Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Haya maneno ya kumuhusisha driver wa Lissu hayana mashiko kabisa. Kama ni yeye, ziko wapi CCTV Camera, kwa nini Serikali haitaki uchunguzi huru? Kama serikali haihusiki, kwa nini walinzi waliondoka eneo la tukio muda mfupi kabla ya shambulizi? Serikali inamjua aliyefanya haya, eti askari wetu hawana AK47, una akili kweli wewe? Unazijua silaha zote za nchi hii? Hao walinzi wa Rais wanatembea na SMG? Umeniboa sana kwa kushindwa kufikiri
 
Wala tusiumize vichwa jamani,waliomtwanga risasi lisu,walikuwa na baraka zote za system,
Hii ni copy and paste,duniani kote,ya serikali za ovyo,hivi waliomtesa Mbunge Boby wine,hawajurikani?si serikali ya UG,hizi ni modus operandi za serikali zote za hovyo
Ukiambiwa uthibitishe utatoa ushahidi upi kuifanya tuhuma hiyo ihalalike?
 
Pale unapoamua kubishana na reliable sources kwa sababu ya rangi ya chama, stupid ,jinga kabisa.
Hata wewe ukifungua blog na kuidesign kiproffessional, ukaandika kufeli kwa Dunia nzima. Ukiisearch Google inakuja, maana ni search engine.
Je nayo ni reliable source?
 
Pole sana Kaka yangu Kitasnia na Kamarada ( Comrade ) Ndugu Pascal Mayalla kwani sijapitia ' pages ' zote ile kwa nilizozipitia niweza Kugundua tatizo Kubwa lililopo katika Kizazi cha Watanzania kwa sasa. Watu wanaongozwa na ' mihemko ' ya Kisiasa pasipo kuangalia Uhalisia wa jambo na hata hao wanaolilazimisha ili liaminike hivyo ukisikiliza tu ' arguments ' zao haraka sana utakubaliana ule Utafiti kuwa Elimu nzima ya Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni ipo katika ICU.

Pole pia kwa Kushambuliwa Wewe kama Wewe kimaelezo na baadhi ya Wachangiaji wetu wale wale ambao Mimi siku hizi nawaita ' Wachangiaji Oya Oya ' ambao Wao kufauta mkumbo na kuamini Upuuzi ndiyo jadi yao huku wakiaminishana huko katika Vijiwe vyao.

Nilishasema katika Uzi mmoja ambao niliwahi Kuuandika hapa hapa Jamvini na leo tena narudia lile lile tena nikiwa najiamini kabisa kwani huhitaji kuwa na Elimu kubwa sana kuweza kujua mchezo mzima ulivyo na nini kinaendelea. Nitakataa mpaka siku ya mwisho kama Tundu Lissu alishambuliwa na Watu wa ' System ' wa Serikalini ( Idara Nyeti ) kama ambavyo humu mitaani na uswahil tunavyoaminishana.

Hapa wala tusidanganyane kama kweli ' System ' ingekuwa inamtaka na imemdhamiria Tundu Lissu sidhani hata kama angeweza na kuthubutu kuwakwepa au kushindana nao. System zote au nyingi zilizoko duniani huwa hazitumii na haziwezi kutumia ile mbinu ya Kipumbavu iliyotumika kule Dodoma. Hivi Tundu Lissu ana ' ubavu ' kweli wa kukwepa ' assassination trap ' kama ' Wanamume ' wamemdhamiria kweli?

Yaani kwa jinsi leo hii ' Teknolojia ' za masuala ya Kijasusi zilivyokuwa na mbinu mpya zilizopo ambazo hata hazihitaji nguvu Kubwa kutumika inawezekana kweli ' System ' ikatuma Watu vile halafu Watu ambao ni ' highly trained and qualified ' kabisa wakarusha risasi 38 halafu bado Mtu awe hai? Jamani hebu muda mwingine tuweke hizi Chuki zetu za Kisiasa pembeni na tujikite zaidi katika Uhalisia wa jambo husika.

Sina ufahamu kihivyo wa masuala haya ( nikimaanisha Kitaaluma na Kiutendaji wake ) kama walivyo wengine ila kwa maarifa machache sana niliyonayo ni kwamba sehemu yoyote ile na hasa kwa tukio zima ambalo limemtokea Mtani wangu wa Kinyiramba Mheshimiwa Mbunge Tundu Lissu kamwe hata kama liwe limekuwa ' coordinated ' na ' anonymous Fellas ' ila kwa 99% lazima pia kutakuwa na Watu wa karibu na Mlengwa / Mhusika wametumika katika kulifanikisha. Mifano ya hii iko mingi sana karibia Watu wengi ambao walikuwa ' assassinated ' ilikuja kugundulika baadae kwamba hata Watu wao wa karibu nao walihusika either directly or indirectly sasa nashangaa kwa hili la Tundu Lissu Watu wake wa karibu ama Kifamilia au Kichama wakigusiwa tu katika kutengeneza mtiririko mzima wa Kiushahidi na Kiuhalisia Watu wenye Mahaba na Siasa za ' Oya Oya ' wanaanza Kuhamaki, Kununa na Kukasirika huku wakidhani kwamba kila ama anayewapinga au anayelihoji hili Kiudadisi kabisa basi ni ' Pro Government ' na ni ' Anti Opposition '. Siasa za Kitanzania zimetufikisha pabaya mno ambapo hazitaki kuruhusu ' Fact Finding ' badala yake zimejikita katika ' rumors ' na ' double standards ' pekee.

Nina uhakika kabisa tena wa 100% kwamba hili jambo au Sakata la Tundu Lissu likifuatiliwa Kitaalam kama siyo Kiuweledi kabisa huenda kuna Watu wataficha Nyuso zao kwa aibu na hawatokuja Kuamini kile ambacho Kimejulikana na si ajabu kuna Watu wanaweza hata wakachinjana hasa kwa hasira za Kupotezeana muda na Kufitiana wao kwa wao. Ni suala la muda tu najua kadri siku zinavyoenda mbele ipo siku ukweli wa haki utajulikana na labda nimwombe tu Tundu Lissu kwamba siku ambayo labda atakuja Kuujua ukweli wa Yeye leo hii Kupewa Kilema kile asisite tena kuandika Waraka wake kutuomba radhi Sisi ambao tumefululiza Kutukanwa juu ya hili sakata lake.

Siku zote nasema na nitasema kwamba Wahenga waliposema KIKULACHO KI NGUONI MWAKO wala hawakukosea!

Akhsanteni na nawatakieni pia uchangiaji mwema wa huu Uzi wa Kaka yangu Mpendwa Kitasnia na Amani itawale Kwenu.
Umemaliza kila kitu
 
Ila upande Wa pili Wa hoja hii ya Pascal naona kama lengo lake ni kuchokoza mada hii ili watu watiririke ukweli upatikane maana na yeye anakerwa na ukimya huu Wa serikali mwaka mmoja baada ya tukio.
Kama ni hivyo naendelea kumsifu kwa weledi huo.
 
duh! Pascal hauhitaji kuwa na shahada ya forensic science kuwajua wahusika wa tukio hili... kiukweli Pascal unayumba
 
Dereva ni kiungo cha pande 2 kati ya mshambuliwaji na mshukiwa wa shambulizi ili jibu liwe rahisi la upande mmoja ajitokeze ili mdajala upande wake ufungwe
 
Bandiko hili la mayala limeambatanishwa na njaa isiyo na kifani kwenda kwa JIWE.Walahi asipokumbukwa sitashangaa kuona mayala ana kwashakoo.
 
Pascal,
Nashukuru kwa uzi wako a


kabla ya ku

Pascal, Humu ndani kwa hivi sasa 'rational thinkers' wamekaa pembeni kutokana na kujaa upupu. wengi wetu hatupendi kuumiza mbongo zetu kwa kutafakari na kutafiti . Hivi sasa kumejaa wale ambao husukumwa aidha na hisia. Ila kwa kuendeleza mjadala huu ninadhani tuanze kivingine kwa mfano
1. Hivi mheshimiwa alikuwa tishio kubwa kwa nani kwa nini?
2. Jee Mh. TL alikuwa tishio kuliko Mabere Marandu, Mrema na Lowassa?
3. Jee kifo chake kingemnufaisha nani zaidi?
4. Jee uchaguzi gani ulikuwa unakaribia kiasi awe tishio?
5. Jee huko nyuma hakukuwa na viongozi ndani ya chama hicho ambao walilalamika kuwa wanatishiwa maisha yao kutokana na kupingana kimtizamo ndani ya chama?
6. Jee kuna yeyote kati ya hao waliotishiwa kukatishwa maisha yao?
7. Nani alinufaika [kama walifariki].
8. Jee vyombo vya serikali kweli vinahusika?
i. Kwa nini vinahusika
ii. Kama kuna mkono wa dola kwenye shambulio lile, jee kuna uwezekano wa kuwepo mkono wa dola?
iii. Kama dola ilihusika kwenye lile shambulio, Jee wataalam walenga shabaha ni wa bovu kiasi cha
kutumia sasi zaidi za 15 na bado wasifanikiwe?
Naomba tuendeleze kujiuliza maswali rational kadiri iwezekanavyo na tutumie logic kutafuta majibu nadhani kwa hilo tunaweza japo tukapata mwanga wa kufahamu japo kinadharia ni akina nani wanahusika.
[
Kwa wenye iq kubwa ulichoandika na unayoyauliza, ama una iq ndogo size ya kichaa wetu au uko na kazi ya jiwe kwa malipo ya kodi zetu. Anyway km ni iq nikusaidie kidogo kuwa pakuanzia ni mtu mbunge amepigwa risasi hata km ingekuwa 1 sasa maswali unanza
1. Uchunguzi unafanywa na nani? Jb = serikali ya jiwe
2. Je kuna uchunguzi umefanyika? Jb = hapana
3. Why haujafanyika? Jb = tuna katiba mbovu ambayo imeweka madaraka yote kwa kichaa
4. Je aliyepigwa risasi anamshakia nani? Jb = kichaa jiwe
5. Why amshakie kichaa jiwe? Jb = upo ushahidi alishasema 'Lissu ni msaliti na anatakiwa apotee'
6. So tunafanyeje? Jb = ondoa kichaa jiwe na genge lake by any means necessary kisha ruhusu serikali ifanye kazi yake, kuchunguza yote ya kina lissu, saanane, azori, mawazo, yona na wengine wote

Nje ya haya km uko kazini endelea ila jua iko siku watz wengi ujinga utawatoka na uvumilivu utafika mwisho na watasema INATOSHA
 
Siku hizi unajidhalilisha sana mkuu!
Sikufichi kakaangu umekuwa kama umefungwa motor

Ewe mtanzania mwenzangu jitahidi sana usije kudhubutu kutafuta chakula cha watoto wako kwa njia haramu namna hii!
Inaudhi, inakera na kukiacha kizazi chako na laana

Kwahiyo dereva wa Lisu anaweza kuwa na nguvu na ushawishi wa kuandaa mazingira ya namna ile hadi kuwaondoa walinzi wa serikali eneo lile?
CCTV camera pia akaziondoa na mwisho kabisa akaishawishi serikali na bunge kwa ujumla wasihusike na matibabu yake?

Nanukuu: "Wakati nalima nikikutana na nyoka namgonga kichwa. Akifa shauri yake na akipona shauri yake"

Hiyo ni kwenye ziara ya baba yetu kwenye mkoa fulani [emoji24] [emoji24]
Baba au kichaa?
 
Haya maneno ya kumuhusisha driver wa Lissu hayana mashiko kabisa. Kama ni yeye, ziko wapi CCTV Camera, kwa nini Serikali haitaki uchunguzi huru? Kama serikali haihusiki, kwa nini walinzi waliondoka eneo la tukio muda mfupi kabla ya shambulizi? Serikali inamjua aliyefanya haya, eti askari wetu hawana AK47, una akili kweli wewe? Unazijua silaha zote za nchi hii? Hao walinzi wa Rais wanatembea na SMG? Umeniboa sana kwa kushindwa kufikiri
Mwisho wa siku yeye ni shahidi/ mtuhumiwq namba moja sababu alikuwapo eneo la tukio na kwa maelezo yake aliona yaliyoyokea. Ni taratibu za dunia nzima za kipelelezi, shahidi/ mtuhumiwa namba moja lazima ahojiwe. Hili halikwepeki. Kama hausiki chq msingi ni kujitokeza ahojiwe ili taarifa zake zisaidie.
 
Maswali uliyouliza yote ya kijinga, ila tu kwa taarifa yako, hakuna uchunguzi rahisi kama huu wa swala la Lissu, na siku wakiletwa wachunguzi wa nje itachukua dakika 5 tu kuwa kamata watu wote waliohusika na huu unyama. Hiyo gari iliyoshambulia ilikua imepaki nje ya ukumbi wa bunge (Kwa mujibu wa maelezo ya awali) so lazima kulikua na mtu aliye ndani alikua anawasiliana na hao watesi kuwahahakikishia Lissu amepanda kwenye hiyo gari, kama zitachukuliwa taarifa za simu za eneo hilo kwa siku Lissu alipopigwa risasi lazima wahusika wajulikane.
Pia yawezekana huyo mtu/ watu walipewa taarifa na dereva kuwa sasa tunakuja, kaeni mkao wa kula.
 
Pasco anashangaa kuna mtu anaweza kuacha milioni 500 kwa kuuza utu wake. Wewe kama ulipewa na umeamua kudhililisha profesional yako hivi, wapo wengi wenye utu.
Aliyepigwa risasi,yupo hai na anasema attempt ilifanywa na aliyemtaja, Ke wewe uliyekusanya kusanya tu story ambaye ulikuwa mbali na tukio tukuamini kuliko yeye?
Hivi kwa akili za kawaida mtu anayetaka kukuua kweli ungemtetea?
Tunaomba zile camera tumalize utata
 
Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
Shambulizi la Lissu, Wanaomdhania Dereva Anahusika, Sio Wajinga!, Wana Hoja za Msingi!. Jee Anahusika?.
Maswali haya ni kufuatia hoja za Lissu kwenye bandiko hili.
Mhe. Tundu Lissu,
Kwanza pole sana kwa yaliyokusibu.
Umezungumza mengi kuhusu kilichotokea mwaka mmoja uliopita, ila watu wanaohoji kuhusu dereva wako, nakuomba sana usiwaite wajinga, au wametumwa, kwa sababu mashaka yao ni very valid.

Kwa vile mashuhuda ni nyinyi wawili tuu, wewe na dereva wako, then kuna mambo tungependa kujua kutoka kwa Lissu mwemyewe na dereva wake.

Hoja kuwa tumetoka naye mbali hivyo tunaaminiana, hazina mashiko mbele ya watu na kazi zao. Lissu alipotoka na dereva wake, anaweza kujilinganisha Dr. Slaa na mlinzi wake Kagenzi walipotoka?, halafu what happened?!. Kwenye mambo ya assignment, anaweza hata akatumika mke wako aliyekuzalia wanao, sembuse itakuwa dereva tuu mliotoka nae mbali!.
Baadhi ya maswali ni haya...
  1. Baada kuona kuna gari linawafuatilia, mlichukua hatua gani?.
  2. The common sense ya kufuatiliwa inaelekeza, uki note you're followed, hatua ya kwanza ni kumpote anaye kufollow kwa makusudi, ili kwanza kujiridhisha kuwa anakufollow.
  3. Ukiisha jiridhisha you are followed, una change direction kumpoteza maboya.
  4. Ukimuona bado yupo, then kama uko fit, unamlengesha mahali kwenye kona ambapo hawezi kuchomoka, mnamalizana!.
  5. Kama hauko fit, unamlengesha kwenye safe area ,usually sehemu open kwenye makundi ya watu na kumripoti kunakohusika.
  6. Baada ya kuona mnafuatwa, kwa nini mliendelea kuelekea nyumbani?.
  7. Mlipofika mkasimama, mkawaona watu wawili wanashuka na AK 47, kitendo tuu cha kujua tuu bunduki zile ni AK 47, hii maana yake ni close proximity, kwenye shooting that close!, risasi 38!, dereva huyu amesalimikaje asipitiwe hata na moja?.
  8. Ametokaje kwenye gari na kujificha chini ya gari ya jirani bila kugundulika?!.
  9. Anafichwa nini kuhojiwa?, kuna nini kinafichwa?.
  10. Maswali haya yameendelea kwa msaada wa mwana jf huyu

  11. Bunduki iliyotumika waliiona ni AK 47 iliyokuwa na full magazine (risasi 40) ambayo ilimimina risasi zote 40 at close range. Kati ya hizo 17 zilizama kwenye miguu, mikono na kiuno cha Tundu Lissu.
  12. Risasi zilimiminwa kutoka upande wa kulia wa gari ambao ni upande wa dreva lakini dreva hakupatwa na risasi hata moja na alipata hata fursa ya kuteremka kwenye gari na kwenda ku take cover kwenye magari yaliyokuwa yamepaki eneo hilo. Assailants walikuwa upande wa kulia wa gari, hivyo risasi zilizama zaidi kwenye mguu wa kulia, paja la kulia, mkono wa kulia, kiuno upande wa kulia na kutokea tumboni na mkono wa kushoto. These are the documented medical forensic clues.
  13. Majeshi yetu hayana bunduki za AK 47, yana SMG badala yake ambayzo full magazine zake ni risasi 30. Bunduki za AK47 zinamilikiwa na majambazi yanazozipata kutoka kwa wanajeshi wa Burundi wanaokimbilia Tanzania ambao huwa wanaziuza kwa bei ya shillingi 20,000 tu!! Silaha hizi ndizo zilitikisa huko Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
  14. Hakuna mwanajeshi ye yote (aliyepata mafunzo ya kijeshi) ambaye ampige mtu (adui) risasi 38 from an AK 47 gun at a close range halafu mtu huyo asalimike!! Never on earth. Kwanza atahitaji risasi moja tu na atafumua kichwa au moyo. Hivyo it is so obvious kwamba assailants wa Tundu Lissu walikuwa ni wahuni tu wa mitaani wasiojua kutumia bunduki. Yaani risasi 38 zote zinakosa target (kichwa au moyo) zinaishia kupiga makalio na hewa!! Hili halihitaji askari wa Scotland yard kulitambua. Swali ni nani aliwakodi hawa wahuni wasiojua shabaha? Kwa nini dreva wa Lissu akawa mkimbizi nchi za nje? Nini kakimbia? Kwani hata polisi wetu wakienda kumhoji huko kwani atasema lo lote la maana? Huko hawawezi kumu arrest. Alipaswa kuwa behind bars ili aeleze vizuri. Tundu Lissu alipaswa kujua hili. Mara nyingi kikulacho unacho nguoni mwako. Eti ninamuamini sana. Mbele ya pesa kunakuamini mtu? Yaani apewe shillingi million 500 aache kukumaliza? Yaani Tundu Lissu hajui kwamba "Money is the source of all evils in this world?"
  15. Hospitali ya serikali ya Dodoma na madaktari wa serikali wa Dodoma hospital ndiyo waliookoa maisha yake. Kama serikali ilikuwa na mpango wa kumuua, ingalishindwaje kumumalizia hapo hapo kwenye hospitali yake ya Dodoma humo humo operation theatre? It was so simple eg hiyo damu aliyopewa hangeipata au angalipewa incompatible blood ambayo ingalimumaliza hapo kwa hapo! Lazima aishukuru serikali kwa kuokoa maisha yake badala ya kuilaumu. Upinzani haupaswi kuwa wa aina hii. Tujifunze kwenye nchi zilizotutangulia.
  16. Bunduki kama AK 47 au SMG ikiunguruma si mchezo. Kwa askari yo yote trained, hata kama naye ana bunduki ya aina hiyo hiyo lakini kashutikizwa, reaction ya kwanza ni ku take cover. Atalala chini na ku craw hadi mahala salama. Hapo ndipo atatafuta kuona adui/ maadui walipo na kutafakari kama anao uwezo wa kupambana nao au kuomba reinfocement au kutokomea kabisa kwenye eneo hilo. Trained soldier hakurupuki tu kuanza kurusha risasi ovyo ovyo anapositukizwa na milio ya risasi. Hivyo kwa jinsi tukio lilivyotokea hapo usingalitarajia askari waliokuwa karibu na eneo hilo kuwa wangaliweza kuanza kujibu mapigo kwa muda huo mfupi uliotumika kabla ya majambazi hayo kutokomea kusikojulikana. Dreva wa Lissu aliyaona live na alitaja hata aina ya gari yalilotumia na plate namba zake. Polisi walikamata magari kadhaa ya aina hiyo lakini dreva huyo alikataa kwenda kuyatambua na hivyo yakabidi yaachiwe kwani hakuna shahidi aliyejitokeza. Shahidi muhimu alikuwa Nairobi akidaiwa anapata tiba ya kisaikolojia. Sasa hivi Lissu anasema dreva huyo yuko masomoni Ubeligiji. Sijui anasoma digrii gani hapo Leuven University teaching hospital anapotibiwa boss wake. Jamani aacheni kutufanya wajinga. Pascal yuko sahihi kabisa.
  17. Huko nyuma niliisha wahi kuzungumza haya kuhusu dereva wa Lissu.

Mpaka sasa the situation ya shambulio la Lissu as it is, limefanywa na watu wasiojulikana. Serikali yetu imeshindwa kuwabaini, lakini sisi watu wa media, tunaweza kusaidia kama nilivyosema hapa.
WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
Hitimisho.
The only defence ya Dereva wa Lissu has nothing to do na hiyo shooting, ni uzito tuu wa serikali yetu kufanya upelelezi wa tukio hili na kugoma kuita wachunguzi wa nje. Ingekuwa ni inside job ya Chadema, tungeshuhudia serikali fasta ingechunguza!.

Lakini kwa vile wasiojulikana ni hawa
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums

Tusitegemee lolote jipya hapa.
Tundu Lissu, just get well soon, na sasa inakubidi uchangue kati ya kuendelea na uanaharakati na kuishi kwa mashaka, au uamue kupunguza makali na kuishi kwa amani.

Pole Sana Mhe. Tundu Lissu, Get Well Soon.
P.
Rejea
Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums

Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?! - JamiiForums

Tundu Lissu: Polisi wa Tanzania hawana mamlaka ya kunihoji nikiwa Kenya au kwingineko nje ya mipaka ya Tanzania - JamiiForums

P.
Umejiona shujaa wa kuuliza maswali ya weledi? Kumbe wewe wa hovyo!
Hujiulizi
1. Kwanini sehemu yote hiyo ambayo inalindwa saa 24/7/30/365 days hapakuwa na mlinzi hata mmoja?
2. Kwanini CCTV camera zilinyofolewa mara baada ya tukio
3. Kwanini wanakataa independent investigation
4. Kwanini wasiende belgium kumhoji kama wana nia ya kweli/hawahusiki?
5. Kwanini serikali inaktaa watu kumwombea Lisu
6. kwanini serikali inaktaa watu kuvaa t shirt zenye picha na maandishi ya Lisu
7. Barabara nzima toka bungeni kuja kwa Lisu and his fellow Mps haikuwa na gari hata moja, kulikoni?

Ulitishwa Bungeni ukatishika, leo unajitokeza kutafuta uDC!
 
Back
Top Bottom