuchambua na kuelewa na kupima kwa akili ya kawaida kabisa. Mimi sijikiti kwenye hayo ya CCTV kwani sina uhakika nayo na nini kinaendelea. Tuje tu kwenye shaka ya wazi, eneo hilo tunaambiwa lina ulinzi mkali wa askari wenye silaha muda wote, ilikuwaje siku hiyo ya shambulio wasiwepo eneo la tukio? Hata kama walikuwa wametoka kwa dharura, kwa mlio wa AK47 tena kwa askari walipaswa kufahamu hili. Ninapofika hapa nairuhusu akili yangu kukubaliana na maelezo yako ww na Paskali lakini moyo unakataa.

Ww na Paskali tunajua ni waandishi makini, na nina uhakika mnaweza kuandika vizuri zaidi ya hivi. Lakini kwa hili shambulio na hali halisi ilivyokuwa, hata muandike vitabu vya ukubwa wa biblia kutuaminisha hicho mnachotetea mtapoteza tu muda wenu adhimu. Kwa hili mtuvumilie tu, mnaweza mkatupa majina mengi ya kebehi na vyovyote mnavyoona, lakini hilo haliwezi kupunguza ukweli tunaouamini.
 
Paskali, kadri ya uelewa wako (ukichanganya na kusoma sheria Mlimani) naomba unisaidie kujibu maswali haya:
1. Linapotokea tukio serious la uhalifu wa kijinai (criminal offence) polisi wanafanya evidence gathering kwa namna ipi hasa kwa suspect number 1-wanakaa ofisini kumsubiri au wanatoka kumfuata tena kwa haraka?

2. Katika tukio kama hilo polisi wanahitaji kupata ruhusa ya suspect number 1 au mwajiri wake katika kumhoji?

3. Unafikiri ni kwanini polisi hawajamhoji dereva wa Lisu kama ni suspect namba moja kama unavyosema-ni kwa sababu hajajipeleka polisi? Hawawezi kumfikia? Amefichwa?

4. Kwa kuzingatia hoja uliyotumia kwamba uhusiano na imani aliyonayo Lisu kwa dereva wake hauwezi kuaminiwa na wenye kazi yao-ni nani ambaye anaweza kuaminika zaidi, angalau kwa sasa-Lisu anayesema anamwamini dereva wake kwamba hawezi 'kumuuza' au wale wanaomsuspect (suspect number 1) huyo dereva lakini wanamsubiri awafuate ofisini?

5. Wakati unaandaa hayo maswali kwa Tundu Lissu ulikuwa umejaza fikra gani kwenye akili yako-kwamba waliomiminia risasi Lisu walidhaminiria kumuua au kumfanyia shambulio kubwa la kutisha lakini bila kumuua?

6. Askari aliyesomea kozi mahususi hawezi kufanya hili la pili-la kufanya shambulio kubwa la kutisha lakini bila kumuua mlengwa hata kama litahusisha ufyatuaji risasi?

Wabeja gete namhala!
 
Pasco anataka kubalansi like swali alilomuuliza jpm ikulu mpk likampa heshima linamuumiza sasa anataka serikali imuone ni mwema kwahiyo anatafuta jukwaa LA kuipendeza system imuone imfikirie pasco umefeli na umejiaibisha
 
Maswari ya kipuuzi sana

Sent from my SM-N7502 using JamiiForums mobile app
 
Paschal tokea uitwe na kamati ya maadili ya Bunge umekuwa mpiga zumzri
 
Aliyesema kuwa askari hawakuwepo ni nani na alikuwa wapi akiangalia kuwa askari hawapo?
 
Mkuu GENTAMYCINE umejaribu kuelezea vizuri kwa muono wako lakini tujaribu kuona kwa upande mwingine basi ukoje.
Ni kweli system ikikuhitaji huwezi kabisa kuchomoka maana inao watu trained wanaojua wana fanya nini.
Lakini system yaweza kutumika Mara mbili, issue official ambayo lazima inapangwa kiuweledi na inafahamika kwa wahusika Wa jambo hilo kwa mkakati kamili na kuna LA pili jambo ambalo halina maslahi ya taifa hivyo linafanyika kiharamu kwa kutumia baadhi ya wahusika Wa system kutekeleza.
Na uharamu huo ndio unao sababisha mambo Ku backfire hadi kuleta sintofahamu ndani ya system hadi wakati mwingine mambo ya "utata" kama yale ya kuhamishianaTabora. Hilo LA siri na haramu ndio laweza kuwa lilitumika kwa Lissu kwa system ile ile kwani Lissu sio tishio kwa taifa na hata ndani ya system anao wafuasi wanaojua umuhimu wake na kumuunga mkono utapangaje kwa uwazi kumdhuru?
Lingine ni ukimya, serikali zote ulimwenguni litokeapo jambo lenye kuichafua ni haraka sana kuweka wazi uchunguzi wake kujisafisha. Lakini mbona hii imeufunga uchunguzi pamoja na mambo ya wazi kabisa ikiwamo kuondelewa ulinzi, CCTV camera na mengineyo?
Kubaki na kusema dereva dereva ni argument isiyo na mashiko hata kidogo katika issue iliyochafua nchi kwa kiasi kikubwa. Tukubaliane tuu kuwa serikali imeshafunga siku nyingi file LA Lissu kwani majibu inayajua na kama ni kwavile ni inside job basi ni wazi serikali hii haitufai hata kwa dakika moja. Inashindwa kichukua hatua? Yaani mie nikimuua mke wangu watasema hayo ni mambo yetu ya ndani?
 
[UOTE="jingalao, post: 28278302, member: 56995"]Aliyesema kuwa askari hawakuwepo ni nani na alikuwa wapi akiangalia kuwa askari hawapo?[/QUOTE]
Jingalao kwe maswali tumia logic ili usionekane unauliza tu bila kujua swali unalouliza litazaa kitu gani. Sababu kama swali lako linataka kuonyesha kuwa askari walikuwepo na anayesema hawakuwepo ni muongo basi hapo utafeli maana utaulizwa kuwa askari wapo halafu wameangalia tu yanayoendelea bila hata kurespond? Hata hakukutokea majibizano ya risasi? Kama ni mahakamani umeuliza hilo swali mtu anakujibu tu inawezekana walikuwepo, ilionekana hawapo sababu hakukuwa na majibizano. Wewe unaamini walikuwepo?
 
Hiyo ndo njia inayotumiwa na professional assassins, hatakiwi kuacha clue
 
Kwani wewe ni ofisa upelelezi?usitafute cheo kwa nguvu ya damu ya mtu.Tuache vyombo vya usalama vitupe taarifa kamili
Pascal Mayalla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…