Waheshimiwa wanabodi,
Niliwahi kuuliza humuhumu kuhusu mengi hayo uliyoandika lakini kwa vile wengi wetu tunapenda ku-brand kila anayepinga hoja kuhusu hili anaonekana ni mpumbavu au mwana ccm.
1.Uongozi wa Chadema hawajawahi kuripoti kwenye kituo chochote kile cha polisi kuhusu
kufuatwa na gari wasilolijua[ Dodoma ni mji mdogo tu njia za kuingia na kutoka na chache
hivyo ingekuwa rahisi sana kulipata hilo gari kama wangeripoti.
2. Mara baada ya tukio ambapo mheshimiwa Lissu alipelekwa hospitali ya Mkoa ili utaratibu ufanye kupelekwa
Muhimbili na baadaye kupelekwa nje kwa matibabu, Uongozi wa Chadema ulisema wazi wazi kuwa hawakuwa na
imani na serikali hivyo wasingempeleka Muhimbili bali wangemsafirisha wenyewe kwenda nje.
3. Hawakutoa ushirikiano wa aina yoyote ile na police na mbaya zaidi, Shahidi muhimu
ambaye ndiye alikuwa dereva wa gari hilo walimkimbizia nairobi pamoja na mgonjwa
4. Mimi sijawahi kuwa mwanajeshi ila nina fahamu kuwa kwa range waliokuwepo kina mheshimiwa, haiwezekani kwa mwanajeshi kumkosa kwa idadi ya risasi zilizotumika.
5. Hilo suala la dereva kukoswa na risasi hata moja bila ya maelezo ni ngumu kuamini.
6. Hivi inaingia akilini eti unafuatwa na watu usiowajua halafu unakimbilia nyumbani????
7. Madereva wengi wa viongozi hufundishwa defensive driving. Imekuaje kwa huyu dereva?
Kwa ufupi kuna maswali mengi kuliko majibu na hakuna kiongozi yeyote aliyoclarify haya na kilichokuwepo ni kwamba serikali inahusika.
Hivi nimekuwa nikijiuliza hivi Mh. TL alikuwa tishio kwa serikali?
Jee uchaguzi ulikuwa unakaribia?
Hivi Mh. Lowassa na Mrema[kwa wakati wake] hawakuwa tishio? Mbona wanadunda mpaka leo?
Mimi ninaamini kuwa majibu yote haya yatajulikana siku moja ila nina uhakika kuna watu ambao sasa wanapiga makelele watainamisha vichwa vyao chini.