Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Acheni porojo nyie,hivi unajua kuvamiwa wewe?Yani wavamizi walitoa hadi mda wa lisu kulaza kiti na dereva kushusha ndipo wakaanza kumimina risasi ovyo?Alijuaje kama wamekuja kumshambulia na sio kumteka?Hili tukio ukilijengea image unakuta unapata movie ya kibongo ambayo muuaji anaonja sumu ka imekolea.
Naona unachapa kaporojoporojo ka kuuficha mwili kwa viganja Vya mikono. Ungemjibu tu na tuswali twake twa kipuuzi kwamba, walinzi wa eneo hill walienda wapi, na kwanini camera zilikuwa chopped ili afute ujinga wake?
 
Pascal Pascal Mayala kwahiyo una assume kwamba watu wote wanajua nini cha kufanya kama wanafwatiliwa are you serious??? Hapana kuna kitu hakiko sawa hapa au unamanisha nn?????!!
 
Ujue bunduki iliyotumika ni assault rifle kwa mujibu wa maelezo yake. Maana AK47 ni aina ya assault rifle, ina uwezo mkubwa mno.
Huna akili, kwani kila risasi iliyopita lazima ipate target yake? Kuna matundu 38 lakini mbona zilimpata 16? Usiwe unauliza maswali ya kutia hasira, Lissu ameumia sana na kulala kitandani mwaka mzima kisha unaleta kejeli?
 
Huna akili, kwani kila risasi iliyopita lazima ipate target yake? Kuna matundu 38 lakini mbona zilimpata 16? Usiwe unauliza maswali ya kutia hasira, Lissu ameumia sana na kulala kitandani mwaka mzima kisha unaleta kejeli?
Zilimpata 16 na zikaja kuondokewa zaidi ya 28 mwilini mwake kule Nairobi kama mnakumbuka mlisema hivyo.

Uongo unahitaji kumbukumbu fasaha sana, haya mwenye akili nyingi hadi kushindwa idadi mbili tofauti hongera kwa kuwa na kichwa ombwe
 
Naona unachapa kaporojoporojo ka kuuficha mwili kwa viganja Vya mikono. Ungemjibu tu na tuswali twake twa kipuuzi kwamba, walinzi wa eneo hill walienda wapi, na kwanini camera zilikuwa chopped ili afute ujinga wake?
Mjadala sio walinzi,hoja ni dereva wa lisu.Kama ni walinzi pia naweza sema Dereva wa lisu,hao waliotoa camera na walinzi wanahusika au lazima wahojiwe.Kila mmoja anasehem yake ya kuhojiwa.Shida ni nyie kumfanya dereva wa lisu ni mtu asiyetakiwa kuhojiwa au kutiliwa shaka na hili ni kosa kubwa mno mnalofanya.Sijaona mwenye hoja zenye mashiko akielezea kwanini dereva asiwe suspected. Utata wa maelezo yake unatosha kuwa miongoni mwa washukiwa haijalishi kuna washukiwa wengine.
 
Angekuwa hausiki angekwenda kuhojiwa, madawa aliyopewa Lissu kusinzia ili afanyiwe hayo, risasi zinapiga kushoto anaumia kulia, kiti cha lissu kinalazwa alale dereva hapati hata jeraha,

Camera zinatolewa kwa uchunguzi watu wanadhani ni serikali imezitoa kuficha ukweli,

Suala la Lissu Mbowe anahusika sana sema hamuelewi n.a. Lissu ni mjanja mno anawasiliana na Magufuli ili akipona ndo amwage cheche, mpaka sasa Mbowe hajatulia anatapa tapa kupoteza ushahid wote , lakin Sami ya Mtu ni nzito sana haimwagiki tu,

Leo hii waliopaswa kulipwa ujira wa kazi hiyo wananyongwa tu kupoteza ushahidi, kuna mengi watu wanajua ila wanaogopaga tu kutoa ushahidi,

Britannica
Ujinga ujinga tu. Kwanini mzuie uchunguz huru na msitoe hata senti ya matibabu? Wanauwaj nyinyi[emoji51]
 
Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
Shambulizi la Lissu, Wanaomdhania Dereva Anahusika, Sio Wajinga!, Wana Hoja za Msingi!. Jee Anahusika?.
Maswali haya ni kufuatia hoja za Lissu kwenye bandiko hili.
Mhe. Tundu Lissu,
Kwanza pole sana kwa yaliyokusibu.
Umezungumza mengi kuhusu kilichotokea mwaka mmoja uliopita, ila watu wanaohoji kuhusu dereva wako, nakuomba sana usiwaite wajinga, au wametumwa, kwa sababu mashaka yao ni very valid.

Kwa vile mashuhuda ni nyinyi wawili tuu, wewe na dereva wako, then kuna mambo tungependa kujua kutoka kwa Lissu mwemyewe na dereva wake.

Hoja kuwa tumetoka naye mbali hivyo tunaaminiana, hazina mashiko mbele ya watu na kazi zao. Lissu alipotoka na dereva wake, anaweza kujilinganisha Dr. Slaa na mlinzi wake Kagenzi walipotoka?, halafu what happened?!. Kwenye mambo ya assignment, anaweza hata akatumika mke wako aliyekuzalia wanao, sembuse itakuwa dereva tuu mliotoka nae mbali!.
Baadhi ya maswali ni haya...
  1. Baada kuona kuna gari linawafuatilia, mlichukua hatua gani?.
  2. The common sense ya kufuatiliwa inaelekeza, uki note you're followed, hatua ya kwanza ni kumpote anaye kufollow kwa makusudi, ili kwanza kujiridhisha kuwa anakufollow.
  3. Ukiisha jiridhisha you are followed, una change direction kumpoteza maboya.
  4. Ukimuona bado yupo, then kama uko fit, unamlengesha mahali kwenye kona ambapo hawezi kuchomoka, mnamalizana!.
  5. Kama hauko fit, unamlengesha kwenye safe area ,usually sehemu open kwenye makundi ya watu na kumripoti kunakohusika.
  6. Baada ya kuona mnafuatwa, kwa nini mliendelea kuelekea nyumbani?.
  7. Mlipofika mkasimama, mkawaona watu wawili wanashuka na AK 47, kitendo tuu cha kujua tuu bunduki zile ni AK 47, hii maana yake ni close proximity, kwenye shooting that close!, risasi 38!, dereva huyu amesalimikaje asipitiwe hata na moja?.
  8. Ametokaje kwenye gari na kujificha chini ya gari ya jirani bila kugundulika?!.
  9. Anafichwa nini kuhojiwa?, kuna nini kinafichwa?.
  10. Maswali yataendelea
Huko nyuma niliisha wahi kuzungumza haya kuhusu dereva wa Lissu.

Mpaka sasa the situation ya shambulio la Lissu as it is, limefanywa na watu wasiojulikana. Serikali yetu imeshindwa kuwabaini, lakini sisi watu wa media, tunaweza kusaidia kama nilivyosema hapa.
WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
Hitimisho.
The only defence ya Dereva wa Lissu has nothing to do na hiyo shooting, ni uzito tuu wa serikali kugoma kuita wachunguzi wa nje. Ingekuwa ni inside job ya Chadema, tungeshuhudia serikali fasta ingechunguza!.

Lakini kwa vile wasiojulikana ni hawa
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums

Tusitegemee lolote jipya hapa.
Tundu Lissu, just get well soon, na sasa inakubidi uchangue kati ya uanaharakati na kuishi.

Pole.
P.
Rejea
Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums

Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?! - JamiiForums

Tundu Lissu: Polisi wa Tanzania hawana mamlaka ya kunihoji nikiwa Kenya au kwingineko nje ya mipaka ya Tanzania - JamiiForums

P.
Pumba tu /wewe kweli dishi lako limeyumba mno
 
Ujue bunduki iliyotumika ni assault rifle kwa mujibu wa maelezo yake. Maana AK47 ni aina ya assault rifle, ina uwezo mkubwa mno.
Mkuu hope ni kwamba lissu hajafa, jambo hili ni faraja kubwa kwa watanzania na familia yake. Ni hivi lissu angekufa waliohusika wangetokea kama watu wema mnooo, kwa pole zenye uchungu na unafiki Mkuu kwa chama na familia yake. Halafu ingefuatiwa na propaganda nyingi mnoo kuhusu kifo chake. Lakini kwasasa ni hivi kila propaganda inayojaribu kuinuliwa mjibuji Mkuu -lissu yupo Mzee, so hii inawatafuna mioyo yao sanaaa[emoji30] [emoji30] [emoji30] [emoji30] [emoji30] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Zilimpata 16 na zikaja kuondokewa zaidi ya 28 mwilini mwake kule Nairobi kama mnakumbuka mlisema hivyo.

Uongo unahitaji kumbukumbu fasaha sana, haya mwenye akili nyingi hadi kushindwa idadi mbili tofauti hongera kwa kuwa na kichwa ombwe
Wewe ndo zero brain kumbukumbu yako ni 5%kati ya 100%.kilichoelezwa maganda ya risasi yaliokotwa zaidi ya 28 ila zilizompata ndo hizo alizokwambia yeye means risasi nyingi zilipigwa hovyo na kupoteza mwelekeo.
 
Kamanda ile Demokrasia na uhuru wa maoni ambao huwa mnasema mnaupigania ndio huu anao fanya paskali na wewe una ukandamiza kamanda hahahaha

Uhuru wa maoni ni kwa wao tu kuikashifu serikali..ILA akitokea mtu akatofautiana na wao basi huyo ni mjinga na mchumia tumbo na wala hajatumia uhuru wa maoni.
 
Wewe ndo zero brain kumbukumbu yako ni 5%kati ya 100%.kilichoelezwa maganda ya risasi yaliokotwa zaidi ya 28 ila zilizompata ndo hizo alizokwambia yeye means risasi nyingi zilipigwa hovyo na kupoteza mwelekeo.

ETI ZILIPIGWA HOVYO....Hivi wee unawajua MAJASUSI /TISS au unawasikia tuu?? Atumwe kwenye misheni ya kuua ya kitoto vile alafu apige risasi 28 hovyohovyo?
 
Bwana Mayalla kwa heshima na taadhima naomba nikurekebishe kitu kimoja katika uandishi wako. Hili jambo nimeliona siku nyingi ila niliamua 'kuuchuna' tu.

Ni hili suala la kufuatisha alama ya mshangao au ya kuuliza na nukta, kama hivi!. au ?.

Hii siyo 'grammatically correct'. Inawezekana lakini ni 'swagger' zako tu za kiuandishi. Kama ni hivyo, basi unaweza kuendelea na swagger zako.
 
ETI ZILIPIGWA HOVYO....Hivi wee unawajua MAJASUSI /TISS au unawasikia tuu?? Atumwe kwenye misheni ya kuua ya kitoto vile alafu apige risasi 28 hovyohovyo?
Wale nadhani sio wanajeshi halafu rafiki angu bunduki ya rasharasha ni spesho kwa kuattack kundi kubwa.kama wangejua labda wangechukua bunduki ya masafa watafute sniper risasi mbili au tatu tu tayeri kazi kwisha sasa wao walipiga hovyo.maganda zaidi ya 28 yaliokotwa pale 16 zilimpata mlengwa
 
NI UJINGA WA KIWANGO CHA LAMI

1. Kuamini kwamba serikali ilihitaji makomandoo wengi tena wenye AK47 kumuondoa Lisu uhai. Kimsingi JASUSI mmoja tu mwenye mafunzo haba kabisa anatosha kumuondoa Tundu Lisu duniani, Tena bila mpuuzi mwingine yeyote yule kujua.

2. Kuamini kuwa pale bungeni MAJASUSI walishindwa kumuwekea sumu kwenye kiti akakalia KAMA AMBAVYO ILISEMEKANA D.R MWAKYEMBE ALIWEKEWA NA MAMVI (Na mpaka leo bado haijajulikana)

3. Kuamini kuwa wangeshindwa kumsubili barabarani wakamsukumia roli la taka ikawa ajali kama ile ililoua watalii kule Arusha

4. Kuamini kuwa Majasusi (TISS) walikosa dawa ya usingizi ya kupulizia ambayo wangeweza kwenda nyumbani kwake wakapuliza kisha wakamchomba syringe ya sumu na wakati wezi tu wa kijingajinga huku mtaani wanayo na wanatumia kuiba majumbani

5. Kuamini kuwa Majasusi (TISS) walikosa food poison ya kumuwekea dereva wa Lisu ili akilewa na kuzidiwa barabarani gari lipinduke.

6. Kuamini kuwa Majasusi (TISS) walishindwa kubuni A silent assassination method waje kumsubiri nyumbani na kupiga kelele nama AK47 ...UPUUZI.

Mimi sijawahi kwenda hata JKT lakini nina uwezo wa kubuni mbinu zaidi ya 50 za kum-eliminate MBOWE ukiachialia mbali Tundu Lisu..

TUNDU LISU hana ulinzi wa kuwapa shida watu wa TISS kama wanania ya kumuondoa.
Nakupa heko kiongozi, umesema ukweli.
Kama ingekuwa serikali na intelijensia yake ina shida ya kumwondoa huyo. Angeuawa kifo ambacho hakitoacha swali hata moja, mtu anakuja kukata uhai inaonekana baada ya kuugua muda fulani full stop.

kinafanyika kifo kisichoacha clue yeyote
 
Back
Top Bottom