Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Jiulize kati ya kelele na honi mfululizo na milio mfululizo ya risasi ipi ingeweza kuleta taharuki na kuhakikisha wanausalama wanafika kwenye eneo lile on time?? Ulitaka washuke wakati tayari wameshawaona watu wasiojulikana wakiwa na silaha pembezoni mwa gari lao?? Kwanini mnajitoa ufahamu?

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwenye hatari utafanya kila kitu ili uwe salama kwa nini hakuendesha gari kwenda Polisi? Wacha kushabikia usiyoyajua huu mchezo wa Chadema unajulikana na TL sio wa kwanza. Uliza ya Chacha Wangwe?
 
Kwenye hatari utafanya kila kitu ili uwe salama kwa nini hakuendesha gari kwenda Polisi? Wacha kushabikia usiyoyajua huu mchezo wa Chadema unajulikana na TL sio wa kwanza. Uliza ya Chacha Wangwe?

..hakukuwa na haja ya kwenda kituo cha Polisi.

..Area D ktk makazi ya TL ni eneo linalolindwa 24/7.

..sasa ni nani aliondoa walinzi wote kuanzia wa getini mpaka wanaolinda kwa Naibu Spika na kwa mawaziri?

..
 
Ni kweli ila kama alishutuka mapema alitakiwa ajiongeze kwa usalama wa boss wake. Kama aliwatambua ndio walewale akili ya ziada ilitakiwa.
Hata kwenda nyumbani anakojua kuna walinzi getini wenye silaha 24/7 ilikuwa hatua yenye akili kubwa zaidi ya kusimama petrol station yeyote.
Kwa maajabu kumbe walinzi WAMEAMRIWA kuondoka ili Lissu na dereva wauwawe.
So sad!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeye na boss wake walikuwa wanafuatuliwa kwa muda mrefu,na hili alilisema boss wake. Mpaka akadiliki kudai kuna vijana wa Mkuu mmoja sasa balozi aliwakaba pale St peters.Sasa kama aliona anafuatiliwa toka bungeni kwa nini asingejiongeza kumuokoa boss wake?
Hata kukimbilia nyumbani kwenye ulinzi wa silaha 24/7 ni kujiongeza, tena kwenye akili kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukila nyama ya mtu...hebu angalia walewale wakawa na hamu ya Nape tena mbele ya vyombo vya habari
Hii awamu inatupeleka kwenye uwanja wa mauwaji ya hadhara

Tusikubali kuwapa muongo mwingine hiyo 5 inawatosha
Sio kuwa inatosha tuu, bali ni lazima tuwashughulikie kwa damu zilizomwagika kwa walioua au kujeruhi.

Bila kufanya hivyo kila kiongozi tutakaye mpa ofisi hatathamini utu wa watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
K
Hapana jinai inafanyika mahala popote. Ndio maana unatakiwa uwe makini sana. Kama Laurent Kabila alipigwa risasi na mlinzi wake tena ikulu.Ije hapo area D Dodoma ampabo kila mtu anaingia muda wote? Huyu dereva ni wa kulaumiwa.
Huna hoja zaidi ya kutetea hoja ya walinzi kuondolewa ionekane haina maana. Hivi kwa akili yako dereva angejua kuna risasi zitakuja kumiminwa baadae dereva angeielekeza gari area D? Au hata petrol station angesimama?

Huyo hata geti la kambi ya jeshi angeingia nalo! Acheni hoja za kinafiki kwenye maisha ya binadamu wengine ili msijiumbie matukio kwenu wenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JokaKuu, Mkuu JokaKuu pole sana kwa kutumia nguvu nyingi kubishana na wauaji (hata muunga mkono mauaji ni muuaji pia).

Tokea lini tukio la hit and run likawa na umakini kama lile la mashindano ya range?
Hata hivyo wauaji walifanikiwa adhima yao kwani risasi 16 zilihit target na kuingia mwilini mwa Lissu. Suala la kwanini hakufa sasa wasilaumiwe hao wauaji bali wamuulize Mungu mwenyezi kwa nini hajaruhusu adhima yao?

Siku yaja ukweli utawekwa wazi kwa kuwafahamu wote kuanzia mzalisha wazo, aliyetoa amri, aliyeondoa walinzi, aliyefadhili hadi mshika AK 47

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kabisa tambua mpaka sasa haijulikani nani aliyefanya tukio lile.
Lakini sote tunafahamu bunge lipo maeneo ya mjini pale Dodoma.
Hivyo sababu tokea bungeni aliwashutukia wale jamaa angeingiza gari petro station ambayo ipo busy hata kama wangefyatua risasi ingekuwa rais kuwa track.
Au angerudi bungeni au eneo lolote salama ambalo kuna watu wengi.
Kwa nini akae kimya mpaka huko area D wanapokaa washua? Ambapo hakuna watu wengi!
Ungefahamu japo mji wa dodoma na hasa huko Area D kukoje ungeelewa vizuri.

Lakini pia ni moja ya maeneo secured,ambayo huwezi thubutu fanya uhalifu wa silaha ukatoka salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Those issues does not justify what TL or Mbowe is doing?
Ndugu andika Kiswahili tu utaeleweka. Angalia jinsi ulivyotumia broken english kwenye verb " Do", kwenye third person plural

Correct English ungeandika;
"Those issues do not justify what TL or Mbowe is doing?"

Siyo DOES! Wacha kutumia kiingereza cha Ndalichako hapa. Tumia Kiswahili tu
 


Pascal, hii ilikuwa acting ila ile ya Tundu Mugwai Lissu ilikuwa ni real alikuwa anaviziwa auwawe
Walyaga hene Mayalla? Zambi ni kutetea zambi
View attachment 1410505
Hawa wazee aina ya kina Mroto wanatakiwa wastaafu tu.

Jeshi la polisi haliwezi kuwa linasubiri taarifa iletwe ofisini ndiyo wanaanza kuifanyia kazi.

Vyanzo vyao vya taarifa ni vipi?

Watendaji hawa ndiyo wanalifanya jeshi lionekane ni la kishamba.

Taarifa yeyote ile inayopatikana kwa namna yoyote ile iwe vijiweni kwenye kahawa,daladalani,magazetini kama inamaslahi ya kuhatarisha usalama kwa namna yeyote ile ni lazima ichukuliwe na kuifanyia kazi hadi mwisho.

Haoni kama US,wakipata hata video inayoleta taharuki juu ya ugaidi inanvyozingatiwa.

Jeshi hili libakie kwa vijana,wachape kazi. Wazee mtupishe,tutawaomba ushauri itakapo lazimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maswali ya kimantiki ni hivi;

1. Ilikuwa ni kanuni hivyo ni kawaida askari
kulinda eneo ambalo Lissu alipigwa
risasi?
2. Nani walikuwa zamu siku hiyo na
kwanini hawakuwepo wakati wa tukio
3. Afisa mpanga zamu na kiongozi wa siku
hawajui waliostahili kuwa zamu siku ya
tukio?
Maswali ni mengi kuhusu walinzi wa siku hiyo. Na kama kuna vyuo vya upelelezi bila shaka wanafunzi wake wengi wangechagua nukta hiyo kuwapata wahalifu kutoka wafyatua risasi hadi mtoa maelekezo wa mwanzo!


Sent using Jamii Forums mobile app
Hii unawapa first year tu,wanakupa majibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye hatari utafanya kila kitu ili uwe salama kwa nini hakuendesha gari kwenda Polisi? Wacha kushabikia usiyoyajua huu mchezo wa Chadema unajulikana na TL sio wa kwanza. Uliza ya Chacha Wangwe?
Jinsi Serikali inavyohangaika kuwatafutia CHADEMA kesi. Hasa Mwenyekiti Mbowe mpaka wanaigeuza kesi ambayo Polisi walimuua Akwilina. Kama kungekuwa mkono wa CHADEMA huoni kama Serikali ingefungua mashtaka haraka sana dhidi ya Mbowe?
Hebu tumieni akili zenu kwa manufaa ya umma !! Mmmebakia kuzitumia akili zenu kwa kwenda chooni kuvua nguo na kuachia mzigo tu.
 
Kwenye hatari utafanya kila kitu ili uwe salama kwa nini hakuendesha gari kwenda Polisi? Wacha kushabikia usiyoyajua huu mchezo wa Chadema unajulikana na TL sio wa kwanza. Uliza ya Chacha Wangwe?
Kwa nini Jamhuri haijafungua majalada ya kifo cha Chacha Wangwe au kujeruhiwa TL dhidi ya CHADEMA mpaka leo?
 
Wanabodi

Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
"Shambulizi la Lissu, wanaomdhania dereva anahusika, sio wajinga!, wana hoja za msingi!" Swali ni Jee Dereva Anahusika?.
Si maanishi kuwa dereva wa Lissu anahusika, bali mazingira ya tukio, yanahalalisha watu wenye udadisi kujiuliza maswali kihusu tukio lenyewe, hivyo kuhisi uhusika wa dereva wa Lissu, sio jambo la ajabu, tena uhusika wenyewe sio lazima uwe expressly but impliedly kwa negligence iliyopelekea Lissu kuwa reached na watu wasiojulikana na kushambuliwa, wakati alikuwa na uwezo wa kumuepusha na shambulizi hili.
Maswali haya ni kufuatia hoja za Lissu kwenye bandiko hili.
Mhe. Tundu Lissu,
Kwanza pole sana kwa yaliyokusibu.
Umezungumza mengi kuhusu kilichotokea mwaka mmoja uliopita, ila watu wanaohoji kuhusu dereva wako, nakuomba sana usiwaite wajinga, au wametumwa, kwa sababu mashaka yao ni very valid.

Kwa vile mashuhuda ni nyinyi wawili tuu, wewe na dereva wako, then kuna mambo tungependa kujua kutoka kwa Lissu mwemyewe na dereva wake.

Hoja kuwa tumetoka naye mbali hivyo tunaaminiana, hazina mashiko mbele ya watu na kazi zao. Lissu alipotoka na dereva wake, anaweza kujilinganisha Dr. Slaa na mlinzi wake Kagenzi walipotoka?, halafu what happened?!. Kwenye mambo ya assignment, anaweza hata akatumika mke wako aliyekuzalia wanao, sembuse itakuwa dereva tuu mliotoka nae mbali!.
Baadhi ya maswali ni haya...
  1. Kwa vile Lissu aliwahi kuripoti kufuatiliwa, kupitia press conference, kwa nini hakuripoti polisi?!.
  2. Baada ya Chadema kupokea taarifa ya Mnadhimu wake kufuatiliwa, walichukua hatua gani?.
  3. Baada kuona kuna gari linawafuatilia, mlichukua hatua gani?.
  4. The common sense ya kufuatiliwa inaelekeza, uki note you're followed, hatua ya kwanza ni kumpote anaye kufollow kwa makusudi, ili kwanza kujiridhisha kuwa anakufollow.
  5. Ukiisha jiridhisha you are followed, una change direction kumpoteza maboya.
  6. Ukimuona bado yupo, then kama uko fit, unamlengesha mahali kwenye kona ambapo hawezi kuchomoka, mnamalizana!.
  7. Kama hauko fit, unamlengesha kwenye safe area ,usually sehemu open kwenye makundi ya watu na kumripoti kunakohusika.
  8. Baada ya kuona mnafuatwa, kwa nini mliendelea kuelekea nyumbani?.
  9. Mlipofika mkasimama, mkawaona watu wawili wanashuka na AK 47, kitendo tuu cha kujua tuu bunduki zile ni AK 47, hii maana yake ni close proximity, kwenye shooting that close!, risasi 38!, dereva huyu amesalimikaje asipitiwe hata na moja?.
  10. (Mimi niliwahi kuwa mwanajeshi wa JWTZ hivyo kuna kitu nakijua kuhusu hizi AK47 ndani ya jeshi letu, lakini vitu vingine ni siri za usalama wa taifa letu, sina uhakika mtu asiyepitia JWTZ, ana uwezo gani kuijua AK 47!.)
  11. Ametokaje kwenye gari na kujificha chini ya gari ya jirani bila kugundulika?!.
  12. Anafichwa nini kuhojiwa?, kuna nini kinafichwa?.
  13. Maswali haya yameendelea kwa msaada wa mwana jf huyu

  14. Bunduki iliyotumika waliiona ni AK 47 iliyokuwa na full magazine (risasi 40) ambayo ilimimina risasi zote 40 at close range. Kati ya hizo 17 zilizama kwenye miguu, mikono na kiuno cha Tundu Lissu.
  15. Risasi zilimiminwa kutoka upande wa kulia wa gari ambao ni upande wa dreva lakini dreva hakupatwa na risasi hata moja na alipata hata fursa ya kuteremka kwenye gari na kwenda ku take cover kwenye magari yaliyokuwa yamepaki eneo hilo. Assailants walikuwa upande wa kulia wa gari, hivyo risasi zilizama zaidi kwenye mguu wa kulia, paja la kulia, mkono wa kulia, kiuno upande wa kulia na kutokea tumboni na mkono wa kushoto. These are the documented medical forensic clues.
  16. Majeshi yetu hayana bunduki za AK 47, yana SMG badala yake ambayzo full magazine zake ni risasi 30. Bunduki za AK47 zinamilikiwa na majambazi yanazozipata kutoka kwa wanajeshi wa Burundi wanaokimbilia Tanzania ambao huwa wanaziuza kwa bei ya shillingi 20,000 tu!! Silaha hizi ndizo zilitikisa huko Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
  17. Hakuna mwanajeshi ye yote (aliyepata mafunzo ya kijeshi) ambaye ampige mtu (adui) risasi 38 from an AK 47 gun at a close range halafu mtu huyo asalimike!! Never on earth. Kwanza atahitaji risasi moja tu na atafumua kichwa au moyo. Hivyo it is so obvious kwamba assailants wa Tundu Lissu walikuwa ni wahuni tu wa mitaani wasiojua kutumia bunduki. Yaani risasi 38 zote zinakosa target (kichwa au moyo) zinaishia kupiga makalio na hewa!! Hili halihitaji askari wa Scotland yard kulitambua. Swali ni nani aliwakodi hawa wahuni wasiojua shabaha? Kwa nini dreva wa Lissu akawa mkimbizi nchi za nje? Nini kakimbia? Kwani hata polisi wetu wakienda kumhoji huko kwani atasema lo lote la maana? Huko hawawezi kumu arrest. Alipaswa kuwa behind bars ili aeleze vizuri. Tundu Lissu alipaswa kujua hili. Mara nyingi kikulacho unacho nguoni mwako. Eti ninamuamini sana. Mbele ya pesa kunakuamini mtu? Yaani apewe shillingi million 500 aache kukumaliza? Yaani Tundu Lissu hajui kwamba "Money is the source of all evils in this world?"
  18. Hospitali ya serikali ya Dodoma na madaktari wa serikali wa Dodoma hospital ndiyo waliookoa maisha yake. Kama serikali ilikuwa na mpango wa kumuua, ingalishindwaje kumumalizia hapo hapo kwenye hospitali yake ya Dodoma humo humo operation theatre? It was so simple eg hiyo damu aliyopewa hangeipata au angalipewa incompatible blood ambayo ingalimumaliza hapo kwa hapo! Lazima aishukuru serikali kwa kuokoa maisha yake badala ya kuilaumu. Upinzani haupaswi kuwa wa aina hii. Tujifunze kwenye nchi zilizotutangulia.
  19. Bunduki kama AK 47 au SMG ikiunguruma si mchezo. Kwa askari yo yote trained, hata kama naye ana bunduki ya aina hiyo hiyo lakini kashutikizwa, reaction ya kwanza ni ku take cover. Atalala chini na ku craw hadi mahala salama. Hapo ndipo atatafuta kuona adui/ maadui walipo na kutafakari kama anao uwezo wa kupambana nao au kuomba reinfocement au kutokomea kabisa kwenye eneo hilo. Trained soldier hakurupuki tu kuanza kurusha risasi ovyo ovyo anapositukizwa na milio ya risasi. Hivyo kwa jinsi tukio lilivyotokea hapo usingalitarajia askari waliokuwa karibu na eneo hilo kuwa wangaliweza kuanza kujibu mapigo kwa muda huo mfupi uliotumika kabla ya majambazi hayo kutokomea kusikojulikana. Dreva wa Lissu aliyaona live na alitaja hata aina ya gari yalilotumia na plate namba zake. Polisi walikamata magari kadhaa ya aina hiyo lakini dreva huyo alikataa kwenda kuyatambua na hivyo yakabidi yaachiwe kwani hakuna shahidi aliyejitokeza. Shahidi muhimu alikuwa Nairobi akidaiwa anapata tiba ya kisaikolojia. Sasa hivi Lissu anasema dreva huyo yuko masomoni Ubeligiji. Sijui anasoma digrii gani hapo Leuven University teaching hospital anapotibiwa boss wake. Jamani aacheni kutufanya wajinga. Pascal yuko sahihi kabisa.
  20. Huko nyuma niliisha wahi kuzungumza haya kuhusu dereva wa Lissu.

Mpaka sasa the situation ya shambulio la Lissu as it is, limefanywa na watu wasiojulikana. Serikali yetu imeshindwa kuwabaini, lakini sisi watu wa media, tunaweza kusaidia kama nilivyosema hapa.
WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
Hitimisho.
The only defence ya Dereva wa Lissu has nothing to do na hiyo shooting, ni uzito tuu wa serikali yetu kufanya upelelezi wa tukio hili na kugoma kuita wachunguzi wa nje. Ingekuwa ni inside job ya Chadema, tungeshuhudia serikali fasta ingechunguza!.

Lakini kwa vile wasiojulikana ni hawa
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums

Tusitegemee lolote jipya hapa.
Tundu Lissu, just get well soon, na sasa inakubidi uchangue kati ya kuendelea na uanaharakati na kuishi kwa mashaka, au uamue kupunguza makali na kuishi kwa amani.

Pole Sana Mhe. Tundu Lissu, Get Well Soon.
P.
Rejea

  1. Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums
  2. Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?! - JamiiForums
  3. Tundu Lissu: Polisi wa Tanzania hawana mamlaka ya kunihoji nikiwa Kenya au kwingineko nje ya mipaka ya Tanzania - JamiiForums
  4. Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli! - JamiiForums
    TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe! - JamiiForums
  5. Bandiko la 5 Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?! - JamiiForums
  6. Bandiko la 6 Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums
  7. Bandiko la 7 https://www.jamiiforums.com/threads...je-tukahukumiwa-karma-ndio-pekee-hutoa-hukumu
  8. Bandiko la 8 Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums
  9. Bandiko la 9 Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija - JamiiForums
  10. Bandiko la 10 WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
  11. Bandiko la 11 Siku ya Sheria: No mention of Tundu Lissu!, Je ni amesahaulika tu kutajwa, amepuuzwa au ameepukwa?!. - JamiiForums
  12. Bandiko la 12 Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi! Je, anahusika? - JamiiForums
  13. Bandiko la 13 Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela! - JamiiForums
  14. Bandiko la 14 Je, Tundu Lissu anaichafua nchi yetu au anasema ukweli wa kilichomtokea? Je, Serikali yetu iwe Proactive kusema ukweli au Reactive kumjibu? - JamiiForums
Hata kama dereva anahusika au hahusiki bado kuna mhusika mkuu ambaye mnamuogopa kumtaja>
 
Kwenye hatari utafanya kila kitu ili uwe salama kwa nini hakuendesha gari kwenda Polisi? Wacha kushabikia usiyoyajua huu mchezo wa Chadema unajulikana na TL sio wa kwanza. Uliza ya Chacha Wangwe?
Polisi kwa nini wasiwakamate sasa hao Chadema? Mtu mpumbavu hajifichi hata iweje.
 
nitajieni waliomuua binti yetu Aquiline kwanza, nami nitawatajia kwa uaminifu kabisa watu waliompiga Tundu Lissu risasi!
Kwa hiyo yakitokea mauaji, uchunguzi hakuna kwa sababu huyo aliyekufa ndio anajua kilichotokea? Tuseme ndio sababu hakuna kesi ya mauaji ya AKWILINA sababu hayuko hai? Naomba unifafanulie hapo maana mimi sijui sheria.
Wakuu Mbabe na Mindi, kwenye mauaji ya 6, kuna polisi 6 waliofyatua risasi, walishikwa wakatiwa ndani kwa uchunguzi. Polisi aliyefyatua risasi akathibitisha yeye alifyatua juu, hivyo risasi ile ikaenda juu, ikapinda kona, ikarudi chini, ikapinda tena kona kuingia kwenye daladala na kumuingia Akwilina, hivyo wao hawana kosa, serikali ikajiridhisha na kuwaachia, na badala yake ndio kikafanyika kilicho fanyika.

P
 
Wakuu Mbabe na Mindi, kwenye mauaji ya 6, kuna polisi 6 waliofyatua risasi, walishikwa wakatiwa ndani kwa uchunguzi. Polisi aliyefyatua risasi akathibitisha yeye alifyatua juu, hivyo risasi ile ikaenda juu, ikapinda kona, ikarudi chini, ikapinda tena kona kuingia kwenye daladala na kumuingia Akwilina, hivyo wao hawana kosa, serikali ikajiridhisha na kuwaachia, na badala yake ndio kikafanyika kilicho fanyika.

P
Hapa sasa nimekuelewa vizuri sana. Ahsante Mkuu Paskali vkwa ufafanuzi kuntu
 
Mayalla pole na hongera sana, umewezaje kuwa reqular contributor hapa Jamii Forum kwa kiwango hichi katika jumuia ambayo au hawana ufahamu wa kuchangia au maadili ya kuchangia yako chini sana au ufahamu wa somo na tukio uko chini mnoo.
Pamoja na hayo kuna kiwango kikubwa sana cha watu wanao jilazimisha kuonekana wajinga. Au tuseme ushabiki uliopindukia na hauwezi kupiwa kwa instrument yeyote.
Nimepita jeshini kwa mwaka mmoja, kuna suala la matumizi ya bunduki umeliibua la aina ya AK 47 katika kushambulia. This is very partinent questions you raised. Japo lazima uwe na kaba kwa kuelezea masuala ya majeshi kwa aifa lako, lakini nawaambia wanaousoma huu uzi kuwa na wanajeshi au waliopita jeshini watathibitisha Taifa la tanzania lina walenga shabaha majeshini ambao ukimpa risasi 100 kati ya risasi 95 mpaka 100 zina piga target. Kama ni pua pua tuu risasi zitarudia mara 95 mpaka 100. na tukio hilo linatokea ukiwa mita 50 mpaka100. Wapo wengi mno wakuujaza uwanja wa taifa muda wowote utakapo waita wapo.

Maswali ya aina ya bunduki na ushambuliaji uluofanywa unatoa lead ya kutosha sana what the investigators must focus on. Siwezi kuchangia zaidi lakini naamini kutakuwa na majibu. Pole sana, unabishana na wengi wasio jua na wenye kujua wanakalia ushabiki ambao unadhalilisha Jamii Forum,Hasa kwa wenye kujua Machine guns zinafanyaje kazi kuna ulazima na sio kubeza Dreva wa Lisu kusaidia upelelezi. Mayalla una ngozi ngumu , Asante.
Mchangia mada wewe siyo mtu makini na kwenye hili Jukwaa bakia unasoma tu. Serikali ilikuwa na uwezo wa kumfuata Dereva wa TL Nairobi hata Brussels kama Ingekuwa na nia ya kufanya uchunguzi. Nenda Dodoma kamuulize Kamanda Moroto kama kuna hata faili la uchunguzi limefunguliwa.

Wewe unaandika kwa kuwa tu una elimu ya ngumbaro (kusoma na kuandika), lakini kichwani hamna kitu.
 
Back
Top Bottom