Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Ndio shida yenu.Yani kila anayewakosoa ni anataka uteuzi.So unataka kusema wote tuimbe wimbo mmoja?
Pamoja na kwamba hizi comments kwako ni kazi sawa tu na wale ambao huwa wanapewa kazi ya kwenda kuua binadamu ila unaifanya chini ya kiwango sana. Hata hivyo sishangaa maana aliyekutuma is worse
 
Mkuu tindo, yapo mambo ambayo hayawezi kuandikwa humu.

Siasa za upinzani zinaruhusiwa Tanzania, kosa ni baadhiya watu kutoweka mipaka kati ya siasa na kukomoana.

Alitaka kuikomoa serikali, kibao kikageuzwa mazima.
 
Mkuu tindo, yapo mambo ambayo hayawezi kuandikwa humu.

Siasa za upinzani zinaruhusiwa Tanzania, kosa ni baadhiya watu kutoweka mipaka kati ya siasa na kukomoana.

Alitaka kuikomoa serikali, kibao kikageuzwa mazima.

Sipingi usemacho, unaweza ukasema ni hatua gani wamechuliwa wale waliotajwa kwa majina kwenye ripoti ya Ossoro kwamba waliingiza nchi kwenye mikataba ya wizi? Kama wale wenye ushahidi wa kusaini mikataba mibovu hawajachukuliwa hatua, huoni hiyo sababu ya uzalendo inayotajwa ni kichaka cha kuhalalisha tu shambulio la Lissu? Philipo tukubali tu shambulio lile ni aina ya siasa chafu kutokea hapa nchini kwa ulevi wa madaraka.
 
Mk
Mkuu pasco nakuheshimu,ila kwa hili hatuko pamoja .Mimi kwa upande wangu ningeomba uanzishe Uzi unaouliza nani alizuondoa CCTV kwenye eneo alilo shambuliwa lisu?
 


..kwa kifupi madai kwamba Mh.Lissu alikataa kuhojiwa akiwa Nairobi siyo ya kweli.

..na madai kwamba amemficha dereva pia siyo ya kweli.

..Upo ushahidi wa Mh.Lissu akisema yeye na dereva wako tayari kuhojiwa.

..nakumbuka hata familia ya Mh.Lissu, kupitia msemaji wao Wakili Mzee Alute Mughwai, walisisitiza kuwa hawana pingamizi kwa Polisi kumhoji Mh.Lissu na dereva wake.

..Swali tunalopaswa kujiuliza ni kwanini SEREKALI / JESHI LA POLISI hawakuchukua hatua ambazo zingewezesha Mh.LISSU na DEREVA wake kuhojiwa wakiwa NAIROBI ambapo walikaa kwa zaidi ya MIEZI 3?

..Mwisho, siamini kama Mh.Lissu anajua taratibu za kukusanya ushahidi kuliko Jeshi lote la Polisi la Tz na lile Kny.

..Tofauti ya Mh.Lissu na wasomi wengine wa sheria ni kwamba Mh.Lissu siyo mchoyo ku-share na wananchi kile "kiduchu" anachokijua kuhusu sheria, pamoja na haki za wananchi.
 
Madai ya police wa Tanzania hawana uwezo wa kwenda kumhoji lisu Nairobi yalitolewa na nani?
 

..TUNDU LISSU aliponzwa na rekodi yake kwa wananchi kwamba yeye ndiye mkweli na aliyejitoa kutetea rasilimali za wananchi bila kujali hali au madaraka aliyokuwa nayo.

..Ripoti za Prof.Mruma na Prof.Osorro pamoja na mambo mengine zilelenga kumjenga mtu fulani kuwa ndiye mtetezi na mzalendo pekee mwenye uchungu na rasilimali zetu.

..Sasa makosa yalifanyika kwa watu na taasisi fulani kuanza kampeni ya KUMCHAFUA na KUMDHALILISHA Mh.Tundu Lissu.

..Kampeni hizo ziliratibiwa vizuri toka Mawaziri na Wabunge kumshambulia na kumkejeli Tundu Lissu ndani ya bunge. Wengine walifanya kazi hiyo ktk vyombo vya habari. Na nakumbuka hata kulikuwa na kundi la wasanii lililopanga kuzunguka nchi nzima kupiga kampeni ya uzalendo.

..Balaa lilianza Tundu Lissu alipoanza kujibu mapigo. Na alikuwa akijibu mapigo utafikiri anatumia "ngumi za chuma." Ilifika wakati wabaya wake wakapoteza muelekeo kabisa kwa kushindwa kujibu hoja na madai ya Tundu Lissu.

..Juhudi za kumnyamazisha Tundu Lissu kupitia mahakama zilionekana kuchukua muda mrefu.

..Wakati huohuo Tundu Lissu alionekana kuumiliki na kuutawala mjadala wa kisiasa nchini, huku waliokuwa wakimchafua wakipotezana na kuonekana vituko machoni mwa jamii.

..Katika mazingira hayo ndiyo likatokea SHAMBULIZI BAYA LA SEPTEMBA 7.
 
Madai ya police wa Tanzania hawana uwezo wa kwenda kumhoji lisu Nairobi yalitolewa na nani?

..Jeshi letu haliwezi kuingia nchini Kenya na kuanza kukamata watuhumiwa, au kuhoji mashahidi, linaowatafuta.

..Wakifanya hivyo watakuwa wame-violate mipaka ya Kenya, na ni kinyume cha sheria za kimataifa.

..Ikiwa Polisi wetu wanamhitaji SHAHIDI au MTUHUMIWA aliyeko Kenya basi wanapaswa kuomba ushirikiano toka jeshi la Polisi la Kenya.

..Mh.Lissu na dereva walikuwa Nairobi kwa zaidi ya miezi mitatu kwahiyo tunapaswa kuwauliza Polisi wetu kwanini hawakuomba ushirikiano na msaada toka Kenya ili Mh.Lissu na dereva wahojiwe/wachukuliwe maelezo.
 

Kula tano mwanangu, hapa umeweka kisu kwenye mfupa.
 
Awe amehusika au hakuhusika, awe amefichwa au hakufichwa, Serikali yetu ambayo ndiyo yenye wajibu wa msingi wa Kumlinda kila mtanzania imefanya nini mpaka sasa? Je dereva wa Lissu amefichwa mbinguni ambapo serikali haiwezi fika?
 
Pia serikali ya Kenya haikuwahi kutoa maelezo Kuwa imekataa ombi la serikali ya Tanzania ya kutaka police wake wakamhoji Lissu Nairobi au la kumkamata drive wa lissu na kumrudisha Tanzania
 
Kazana utapata uDC hata murro alianza hivi kujitoa akili
 
Kesi hii yaweza kuwa rahisi sana, kinachotakiwa ni uchunguzi huru. Nakuongezea maswali, je risasi zilipigwa mbele, nyuma au pembeni ya Lissu, je! risasi yaweza kupoteza mwelekeo ikikutana na kizingiti, je! uelekeo wa gari ya wasiojulikana na gari ya Lissu ulikuwaje, je! uchunguzi wa awali wa mashuhuda wa tukio tofauti na dereva wa Lissu unasemaje, je! magari yaliodhaniwa yalikamatwa muda gani baada ya tukio, je! Polisi walijisahau vipi kuchukua Maelezo ya awali kutoka kwa dereva wa Lissu kwa zaidi ya masaa kumi hasa ikizingatiwa hili ni tukio la kipekee. Yapo maswali mengi zaidi kuanzia alipotoka bungeni, nje ya geti la makazi na ndani ya makazi, pia kuna response ya polisi kwenye tukio na barabara zote kuu kabla na baada ya tukio. Hata kama ni Fundi wa kutumia silaha ukikosa uelekeo sahihi hata uwe na risasi mia moja inaweza kuwa kazi bure.
 

Huku mtaani kuna story kibao za watu mashuhuri walioshughulikiwa..kiasi kwamba ukiambiwa unakataa ila ndio ukweli. ETI LEO Tundu Lissu tu watu waende wakapoteze risasi 38.
 
Huku mtaani kuna story kibao za watu mashuhuri walioshughulikiwa..kiasi kwamba ukiambiwa unakataa ila ndio ukweli. ETI LEO Tundu Lissu tu watu waende wakapoteze risasi 38.
Kwanza eti walianza kumfuatilia toka Dar.Yani hao watu ni vichaa kiasi gani wajue jamaa kashatushtukia bado waendelee kumfuatilia tu hadi dodoma.Anatoka bungeni hao wako nyuma nyuma.Wale wale waliokuwa wanamfuatilia toka Dar.Nimesoma visa vingi sana vya mauaji ya watu mashuhuri lkn sijawahi kutana na movie mbovu ka hii.Serikali yenye kucontrol kila kitu hadi huko bungeni kwenye viti na maiki anayotumia,leo impe mtu AK47 ianze kumfukuzia lisu toka Dar hadi Dodoma.

Walivyo vichwa maji wanakuambia baada ya tukio eti hilo gari likaanza kurudi Dar na escort njiani kwa mwendo wa kasi.Inawezekana vipi?Hao wauaji kweli walishindwa hata kupanda ndege dodoma hapo chap had waache alama kama hii?Maswali ni mengi sana kuliko majibu.Na nilichogundua hili tukio watu wanalijadili kwa mihemko ya kivyama,lkn ukichukua maelezo kuanzia mwanzo hadi mwisho na ukaamua kutengeneza movie utakuta unapata movie mbovu mno yani bora hata bongo movie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…