Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?


Kwa nini walipofika mahali salama (Nyumbani) hawakutoka kwenye gari na kupiga kelele au honi mfululizo?
 
Kamuulize BASHITE
 
K
Hapana jinai inafanyika mahala popote. Ndio maana unatakiwa uwe makini sana. Kama Laurent Kabila alipigwa risasi na mlinzi wake tena ikulu.Ije hapo area D Dodoma ampabo kila mtu anaingia muda wote? Huyu dereva ni wa kulaumiwa.

..U nailed it!!

..Kabila aliuwawa na mlinzi wake.

..ili ufanye jinai ktk eneo lenye ulinzi ni lazima uwe mlinzi wa eneo hilo, au ushirikiane na walinzi.

..na TL alishambuliwa na watu wenye mahusiano na walinzi wa area D.

..dereva kama anahusika basi alishirikiana na walioondoa walinzi wa area D.
 
Maswali ya kimantiki ni hivi;

1. Ilikuwa ni kanuni hivyo ni kawaida askari
kulinda eneo ambalo Lissu alipigwa
risasi?
2. Nani walikuwa zamu siku hiyo na
kwanini hawakuwepo wakati wa tukio
3. Afisa mpanga zamu na kiongozi wa siku
hawajui waliostahili kuwa zamu siku ya
tukio?
Maswali ni mengi kuhusu walinzi wa siku hiyo. Na kama kuna vyuo vya upelelezi bila shaka wanafunzi wake wengi wangechagua nukta hiyo kuwapata wahalifu kutoka wafyatua risasi hadi mtoa maelekezo wa mwanzo!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
..wangetoka kwenye gari wangesambaratishwa vibaya kwa risasi.

..kilichomuokoa TL ni kutokutoka ndani ya gari.
Hufahamu kingetokea nini? Huo ni mtazamo wako kwa sababu unategemea kuelemea kwenye hoja yako. Huwezi kuwa 100%
 
Majungu hayo!
Novemba mwaka 2014 alipomkunja JS Warioba pale Ubungo Plaza mlikaa kimya, kwa vile nyinyi hamkuwa upande wa Katiba Mpya ya Serikali 3. Akaingia Clouds Media na mabunduki napo mka kaa kimya kwa vile nyinyi si wamiliki wa vyombo vya habari. Alipomteka BenSaa Nane na kumuua, pia mlikaa kimya kwa kuwa nyinyi siyo CHADEMA. Hatimaye akamshambulia Tundu Lissu na kumjeruhi, mka kaa kimya vile vile kwa kuwa nyinyi siyo wana harakati wa haki za madini....

Alipomteka RomaMkatoliki mka kaa kimya tena kwa vile nyie siyo wana HipHop...
Subiri zamu yenu ndiyo mtajua BASHITE ni muuaji kichaa ambaye hajali kumwaga damu ya binadamu nwingine
 

Those issues does not justify what TL or Mbowe is doing?
 
Mayalla pole na hongera sana, umewezaje kuwa reqular contributor hapa Jamii Forum kwa kiwango hichi katika jumuia ambayo au hawana ufahamu wa kuchangia au maadili ya kuchangia yako chini sana au ufahamu wa somo na tukio uko chini mnoo.
Pamoja na hayo kuna kiwango kikubwa sana cha watu wanao jilazimisha kuonekana wajinga. Au tuseme ushabiki uliopindukia na hauwezi kupiwa kwa instrument yeyote.
Nimepita jeshini kwa mwaka mmoja, kuna suala la matumizi ya bunduki umeliibua la aina ya AK 47 katika kushambulia. This is very partinent questions you raised. Japo lazima uwe na kaba kwa kuelezea masuala ya majeshi kwa aifa lako, lakini nawaambia wanaousoma huu uzi kuwa na wanajeshi au waliopita jeshini watathibitisha Taifa la tanzania lina walenga shabaha majeshini ambao ukimpa risasi 100 kati ya risasi 95 mpaka 100 zina piga target. Kama ni pua pua tuu risasi zitarudia mara 95 mpaka 100. na tukio hilo linatokea ukiwa mita 50 mpaka100. Wapo wengi mno wakuujaza uwanja wa taifa muda wowote utakapo waita wapo.

Maswali ya aina ya bunduki na ushambuliaji uluofanywa unatoa lead ya kutosha sana what the investigators must focus on. Siwezi kuchangia zaidi lakini naamini kutakuwa na majibu. Pole sana, unabishana na wengi wasio jua na wenye kujua wanakalia ushabiki ambao unadhalilisha Jamii Forum,Hasa kwa wenye kujua Machine guns zinafanyaje kazi kuna ulazima na sio kubeza Dreva wa Lisu kusaidia upelelezi. Mayalla una ngozi ngumu , Asante.
 

..hata sisi tumepita jeshini.

..kuna elements nyingi ambazo zilikuwa against walenga shabaha waliotumwa kumuua TL.

..TL alikuwa ndani ya gari / haonekani kwa macho hivyo hiyo ilikuwa challenge kubwa kwa mlenga shabaha yeyote.

..pamoja na kwamba walikuwa hawamuoni lakini waliweza kumdungua kwa risasi kadhaa na kumjeruhi mwilini kati ya magotini na tumboni.

..kitu kingine unachotakiwa kuzingatia ni kuwa tukio lile lilikuwa ni HIT & RUN.
 
Huyu jamaa nilikuwa namuelewa na kuzielewa.sana mada zake humu Jf lakini sasa nimemdharau sana tena sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini walipofika mahali salama (Nyumbani) hawakutoka kwenye gari na kupiga kelele au honi mfululizo?
Jiulize kati ya kelele na honi mfululizo na milio mfululizo ya risasi ipi ingeweza kuleta taharuki na kuhakikisha wanausalama wanafika kwenye eneo lile on time?? Ulitaka washuke wakati tayari wameshawaona watu wasiojulikana wakiwa na silaha pembezoni mwa gari lao?? Kwanini mnajitoa ufahamu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
No file halijafungwa because they survived. Sasa ndio wanasubiriwa wahojiwe uchunguzi ndipo uanze.
P
Kwa hiyo yakitokea mauaji, uchunguzi hakuna kwa sababu huyo aliyekufa ndio anajua kilichotokea? Tuseme ndio sababu hakuna kesi ya mauaji ya AKWILINA sababu hayuko hai? Naomba unifafanulie hapo maana mimi sijui sheria.

Ila natambua kwamba suala hili la kushambuliwa Tundu Lissu, lina makandokando ya kisiasa zaidi kuliko kisheria. Tundu Lissu mwenyewe ameshangazwa na kutokuwepo na uchunguzi wa tukio hilo.

Kwangu mimi ni wazi kwamba katika awamu hii, kuna maelekezo yanatolewa "toka juu" ambayo ni kinyume kabisa na sheria, kanuni na miongozo, kiasi cha kuwafedhehesha wale wanaopewa maelekezo hayo. Naamini ni katika mtizamo huo, Rais Magufuli aliwahi kutamka kwamba anatamani angekuwa IGP. Pia IGP Sirro naye alitamka kusikitishwa na suala la AKWILINA ilivyoshughulikiwa na polisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…