Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Su

Suala ni jee aliripoti polisi rasmi na kupewa RB? Kulalamika na kuripoti tukio ni vitu tofauti.

Kwani kuripoti au kutoripoti polisi kwamba kuna "watu ninahisi ni wabaya, wenye lengo la kunidhuru" wananifuatilia kinaweza kikawa kigezo cha polisi kutoshughulikia/chunguza uhalifu ambao umekwisha tokea?

Kwani MO Dewji aliwahi kuripoti polisi kuwa kuna watu wana "intention" ya kumteka? Polisi walipoingia kwenye uchunguzi hata mwisho wa siku MO akapatikana, walitumia vigezo gani?

Wanaopigwa risasi bila kwanza hata kujua kuwa leo wangeuawa kwa kupigwa risasi, wataachwa wasipewe haki yao na vyombo vya dola kwa kuwatafuta wahalifu kwa kigezo kuwa "the victim" awe yuko hai ama amekufa hakutoa taarifa polisi na kupewa RB??

Hebu fafanua, ikikupendeza
 
Una
Ingekuwa vigumu kujua kama MO ametekwa kama jamaa hawajarusha risasi.
Hivyo kitendo cha kurusha risasi na walinzi pamoja na vyombo vya usalama vilivyo karibu na tukio ilikuwa tosha.
Kwenye suala la TL, polisi baada ya tukio hawakuaminiwa kabisa na hivyo kukosa taarifa muhimu toka kwa eye witness ambazo zingeweza kumaliza tatizo. Hadi leo nadhani kuna gaps kubwa kwenye uchunguzi wao ambao ungeweza kumaliza tatizo hili kama eye witnesses wange record statements zao. Kwa TL ingekuwa vigumu lakini taarifa toka kwa dereva zingeweza sana kusaidia.
 
Mkuu Mag3, japo humu tumo wana jf wengi, na hatufahamiani in reality, lakini wana jf tunaheshimiana kwa viwango tofauti kutokana na mabandiko yao humu, mtu kama wewe, Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Mchambuzi, just to mention but few, ni miongoni mwa the top 10 highly respected members kwenye list yangu, hivyo ukisema kitu au ukishauri, lazima niuzingatie sana ushauri wako.

Hivyo uliposhauri niufute uzi huu, amini usiamini, nimeusoma tena na tena huku nikijiuliza kwa nini niufute, sikuona, ukinielimisha nitakushukuru.

Mimi ni miongoni mwa members humu, tuliojitanabaisha kuwa hatuna vyama, tunaegemea kwenye ukweli na uwazi. Hivyo kwa vile najiaminisha kuwa mimi ni mkweli na kila ninachopandisha humu ni ukweli mtupu, then siufuti ukweli wowote niliopandisha humu, hata kama itanibidi mimi kubadilika ili kuweza kuendana na wakati uliopo, kwa sasa sasa tunaishi under the law of the jungle, survival is for the fittest, one you have to be real fit to survive katika nyakati hizi, mimi ni that fit and I'm survival.

P
 
Hivyo uliposhauri niufute uzi huu, amini usiamini, nimeusoma tena na tena huku nikijiuliza kwa nini niufute, sikuona, ukinielimisha nitakushukuru.P
La kwanza kabisa; uzuri wa ushauri ndio huo, hulazimiki kuufuata. Hata mimi wakati natoa ushauri, nilijua hivyo...ushauri si maagizo, unabakia ni ushauri tu.

La pili; una haki kabisa ya kuukataa na kusimamia unachoamini na hapo nakupongeza sana ndugu yangu na kama kuna misimamo inayohitaji ujasiri, huu wa kwako ni miongoni mwa "tops".

La mwisho; hata ile misimamo yako ambayo kwa kiasi inaonekana kupingana na huu una haki kabisa kuisimamia, hongera sana!
 

..hapo alipopigwa risasi TL kulikuwa na CCTV cameras.

..pia ni eneo linalolindwa na askari Polisi muda wote.

..pia ni jirani na makazi ya Naibu Spika ambaye anapewa ulinzi.

..kwa hiyo jambo la kwanza ilitakiwa kuangalia CCTV na kuwahoji askari wanaolinda area D.

..kama askari hawakuwepo yatatakiwa maelezo ya kuridhisha kwanini hawakuwepo.

..Askari huwa haondoki ktk lindo lake bila maelekezo toka kwa viongozi wake.

..Dereva wa TL siyo eye witness. Yeye pia ni victim wa tukio ni bahati kwamba alisalimika.

..Jeshi la Polisi walitakiwa washirikiane na INTERPOL ktk kuchukua maelezo ya victims wa shambulizi lile ambao ni TL na dereva wake.

..Kwanini ktk tukio la Mo Polisi wameshirikiana na Interpol lakini shambulizi dhidi ya TL hawashirikiani nao?

..Pia tukio la TL linaweza kuwa lilishuhudiwa na majirani zake wa Area D. JE, kwanini hao hawahojiwi?
 
Mkuu jaribu kuwa na hofu ya Mungu, hayo unayoyasema yanaweza kuja kukusumbua nafsi yako baadae
 

1. Ni kama vile hujayajibu maswali yangu karibu yote niliyokuuliza hapo juu...

2. Hivi kweli kwa maelezo yako yanaweza kuwa ndicho kigezo cha polisi kushindwa kufanya kazi yao ya kuchunguza na kukamata wahalifu wa uhalifu huu dhidi mbunge TL na kuwapeleka mbele ya sheria??

3. Aidha kuna watu wamekomaa kweli na ishu ya dereva mpaka hata na polisi nao wamethubutu kusema kuwa ni vigumu kushughulikia tukio baya la jaribio la kuuwawa kwa TL eti kwa sababu "CHADEMA WAMEMZUIA DEREVA WA TL ASIHOJIWE"

4. Hivi Mkuu Abunwasi, unaamini kuwa hii ndiyo sababu "genuine" ya polisi kutotekeleza wajibu wao muhimu wa kulinda usalama wa RAIA (TL ni raia halali kabisa wa nchi mwenye haki zote) na MALI zao? Hivi kweli inaingia akilini kuambiwa kuwa CHADEMA wanaweza kuzuia polisi kufanya kazi yao?? Wao ni kina nani haswa wazuie?

5. Kwa upande mwingine, tumeona karibu CHADEMA yote (kwa maana viongozi wote wakuu wa chama) wana kesi ktk mahakama na vituo vya polisi mbalimbali hapa nchini wakituhumiwa kwa jambo hili ama lile...

Hii inanileta kwenye swali moja la msingi sana ambalo mimi hujiuliza kila mara:

Kwamba, kama chama karibu chooote kina kesi mahakamani......

Hivi polisi wanashindwa ktk engo gani kumpata na kumhoji dereva tu (tunayeambiwa ndiye mtu muhimu ktk tukio zima la shambulizi la TL) ambaye pengine hata siyo mwanachama wa CHADEMA??

Mimi akili yangu inakataa kabisa kuamini haya!!.

Inaniambia lipo jambo jingine kubwa zaidi ambalo hakika ndilo kikwazo cha polisi kushindwa kutenda wajibu wao....

Ishu ya dereva inatumika tu kama kichaka cha kuchelewesha ukweli halisi na wahusika halisi wa shambulio la mbunge Lissu kujulikana!!

ON THE OTHER HAND, kuna possibility ya ukweli huu:

Kwamba, inawezekana kweli kabisa dereva ni mmoja wa watu muhimu sana ktk upelelezi wa tukio zima la kushambuliwa kwa TL.....

Na hii inawezekana ni kwa pande zote kwa maana ya Mwathirika wa tukio Tundu Lissu pamoja CHADEMA kama chama na kwa upande mwingine serikali/vyombo vya dola ambavyo vinatupiwa lawama kuwa likely vimehusika kutaka kumuua TL na kwa sbb hiyo vimenyuti, hawashughulikii kukamata wahalifu wa RAIA huyu.....

Kama ndivyo, ni wazi basi kuwa CHADEMA na Tundu Lissu wanamuona dereva kama mtu muhimu na ana "taarifa zote muhimu" za shambulio hilo na kwamba watamlinda kwa nguvu zao zote na kama ni kwenda kutoa maelezo, basi ni lazima iwe "under very very special condition" kwa nia ya kimlinda as I said before...

Why?

Kwa sbb wanaelewa wakimwachia aende kwa njia za kawaida kama ilivyozoeleka, uwezekano mkubwa ni kupotezwa na akapotea na ushahidi muhimu ambao mwisho wa siku itasemwa, dereva ndiye alitaka kuua bosi wake, ama alitumwa na "M/kiti Mbowe Freeman Aikael!!"

Na kwa kuwa atakuwa "amepotezwa", hakuna atakayepinga maelezo hayo na defenetely itakuwa ndiyo pengine mwisho wa " No. 1 wanted wa CCM anayetakiwa apotee" Bwana Mbowe na CHADEMA yake!!

On the other hand, serikali inalijua hili na haiko tayari kukubaliana na "conditions" hizo kwa sababu zita expose kila kilichofichwa chini ya carpet na wao walishakubali kabisa liwalo na liwe na si "technically and strategically" kukubali kushindwa na CHADEMA/Mbowe kirahisi rahisi hivyo!!

For that case, inataka ifanye inavyojua na kutaka yenyewe ili mwisho wa siku izibe siri hiyo...

Otherwise, mimi nabaki kuamini liko jambo haliko sawa kwa ishu ya shambulio la TL na mzigo unaielemea serikali/vyombo vya dola zaidi bila kujali kama WANAPENDA ama HAWAPENDI kusikia haya!!
 
Mwenzako yuko kikazi zaidi.
 
Hivi waliopanga njama za kutaka kumwua Mheshimiwa Tundu Lisu watamaliza huu mwaka bila kujulikana au kutwaliwa?

Mwenyezi Mungu, please intervene!
 
Dereva angesaidia kutoa abc but mambo yanaenda kisiasa ningumu kufikia mwafaka
 
Nakumbuka kwenye ile kesi ya Prof Mahalu ezi za kikwete shahidi japo alikuwa nchi za nje, technologia ilitumika ili kumfanya shahidi atoe ushahidi wake.

Kwa hiyo serikali ikizamilia haishindikani, sasa kwanini kwa dereva amekaa hapo kenya imeshindikana?

Umesema kwamba walitakiwa waende sehemu safe baada ya kugundua kuwa wamefuatiliwa, sasa kwa mujibu wa maelezo ya lisu ni kwamba pale ni sehemu safe kwa sababu inalindwa masaa ishirini na nne, kutokana na unyeti wa eneo lenyewe, lakini kwa mshangao wao hawakukuta hata mlinzi mmoja kitu ambacho si chakawaida.

Pia pale kulikuwa na cctv camera nani kazitoa,.tena zimetolewa baada ya tukio, maana yake ni kwamba zile cctv camera zina records za hilo tukio ndio maana wamezitoa.

Najua unataka kuwatoa tiss na serikali kuhusika na hili tukio, ila kinyume chake unazibitisha uhusika wao katika hili tukio pale, unaposema eti how come mtu ana Ak47 kashindwa kupiga target katika distance fupi namna hiyo lazima watakuwa wahuni fulani hivi, kwa mujibu wa mashuhuda wa ambao ni bodaboda hiyo gari ilionekana ikipewa escort na police ikitokomea kusiko julikana,.eti serikali ya tz, haina ak47, wao wanatumia smg, tu, poor me.

Kifupi kumsafisha huyo mtu haiwezekani na tiss waliplay part ili kuhakikisha hilo tukio linafanikiwa sema, Mungu hakuruhusu muitoe roho yake, sasa hizi cover up mnazo kuja nazo zinazidi kuthibitisha ushiriki wa tiss na serikali, na pia hai tiss wamehusika kwenye dirt game nyingi na ndio kila mahali kuna grand corruption, ukiachana kuisadia ccm kuiba kura na kupora ushindi.
 
Ata mimi binasi sijawahi kuamini hili.
Tukio la kushambuliwa kwa Lissu lilipangwa liwe mtaji wa kisiasa.
Over
 
Ukiandika hoja za kuwafurahisha utalamba sifa zote. Siku ukiwakosoa ni lawama za usukuma. Hivi usukuma ungekuwa ndio tiketi ungehojiwa dodoma? Endelea kusimamia unachoamini bila kujali fikra za wafia vyama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We ndugu nimekushangaa sana leo
 
Hii umefeli sana mkuu .
Kafeli nini? wewe kijana nakuoneaga huruma sana. sijui hata akili yako huwa inafikiriaga nini? Paschal ameweka mambo yote ya kufikirisha akili zetu kuhusu hili shambulio, unasema amefeli. Kisa tu hakusema Serikali imehusika kama mlivyokaririshwa. Wakati mwingine tuweke pembeni mapenzi na mahaba yetu kwenye hivi vyama hasa kwenye mambo ya msingi kama haya. Ushabiki wetu ndo sababu ya kulea maovu kwenye jamii.
 
Ukiandika hoja za kuwafurahisha utalamba sifa zote. Siku ukiwakosoa ni lawama za usukuma. Hivi usukuma ungekuwa ndio tiketi ungehojiwa dodoma? Endelea kusimamia unachoamini bila kujali fikra za wafia vyama.
Masikini MTAZAMO, kweli umeshuka kiasi hiki...
  • Kumiminiwa risasi Mbunge Mh. Tundu Antiphas Lissu, mnadhimu wa Upinzani bungeni na Rais wa TLS ilikuwa ni mbinu tu ya wapinzani kutafuta kiki ya kisiasa na dereva wake alihusika.
  • Kupotea kwa kijana mwanaharakati Ben Saanane aliyekuwa akihoji elimu ya Rais Magufuli ilikuwa ni mbinu ya wapinzani kutafuta kiki ya kisiasa na Chadema inatuhumiwa kuhusika.
  • Kutekwa, kuteswa na miili ya baadhi ya watu kuokotwa kwenye viroba ni mbinu tu ya wapinzani katika kutafuta kiki ya kisiasa kwa kuichafua serikali wakitumiwa na mabeberu.
  • na mengine mengi...
Ndugu yangu MTAZAMO usipate taabu, hauko peke yako...kuna asilimia kubwa tu ya Watanzania wanaoamini hivyo. Endelea kusimamia unachoamini bila kujali fikra za wafia chama! (hata Dr. Slaa popote alipo labda atakuunga mkono)

Na mwisho kwa usahihisho tu, nakupa rasmi taarifa hii...mimi si mwana Chadema na sijawahi kuwa mwana Chadema wala sina nia na kujiunga nao ila nakiri na ninaamini kutoka moyoni kwamba adui mkubwa wa taifa hili ni CCM na hapo labda ndipo ninapoungana na msimamo wa Chadema. Kumbuka adui wa adui yako ni rafiki yako.

Kwa upande wa Pascal Mayalla, amini usiamini yuko katika wakati mgumu sana (between the rock and a hard place). Anataka acheze kama pele na kweli angeweza ila kafungwa mguu. Wako rafiki zangu wengi tu wako hivyo na naelewa kwa nini wako hivyo. You have no idea what's going on behind the scenes, wanateseka nafsi zao!

Naam, wanateseka kweli kweli!
 
Leo siku ya tarehe 7/Sept. 2019 ni siku ya kumbukumbu ya miaka miwili toka Mh.Tundu Lisu aliposhambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana. Mpaka leo bado wasiojulikana hawa bado hawatajulikana na uchunguzi mkubwa, makini na mkali wa Jeshi letu adilifu la polisi, unaendelea kuwabaini wasiojulikana hawa, hivi sasa kuna mashuhuda wawili muhimu sana, wanasubiriwa wao tuu kuhojiwa ndipo taarifa rasmi ya polisi kuhusu maendeleo ya uchunguzi huu ndipo ilatolewa.

Tuvute subra.
Get well soon Mhe. Tundu Lissu and welcome back home.
P
 
Pascal unajuwa kwa nini ASP Bageni kahukumiwa kunyongwa na mahakama kuu na Court of Appeal kubariki hukumu hiyo? Kwani kuna mtu mahakamani kasema kamuona Bageni akiwafyatulia risasi wale wafanya biashara wa madini?
Theory iliyotumika pale kumpata Bageni hatiani ndio hiyohiyo imetumika na Watanzania kuwatambua wasiojulikana. Hiyo rekebisha andiko lako, sema Wasiojulikana wamejulikana tatizo ni kuwa at the meantime they are untouchable.
Hapo watu wawe wavumilivu tuu muda utafika kwa untouchable kuwa touchable na kwa mshangao wale wasio wajua watashikwa butwaa, kumbe ndiwo ambao siwo!
 
Siyo kila jambo unatakiwa ulitolee maoni, kukaa kimya wakati mwingine ni jibu sahihi na muafaka zaidi.

Watu wote hao ambao wapo kimya baada ya kutokea KWA tukio hili usidhani kuwa hawana la kusema au hawajui kusema, LA hasha, wanalo LA kusema isipokuwa wamechagua kukaa kimya.
 
Takataka Usiye Na Aibu Wala Utu Hata Chembe.

Bahati Nzuri Maisha Bado Yanaendelea, Sisi Yetu Macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…