Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Umenena vema,
Swala ni moja a punguza kuishi kwa hisia na kutuhu watu.Pili atambue yeye siye wa kwanza kupigwa risasi .....Kuachiliwa kwakwe kwa adui ni kwa sababu ya kujiamini zaidi kuliko kumuamini Mungu.

Kwa serikali kufanya uchunguzi ni Dereva ni mtu wa kwanza kwani kila uchunguzi una source ya kuanzia.

Mwisho aache kuwadanganya watanzania wasiojua kanuni za bunge,ni kweli hakufuata taratibu za serikali hakuzifuata,yeye siyo mtu wa pekee mpaka bunge likiuke utaratibu...amekuwa a kipiga kelele juu ya Bunge kukiuka taratibu,sasa wamemuonyesha namna gani huwa wanajitahidi na kupambana na watu wa style yake (wanaovunja taratibu) kuzisimamia.

Bado naamini hata ingekuwa Muhimbili bado angepata huduma na kulindwa...kwa kama ni ulinzi wapo madaktari na wahuguzi wengi ambayo uwenda ni wafuasi wake.Kwa maana hiyo bado nasema kimbiza kimbiza kuna jambo....polisi wasilaumiwe kwakuwa hawa kupata fursa ya kuruhusiwa kuifanya kazi yao.

Ni sisi watanzania tunaosukima vyombo vya usalama vifanye kazi kisiasa...however nawapongeza jeshi la polisi kipindi hiki hakuna wanasiasa wengi ndani yake wote wanasimamia taaluma.
Muulize Lisu kama a nafuatilia taarifa hata huko ulaya wapo viongozi wakubwa wa kisiasa waliwahi kupigwa risasi na mpaka kesho wahusika hawajakamatwa.

Ni vema sasa apunguze habari za kufikirika na kuipa nafsi yake nafasi ya kuyatambua yaliyo ya kweli.
 
Yani kwa hoja hizi,Mayala bado yuko sahihi kabisa.Mmekazana na habari za walinzi mara CCTV nk.Kwani huyo dereva hawezi kuwa sehem ya hao waliotoa camera? Ni mambo ya ajabu lisu kupata mda wa kufanya press conference Kenya lkn akashindwa kuja kudai haki yake Tz. Anayetakiwa apiganie haki yake ni lisu na sio serikali, yani lisu ndo anapanga nini serikali ifanye ikitaka kumhoji,serious? Mara ooh polisi ya Tz haina mamlaka ya kunihoji mara wanifuate Belgium. Huyu mtu yuko serious? Wale anaodai wampe haki yake ndio haohao anakesha kuwakejeli na kuwadhihaki anafanya hivi makusudi tu
 
Ukweli wa yote, huwezi kuanza upelelezi bila shahidi/mshukiwa namba moja kuhojiwa. Yeye ndiye angetoa mwangaza upelelezi uanzie wapi, kitendo cha kumzuia shahidi ni jambo la kukwamisha upelelezi wenyewe.

Kama ni shida ni haki mnayoitafuta,kwanini shahidi namba moja azuiwe? Tukisema mlikwamisha kupatikana kwa haki tunakosea?

Tukumbuke jeshi la polisi lina taratibu zake za ufanyaji kazi pia, lilipotoka kitu kwa ajili ya ufanyaji kazi wake(kumuhoji dereva). Mlimsaidia?
Huyo ndiye aliyekuwa eneo la tukio anajua vitu vingi alivyoviona siku ile ya tukio kuliko mtu yeyote, yeye ndiye angeweza kusaidia hilo suala kiupana.

=======

Kiupande wa Lissu naye ana makosa, pamoja na kuwa mwanasheria anakiuka baadhi ya taratibu zinazofahamika. Huku akijinasibisha anafuata utawala wa sheria, napo simwelewi utawala wa sheria upi huo anaoudai?

Sote tunafahamu ukihisi hali ya hatari na namna ya kufuatiliwa. Ni Kutoa taarifa juu ya wasiwasi wa usalama wako kwa jeshi la polisi, yeye kaitisha mkutano na wanahabari ndiyo anaongea hayo na si kuripoti kwa idara husika yenye msaada kwake.
Sote tunajua Lissu ni mwanasiasa, kama ikidhaniwa ni njia yake ya kutafuta jina zaidi alilonalo. Maana kipindi kile wanasiasa wengi walitamka hayo, ila hakukuwa na chochote. Hivi kwa mantiki hii hilo suala lingepewa uzito gani kuliongea mbele ya kamera pasipo kuwapa taarifa wenye mamlaka ya kukusaidia.

Sasa kama yeye kama mwanasheria, kwanini akiuke utaratibu husika?

=========

Tukija upande wa wahalifu wale, sote hatujui ni kina nani na hatuna uhakika na tuhuma zinazotuhumiswa serikali.

Pia hatujui Tundu Antipas Lissu ana maadui wangapi, nje ya siasa, haswa kwenye taaluma yake ya sheria, kwenye biashara zake na kwingineko.

Maana hata 99% walengaji ni wahuni hawana mafunzo stahiki ya kijeshi, wamefundishiwa kichochoroni kutumia silaha. Mwenye mafunzo stahiki ya kijeshi ya utumiaji silaha, hawezi fyatua risasi kiholela namna ile.

Pia silaha iliyotumika ,(AK47 ingawa mwanzo ilisemwa ni SMG/sijui tushike lipi hapo? ) haimilikiwi na majeshi ya ndani ya nchi hii, hutumiwa kiholela na vikundi vya silaha vya nchi jirani na hivyo ndiyo huwauzia majambazi na wahuni huku.
Bado waliyofyatua risasi ni wahuni na si watu waliyofunzwa kutoka ndani ya system.

System maafisa wake wanatumia bunduki za mchina zenye kuchukua risasi 30 tu na si hiyo ya kirusi(Ak47) yenye risasi kubeba 40 .

============

Suala la kuitwa wapelelezi wa nje wasaidie upelelezi ndani ya nchi, si la kiholela kama kuita fundi bomba aje kukaza koki ya maji jikoni kwenye sink la kuoshea vyombo.

Wale wanaitwa kama kazi ya wapelelezi wa ndani ni ngumu kuwasaidia, au wanaruhusiwa kufanya kazi kama eneo husika lina kitu chenye maslahi na taifa lao.
Rejea tukio la kuungua kwa BOT, kuna wapelelezi wa nje walifika. Wale walikuja kwasababu mule kuna vitu vya taifa lao, si kuja kiholela tu.

Sasa wapelelezi wa ndani hilo suala halijawashinda, upelelezi wao walipotaka kuanzia ndiyo kumekwamishwa kisa mambo ya kisiasa.
Hawawezi kuitwa watu wa nje, kwa suala wanaloliweza watu wa ndani abadani.

Hakuna cha uchunguzi huru wala uchunguzi utumwa, hilo jambo kisheria halipaswi kushirikishwa majasusi wa nje ilihali wa ndani wanaliweza. Hebu tusitie siasa kwenye kazi za watu
 
Aliyesema kuwa askari hawakuwepo ni nani na alikuwa wapi akiangalia kuwa askari hawapo?


Kwa mada hii tunaomba ukae utulie tu maana uwezo wako tunaufahamu tuachie tuongee na kina paskali mayalla, gentamycine, misuli nk, hawa wanauwezo wa kuongea jambo likaeleweka. Ww nenda kaandae tu lile jedwali la viwanda mia moja kila mkoa. Mwaka unaenda ukingoni huu.
 
Muuaji huyu alikua anajifunza kuua kwa kutumia mwili wa lisu hahahahah risasi 38.Yani hata ktk movie sijawahi ona wingi wa risasi ka huu.Hili tukio liingizwe Guinness World Records.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Ajabu la dunia, au ni mtoto anayecheza kibunduki kashika akijua ni ya gololi


Halafu Maafisa wa system risasi zao full magazine ni risasi 30 tu na hawatumii AK47
 
Paskali, wewe mbona hukuwakwepa na kuwapoteza? Walichokufanya ni wewe na wao mnaojuana. You fit to be potential "usiyejulikana". Poor you.
HUYO ACHANA NAE...NI MMOJA KWENYE KIKOSI CHA WASIOIJULIKANA...NA AKIENDELA NA YEYE ATAOKOTWA COCO BEACH.
 
mkuu nimecheka sana..KULA LIKE KAMA CHAI IVI...YAANI CHAI 3 ASUBUHI!!!!
 
Risasi 38 jembe bado lipo hai linarudi tena na moto ule ule, mjipange upya ss sijui mtatumia nyuklia???!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Ajabu la dunia, au ni mtoto anayecheza kibunduki kashika akijua ni ya gololi


Halafu Maafisa wa system risasi zao full magazine ni risasi 30 tu na hawatumii AK47
HAWATUMOO AK7 COZ IMEPITWA NA WAKATI...KUNA GOOGLE GLASS....DO YOU KNOW IT?
 
Hivi unajua unachokisema?
NDIYO NAJUA. KWANINI HIYO PRODUCT ILIPIGWA VITA? NI KWASABABU ILIKUWA INFUNUA MBINU/BIDS/KAMPUNI ZA SIRI AMBAZO WATEJA WAKE NI SERIKALI TU...HIVYO HATA TEKNOLOJIA PUBLIC ITASUBIRI SANA...

na mimi nikuulize:
UNANIJUA?
2. UNAIJUA INTERPOL?
 

Ulichoandika hapa ni kuonyesha kwamba una uwezo wa kufikiri na hata ukipewa kazi ya kutetea watuhumiwa wa kumshambulia Lissu unaweza kutetea kwa kiwango fulani kimantiki. Hii ni haki yako kutumia akili yako kwa jambo lolote ambalo una maslahi nalo ama kwa kuwiwa kufanya hivyo. Lakini napenda nikuambie kwamba utetezi wako huu ungeweza kufanya kazi sehemu ambayo kuna watu wenye upeo finyu. Kama askari waliokuwepo eneo hilo walitishika na mlio wa hiyo AK47, je CCTV Camera nazo zilitishwa na nini? Pole ndugu, hata kama una maelezo yenye mantiki lakini kumbuka huwezi kuficha ukweli kwa maelezo mazuri. Hapa ulichoandika ni sawa na kuanika nguo kavu.
 
NDIYO NAJUA. KWANINI HIYO PRODUCT ILIPIGWA VITA? NI KWASABABU ILIKUWA INFUNUA MBINU/BIDS/KAMPUNI ZA SIRI AMBAZO WATEJA WAKE NI SERIKALI TU...HIVYO HATA TEKNOLOJIA PUBLIC ITASUBIRI SANA...

na mimi nikuulize:
UNANIJUA?
2. UNAIJUA INTERPOL?
Jamaa kabla ya kujibu maswali yako hayo, hiyo mbinu unayotaka kuitumia nikwambie ni ya kizamani sana. Hao Interpol nawajua vilivyo ni international police.

Hilo la kukujua wewe sina haja nalo
 
Lissu ameshasema atarudi. Na ndiye aliyepigwa risasi hivyo yeye tusimuongelee sana. kama ni lazima ahojiwe nchini na si kwingine atahojiwa atakaporudi. Na asiporudi yeye ndiye atakayepoteza haki lakini ataendelea na maisha. Mm siangalii haki wala siasa. Nimeangalia uwezekano wa dereva kuongeza dakika za kuishi duniani esp kama si muhusika. Kama anaona uwepo wake hapa utapunguza dakika zake za kuishi ni sawa akibaki huko alipo mpaka itakapolazimika yeye kuwepo. Jiulize tu mtu akifanya uhalifu akakimbilia nje ya nchi, hakuna utaratibu wa kumpata pale vyombo vya usalama vitakapotoa ushahidi? Kama ni dereva kafanya uhalifu serikali itaweza tu kupata ushahidi na atarudishwa kwa ushirikiano wa nchi zote mbili. Kwa sasa ngoja aishi.
 
HUYU NAE TUTAMLA RISASA...anaingila maslahi, achana nae.
 
Jamaa kabla ya kujibu maswali yako hayo, hiyo mbinu unayotaka kuitumia nikwambie ni ya kizamani sana. Hao Interpol nawajua vilivyo ni international police.

Hilo la kukujua wewe sina haja nalo
MAANA YAKE WEWE NAE NI KICHAA...KAMA RAIS WAKO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…