Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Ulichoandika hapa ni kuonyesha kwamba una uwezo wa kufikiri na hata ukipewa kazi ya kutetea watuhumiwa wa kumshambulia Lissu unaweza kutetea kwa kiwango fulani kimantiki. Hii ni haki yako kutumia akili yako kwa jambo lolote ambalo una maslahi nalo ama kwa kuwiwa kufanya hivyo. Lakini napenda nikuambie kwamba utetezi wako huu ungeweza kufanya kazi sehemu ambayo kuna watu wenye upeo finyu. Kama askari waliokuwepo eneo hilo walitishika na mlio wa hiyo AK47, je CCTV Camera nazo zilitishwa na nini? Pole ndugu, hata kama una maelezo yenye mantiki lakini kumbuka huwezi kuficha ukweli kwa maelezo mazuri. Hapa ulichoandika ni sawa na kuanika nguo kavu.
Hivi unaijua teknolojia ya CCTV wewe? Unazani ndiyo mwarobaini ya mambo yote. It is not that simple. Huko ulaya ambako kuna ma cctv kila sehemu, tena ya high definition na zoom za 360 degrees bado magaidi na wahalifu wengine wanaendelea kufanya mambo yao bila msaada wa maana wa kutambuliwa kutoka kwa hayo ma cctv. Sembuse hizi za kwetu zenye ubora duni ambao ukiwa umbali wa zaidi ya mita mbili picha zake ni vivuli vivuli tu. Huwezi pata sura ya kumtambua mhalifu kama hao walioficha sura zao kwa kushusha chini kofia zao za kapero na kuvaa miwani myeusi (kwa maelezo ya dreva wa Lissu aliyewaona live). Kwa aina zetu za cctv ili waweze kuzi study vizuri images zake polisi ni lazima waende nazo kwenye kitengo chao maalum kwa kazi hiyo. Inawabidi waondoke nazo.
 
Hapa ndani uwezekano wa kufanya uchunguzi upo lakini kwa mujibu wa Lissu mwenyewe ambaye ni mhanga wa huo unyama,mtuhumiwa wake wa kwanza ndio hao unaotaka wafanye uchunguzi.Huhitaji kuwa na Phd kujuwa huo uchunguzi utakuwa wa magumashi.
Basi ingekua hatari kama kila mhanga atachagua nani aendeshe kesi au uchunguzi wake.Ukiangalia hata mahakaman kuna kumkataa hakimu lkn ndio uwe na hoja za mcng.Je hoja za mcng za lisu ni zipi?
 
Mkuu inaonekana umejibu watu wengi mpaka hujui nilikuambia hiyo jana. Nakubali kabisa dereva ni shahidi, awe namba moja au mbili kwangu hiyo sio tatizo. Na sio dereva tu, hata Lissu ni shahidi tena anapaswa kuwa namba moja kwani ndiye aliye shambuliwa na bado yuko hai na aliona hilo shambulio.

Lakini kama ni huyo dereva alikuwa hapo Kenya, Lissu alisema waende wakawahoji wote na wako tayari. Tulio wengi tunafahanu jeshi letu halifanyi kazi kwa weledi kwani linaamini kwenye matumizi ya nguvu. Linachotaka ni huyo dereva aje apewe kipigo ili limuwekee maneno mdomoni kwa nia ya kufunika kombe. Ni kipi kililifanya jeshi letu lisiende hapo Kenya kumuhoji? Kipi kinashindikana kwenda hapo ubeligiji kumuhoji dereva na huyo Lissu? Mbona kamati ya kina Mwakyembe ilienda mpaka US kupata ukweli wa richmond? Misuli hii mada imejaza watu kibao wa system, kila mmoja anarusha kete yake, ni kipi haya maoni hayafanyiwi kazi?

Narudia tena, Shambulizi lile ni aina ya siasa chafu kutokea hapa nchini, tutakuwa watu wa ajabu kufumbia macho uovu ule kisa aliyefanyiwa huo unyama hakuwa mshabiki wa utawala uliopo. Hakuna haja ya kupoteza muda kwa kuokoteza utetezi dhaifu ili kubadili ukweli ule. Tufungueni ukurasa mpya na iwe mwisho wa siasa za majukwaani kujibiwa kwa mashambulio ya risasi.
Sio ndio huyo lisu alisema police Tanzania haina haki ya yy kwenda kumhoji huko Kenya na kutaka kuhojiwa na police wa Kenya? Au huwa hamkumbuki ya nyuma?
 
Hivi unaijua teknolojia ya CCTV wewe? Unazani ndiyo mwarobaini ya mambo yote. It is not that simple. Huko ulaya ambako kuna ma cctv kila sehemu, tena ya high definition na zoom za 360 degrees bado magaidi na wahalifu wengine wanaendelea kufanya mambo yao bila msaada wa maana wa kutambuliwa kutoka kwa hayo ma cctv. Sembuse hizi za kwetu zenye ubora duni ambao ukiwa umbali wa zaidi ya mita mbili picha zake ni vivuli vivuli tu. Huwezi pata sura ya kumtambua mhalifu kama hao walioficha sura zao kwa kushusha chini kofia zao za kapero na kuvaa miwani myeusi (kwa maelezo ya dreva wa Lissu aliyewaona live). Kwa aina zetu za cctv ili waweze kuzi study vizuri images zake polisi ni lazima waende nazo kwenye kitengo chao maalum kwa kazi hiyo. Inawabidi waondoke nazo.

Narudia tena kukuambia, ww una uwezo mzuri wa kujieleza na unaongea kwa mantiki. Tatizo unajaribu kutumia uwezo wako kugeuza ukweli kuwa uongo. Usipoteze muda wako kumlaumu dobi kwani kaniki ndio rangi yake. Hili suala la Lissu liko kama anavyolisema, tumia uwezo wako kuelezea jinsi mwili wa binadamu unavyofanya kazi na sio kubadili ukweli wa shambulio la Lissu. Ona aibu kutumia uwezo wako kutetea uovu. Tufungue ukurasa mpya, ile ilikuwa ni siasa chafu, full stop.
 
pascal Mayala,jibu swali hili,

Kwa nini Uongozi wa bunge na wabunge wa CCM hawajawahi kutoa pole kwa Lissu au kwenda kumuona?

Wewe pia unajua kwa nini bunge lilikataa kumtibia

Leo hii unakuja na andishi kama hili,tunatatizo kubwa la waandishi wa habari nchi hii
 
Paskali toka uitwe kwenye kamati ya maadili ya Bunge naona hujakaa sawa..kiakili.
 
Sio ndio huyo lisu alisema police Tanzania haina haki ya yy kwenda kumhoji huko Kenya na kutaka kuhojiwa na police wa Kenya? Au huwa hamkumbuki ya nyuma?

Misuli nimekuambia hili suala tukubali tu ilikuwa ni siasa chafu, tufungue ukurasa mpya maana hapa sioni anayeweza kuugeuza ukweli wa nani aliyetuma watu wa kumshambulia. Lissu kaongea meengi sana, lakini kwenye maongezi yake yote kuna mtu mmoja anamtaja kila mara kama msukumo wa shambulio hilo. Sasa kama unataka kubeba hayo maneno fulani eti alisema polisi haina haki na unataka kufanya ni utetezi wa hii post, mbona usikubali na huyo anayemtaja kila mara kama sababu ya yeye kushambuliwa?

Usipoteze muda wako adhimu kutetea uovu kisa madaraka. Nakubali una mantiki kwenye hoja zako, lakini hata uwe na mantiki vipi huwezi kubadili ukweli.
 
Narejea kauli za huyohuyo unayemuamini kuwa anamjua aliyefanya ashambuliwe.Niambie Kwa maelezo yake CCTV zilikua nyumban kwake,nani alizitoa?
 
Waliotaka kumuua lissu, kama wangekuwa na mpango wa kumtumia dereva wake, wasingetumia nguvu kubwa kiasi kile.
 
Waliotaka kumuua lissu, kama wangekuwa na mpango wa kumtumia dereva wake, wasingetumia nguvu kubwa kiasi kile.
Iliwezekana vipi wauaji wasubiri lisu ashushe kiti na alale kifudifudi,dereva ashuke kujificha chini ya gari ndo mvua ya risasi ianze?Huoni hii ni movie ya kichina?
 
Wanabodi

Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
Shambulizi la Lissu, Wanaomdhania Dereva Anahusika, Sio Wajinga!, Wana Hoja za Msingi!. Jee Anahusika?.
Si maanishi kuwa dereva wa Lissu anahusika, bali mazingira ya tukio, yanahalisha wadadi kujiuliza maswali kihusu tukio lenyewe, hivyo kuhisi uhusika wa dereva wa Lissu, sio jambo la ajabu, tena uhusika wenyewe sio lazima uwe expressly but impliedly kwa negligence iliyopelekea Lissu kuwa reached na kushumbuliwa, wakati alikuwa na uwezo.
Maswali haya ni kufuatia hoja za Lissu kwenye bandiko hili.
Mhe. Tundu Lissu,
Kwanza pole sana kwa yaliyokusibu.
Umezungumza mengi kuhusu kilichotokea mwaka mmoja uliopita, ila watu wanaohoji kuhusu dereva wako, nakuomba sana usiwaite wajinga, au wametumwa, kwa sababu mashaka yao ni very valid.

Kwa vile mashuhuda ni nyinyi wawili tuu, wewe na dereva wako, then kuna mambo tungependa kujua kutoka kwa Lissu mwemyewe na dereva wake.

Hoja kuwa tumetoka naye mbali hivyo tunaaminiana, hazina mashiko mbele ya watu na kazi zao. Lissu alipotoka na dereva wake, anaweza kujilinganisha Dr. Slaa na mlinzi wake Kagenzi walipotoka?, halafu what happened?!. Kwenye mambo ya assignment, anaweza hata akatumika mke wako aliyekuzalia wanao, sembuse itakuwa dereva tuu mliotoka nae mbali!.
Baadhi ya maswali ni haya...
  1. Kwa vile Lissu aliwahi kuripoti kufuatiliwa, kupitia press conference, kwa nini hakuripoti polisi?!.
  2. Baada ya Chadema kupokea taarifa ya Mnadhimu wake kufuatiliwa, walichukua hatua gani?.
  3. Baada kuona kuna gari linawafuatilia, mlichukua hatua gani?.
  4. The common sense ya kufuatiliwa inaelekeza, uki note you're followed, hatua ya kwanza ni kumpote anaye kufollow kwa makusudi, ili kwanza kujiridhisha kuwa anakufollow.
  5. Ukiisha jiridhisha you are followed, una change direction kumpoteza maboya.
  6. Ukimuona bado yupo, then kama uko fit, unamlengesha mahali kwenye kona ambapo hawezi kuchomoka, mnamalizana!.
  7. Kama hauko fit, unamlengesha kwenye safe area ,usually sehemu open kwenye makundi ya watu na kumripoti kunakohusika.
  8. Baada ya kuona mnafuatwa, kwa nini mliendelea kuelekea nyumbani?.
  9. Mlipofika mkasimama, mkawaona watu wawili wanashuka na AK 47, kitendo tuu cha kujua tuu bunduki zile ni AK 47, hii maana yake ni close proximity, kwenye shooting that close!, risasi 38!, dereva huyu amesalimikaje asipitiwe hata na moja?.
  10. (Mimi niliwahi kuwa mwanajeshi wa JWTZ hivyo kuna kitu nakijua kuhusu hizi AK47 ndani ya jeshi letu, lakini vitu vingine ni siri za usalama wa taifa letu, sina uhakika mtu asiyepitia JWTZ, ana uwezo gani kuijua AK 47!.)
  11. Ametokaje kwenye gari na kujificha chini ya gari ya jirani bila kugundulika?!.
  12. Anafichwa nini kuhojiwa?, kuna nini kinafichwa?.
  13. Maswali haya yameendelea kwa msaada wa mwana jf huyu
  14. Bunduki iliyotumika waliiona ni AK 47 iliyokuwa na full magazine (risasi 40) ambayo ilimimina risasi zote 40 at close range. Kati ya hizo 17 zilizama kwenye miguu, mikono na kiuno cha Tundu Lissu.
  15. Risasi zilimiminwa kutoka upande wa kulia wa gari ambao ni upande wa dreva lakini dreva hakupatwa na risasi hata moja na alipata hata fursa ya kuteremka kwenye gari na kwenda ku take cover kwenye magari yaliyokuwa yamepaki eneo hilo. Assailants walikuwa upande wa kulia wa gari, hivyo risasi zilizama zaidi kwenye mguu wa kulia, paja la kulia, mkono wa kulia, kiuno upande wa kulia na kutokea tumboni na mkono wa kushoto. These are the documented medical forensic clues.
  16. Majeshi yetu hayana bunduki za AK 47, yana SMG badala yake ambayzo full magazine zake ni risasi 30. Bunduki za AK47 zinamilikiwa na majambazi yanazozipata kutoka kwa wanajeshi wa Burundi wanaokimbilia Tanzania ambao huwa wanaziuza kwa bei ya shillingi 20,000 tu!! Silaha hizi ndizo zilitikisa huko Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
  17. Hakuna mwanajeshi ye yote (aliyepata mafunzo ya kijeshi) ambaye ampige mtu (adui) risasi 38 from an AK 47 gun at a close range halafu mtu huyo asalimike!! Never on earth. Kwanza atahitaji risasi moja tu na atafumua kichwa au moyo. Hivyo it is so obvious kwamba assailants wa Tundu Lissu walikuwa ni wahuni tu wa mitaani wasiojua kutumia bunduki. Yaani risasi 38 zote zinakosa target (kichwa au moyo) zinaishia kupiga makalio na hewa!! Hili halihitaji askari wa Scotland yard kulitambua. Swali ni nani aliwakodi hawa wahuni wasiojua shabaha? Kwa nini dreva wa Lissu akawa mkimbizi nchi za nje? Nini kakimbia? Kwani hata polisi wetu wakienda kumhoji huko kwani atasema lo lote la maana? Huko hawawezi kumu arrest. Alipaswa kuwa behind bars ili aeleze vizuri. Tundu Lissu alipaswa kujua hili. Mara nyingi kikulacho unacho nguoni mwako. Eti ninamuamini sana. Mbele ya pesa kunakuamini mtu? Yaani apewe shillingi million 500 aache kukumaliza? Yaani Tundu Lissu hajui kwamba "Money is the source of all evils in this world?"
  18. Hospitali ya serikali ya Dodoma na madaktari wa serikali wa Dodoma hospital ndiyo waliookoa maisha yake. Kama serikali ilikuwa na mpango wa kumuua, ingalishindwaje kumumalizia hapo hapo kwenye hospitali yake ya Dodoma humo humo operation theatre? It was so simple eg hiyo damu aliyopewa hangeipata au angalipewa incompatible blood ambayo ingalimumaliza hapo kwa hapo! Lazima aishukuru serikali kwa kuokoa maisha yake badala ya kuilaumu. Upinzani haupaswi kuwa wa aina hii. Tujifunze kwenye nchi zilizotutangulia.
  19. Bunduki kama AK 47 au SMG ikiunguruma si mchezo. Kwa askari yo yote trained, hata kama naye ana bunduki ya aina hiyo hiyo lakini kashutikizwa, reaction ya kwanza ni ku take cover. Atalala chini na ku craw hadi mahala salama. Hapo ndipo atatafuta kuona adui/ maadui walipo na kutafakari kama anao uwezo wa kupambana nao au kuomba reinfocement au kutokomea kabisa kwenye eneo hilo. Trained soldier hakurupuki tu kuanza kurusha risasi ovyo ovyo anapositukizwa na milio ya risasi. Hivyo kwa jinsi tukio lilivyotokea hapo usingalitarajia askari waliokuwa karibu na eneo hilo kuwa wangaliweza kuanza kujibu mapigo kwa muda huo mfupi uliotumika kabla ya majambazi hayo kutokomea kusikojulikana. Dreva wa Lissu aliyaona live na alitaja hata aina ya gari yalilotumia na plate namba zake. Polisi walikamata magari kadhaa ya aina hiyo lakini dreva huyo alikataa kwenda kuyatambua na hivyo yakabidi yaachiwe kwani hakuna shahidi aliyejitokeza. Shahidi muhimu alikuwa Nairobi akidaiwa anapata tiba ya kisaikolojia. Sasa hivi Lissu anasema dreva huyo yuko masomoni Ubeligiji. Sijui anasoma digrii gani hapo Leuven University teaching hospital anapotibiwa boss wake. Jamani aacheni kutufanya wajinga. Pascal yuko sahihi kabisa.
  20. Huko nyuma niliisha wahi kuzungumza haya kuhusu dereva wa Lissu.

Mpaka sasa the situation ya shambulio la Lissu as it is, limefanywa na watu wasiojulikana. Serikali yetu imeshindwa kuwabaini, lakini sisi watu wa media, tunaweza kusaidia kama nilivyosema hapa.
WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
Hitimisho.
The only defence ya Dereva wa Lissu has nothing to do na hiyo shooting, ni uzito tuu wa serikali yetu kufanya upelelezi wa tukio hili na kugoma kuita wachunguzi wa nje. Ingekuwa ni inside job ya Chadema, tungeshuhudia serikali fasta ingechunguza!.

Lakini kwa vile wasiojulikana ni hawa
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums

Tusitegemee lolote jipya hapa.
Tundu Lissu, just get well soon, na sasa inakubidi uchangue kati ya kuendelea na uanaharakati na kuishi kwa mashaka, au uamue kupunguza makali na kuishi kwa amani.

Pole Sana Mhe. Tundu Lissu, Get Well Soon.
P.
Rejea
Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums

Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?! - JamiiForums

Tundu Lissu: Polisi wa Tanzania hawana mamlaka ya kunihoji nikiwa Kenya au kwingineko nje ya mipaka ya Tanzania - JamiiForums

P.
Actually wewe ni puuzi sana. Lakini sio kosa lako pia...wasukuma kwa kadri ya uelewa wangu, ni watu wa ajabu sana. Na tatizo linajulikana kabisa kabisa.. ni "lack of traditional governing system" ambao ndio msingi muhimu wa kila jamii.....ethics na mambo mengine muhimu sana ya kijamii yanajengwa mle...Sasa hawa ndugu zetu hayo hayapo.....

Upuuzi mwingi wa huyu bwana ni matokeo ya kukosekana kwa misingi hiyo..
 
Narejea kauli za huyohuyo unayemuamini kuwa anamjua aliyefanya ashambuliwe.Niambie Kwa maelezo yake CCTV zilikua nyumban kwake,nani alizitoa?

Misuli don't waste your precious time on this matter. Huna utetezi wowote wenye mashiko zaidi ya kujitahidi kufunika kombe mwanaharamu apite. Nimekuambia ulicho nacho ni utetezi wenye mantiki, lakini huna uwezo wa kubadili ukweli. Ukweli huwa haubadilishwi na hoja zenye mantiki. Hapa ni kama unazuia tu risasi na debe.
 
Hahahahah ni hatar sana.Hoja zenye mantiki ndizo zinazojenga ukweli.Kuongea sana kwa lisu bila logic yyt ukweli unautoa wapi?Katika kujua ukweli moja ya hoja zilikua ni CCTV camera zilitolewa,lkn leo kuna hoja ya hizo CCTV camera zilikua nyumban kwa lisu.Huoni hapa ukweli mliokarrshwa unaweza kubadilika?Au saizi hamruhusu hoja yyt mpya nje ya mlizopewa na kuambiwa ndio sahihi?
 
Msaada wa bure tu. .nowadays money is not the source of all evils. But fame is the source of all evils braza kaka kama hukuwa unajua
 
Hii umefeli sana mkuu .
Binafsi nilikuwa namkubali sana Paschal Mayalla kabla, lakini kwa hili nimekutoa kwenye kundi la waandishi/wachambuzi wabobezi, nimeipitia maelezo yako napata taabu saana kuelewa kama kweli ni Paschal Mayalla niliyemfuatilia makala zake kwenye magazeti ya Raia mwema na Rai ile original, sipati jibu, Hivi unategemea Lissu angeenda kuripoti polisi kufuatilia na wahalifu nini kingebadilika, (kesi ya ngedere umpelekee nyani), Polisi ndio hao hao washirika wakuu wa washambuliaji, naamini they know each and everything. tuletee ushahidi wa dereva wa Lissu kupewa hiyo 500ml
 
Actually wewe ni puuzi sana. Lakini sio kosa lako pia...wasukuma kwa kadri ya uelewa wangu, ni watu wa ajabu sana. Na tatizo linajulikana kabisa kabisa.. ni "lack of traditional governing system" ambao ndio msingi muhimu wa kila jamii.....ethics na mambo mengine muhimu sana ya kijamii yanajengwa mle...Sasa hawa ndugu zetu hayo hayapo.....

Upuuzi mwingi wa huyu bwana ni matokeo ya kukosekana kwa misingi hiyo..
Haya matusi ndio Uhuru wa kutoa maoni?Hizi ndio hoja zenyewe?Nyinyi ndio mnaofanya hili jukwaa lisitofautiane na fb au insta.
 
Hahahahah ni hatar sana.Hoja zenye mantiki ndizo zinazojenga ukweli.Kuongea sana kwa lisu bila logic yyt ukweli unautoa wapi?Katika kujua ukweli moja ya hoja zilikua ni CCTV camera zilitolewa,lkn leo kuna hoja ya hizo CCTV camera zilikua nyumban kwa lisu.Huoni hapa ukweli mliokarrshwa unaweza kubadilika?Au saizi hamruhusu hoja yyt mpya nje ya mlizopewa na kuambiwa ndio sahihi?
Misuli, mbona unatumia nguvu nyingi sana kubadiri ukweli uliopo ?, Kuondolewa CCTV Cameras wewe unaona ni jambo dogo na la kawaida ?. (type ya Musiba)
 
Haya matusi ndio Uhuru wa kutoa maoni?Hizi ndio hoja zenyewe?Nyinyi ndio mnaofanya hili jukwaa lisitofautiane na fb au insta.
Ni facts sio matusi lkn kama ni matusi kwako hapana shaka jiwe limekupata sawa sawa...
 
Back
Top Bottom