Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Wanabodi

Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
"Shambulizi la Lissu, wanaomdhania dereva anahusika, sio wajinga!, wana hoja za msingi!" Swali ni Jee Dereva Anahusika?

Si maanishi kuwa dereva wa Lissu anahusika, bali mazingira ya tukio, yanahalalisha watu wenye udadisi kujiuliza maswali kihusu tukio lenyewe, hivyo kuhisi uhusika wa dereva wa Lissu, sio jambo la ajabu, tena uhusika wenyewe sio lazima uwe expressly but impliedly kwa negligence iliyopelekea Lissu kuwa reached na watu wasiojulikana na kushambuliwa, wakati alikuwa na uwezo wa kumuepusha na shambulizi hili.
Maswali haya ni kufuatia hoja za Lissu kwenye bandiko hili.
Wanabodi, maadam Tundu Lissu sasa karejea nchini na ameanza kufanya mahojiano mbalimbali, LIVE: Mahojiano na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu katika Clouds 360
Basi nami nitamtafuta na maswali haya yatapatiwa majibu
Asante Lissu kurejea, nitakutafuta ili ujibu maswali ya bandiko hili
P
 
Wanabodi, maadam Tundu Lissu sasa karejea nchini na ameanza kufanya mahojiano mbalimbali, LIVE: Mahojiano na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu katika Clouds 360
Basi nami nitamtafuta na maswali haya yatapatiwa majibu
Asante Lissu kurejea, nitakutafuta ili ujibu maswali ya bandiko hili
P
Fair enough Adv.Mayala, but anzia kwanza kwa RCO wa Dodoma, maana crime scene ipo chini yake, then utakapokutana na Mr.Lissu unakua na story za pande zote mbili, elewa every story ina two sides!,welldone na usiishie kwenye hii case ya Mr.Lissu pekee pia fanya uhabari wa kiuchunguzi kuhusu kupotea kwa Mr.Saanane, Je nini kilipelekea Akwilina kupigwa risasi kwenye ile protest, who fired the shot, why,je zile bunduki zilizokuwepo kwenye tukio zilifanyiwa ballistic test, pata report ya pathologist, je police walifungua docket ya kuchunguza ile issue, nipo tayari kuchangia gharama za data na usafiri kama utaamua kuifanya hii assignments good luck
 
Akina Afande goodluck (kwenye kesi ya mbowe) Sabaya ndio wasiojulikana.
Afande Goodluck anajulikana, aliwakamata makomandoo wa mbowe pale Rau Madukani wakinywa pombe na kuvuta bangi kupata nishai kumuua ole Sabaya, la sivyo ni kweli wangemuua. Lakini na wao wa genyongwa kwa ushahidi wa Afande Urio unaoitwa sting operation. Naye mbowe angenyongwa pia kwa ushahidi wa Lawyer wa tigopesa alipoitambua miamala ya malipo. Kama haya huyajui ni wewe peke yako wote wanajulikana.
 
Wanabodi

Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
"Shambulizi la Lissu, wanaomdhania dereva anahusika, sio wajinga!, wana hoja za msingi!" Swali ni Jee Dereva Anahusika?

Si maanishi kuwa dereva wa Lissu anahusika, bali mazingira ya tukio, yanahalalisha watu wenye udadisi kujiuliza maswali kihusu tukio lenyewe, hivyo kuhisi uhusika wa dereva wa Lissu, sio jambo la ajabu, tena uhusika wenyewe sio lazima uwe expressly but impliedly kwa negligence iliyopelekea Lissu kuwa reached na watu wasiojulikana na kushambuliwa, wakati alikuwa na uwezo wa kumuepusha na shambulizi hili.
Maswali haya ni kufuatia hoja za Lissu kwenye bandiko hili.
Mhe. Tundu Lissu,
Kwanza pole sana kwa yaliyokusibu.
Umezungumza mengi kuhusu kilichotokea mwaka mmoja uliopita, ila watu wanaohoji kuhusu dereva wako, nakuomba sana usiwaite wajinga, au wametumwa, kwa sababu mashaka yao ni very valid.

Kwa vile mashuhuda ni nyinyi wawili tuu, wewe na dereva wako, then kuna mambo tungependa kujua kutoka kwa Lissu mwemyewe na dereva wake.

Hoja kuwa tumetoka naye mbali hivyo tunaaminiana, hazina mashiko mbele ya watu na kazi zao. Lissu alipotoka na dereva wake, anaweza kujilinganisha Dr. Slaa na mlinzi wake Kagenzi walipotoka?, halafu what happened?!. Kwenye mambo ya assignment, anaweza hata akatumika mke wako aliyekuzalia wanao, sembuse itakuwa dereva tuu mliotoka nae mbali!.
Baadhi ya maswali ni haya...
  1. Kwa vile Lissu aliwahi kuripoti kufuatiliwa, kupitia press conference, kwa nini hakuripoti polisi?!.
  2. Baada ya Chadema kupokea taarifa ya Mnadhimu wake kufuatiliwa, walichukua hatua gani?.
  3. Baada kuona kuna gari linawafuatilia, mlichukua hatua gani?.
  4. The common sense ya kufuatiliwa inaelekeza, uki note you're followed, hatua ya kwanza ni kumpote anaye kufollow kwa makusudi, ili kwanza kujiridhisha kuwa anakufollow.
  5. Ukiisha jiridhisha you are followed, una change direction kumpoteza maboya.
  6. Ukimuona bado yupo, then kama uko fit, unamlengesha mahali kwenye kona ambapo hawezi kuchomoka, mnamalizana!.
  7. Kama hauko fit, unamlengesha kwenye safe area ,usually sehemu open kwenye makundi ya watu na kumripoti kunakohusika.
  8. Baada ya kuona mnafuatwa, kwa nini mliendelea kuelekea nyumbani?.
  9. Mlipofika mkasimama, mkawaona watu wawili wanashuka na AK 47, kitendo tuu cha kujua tuu bunduki zile ni AK 47, hii maana yake ni close proximity, kwenye shooting that close!, risasi 38!, dereva huyu amesalimikaje asipitiwe hata na moja?.
  10. (Mimi niliwahi kuwa mwanajeshi wa JWTZ hivyo kuna kitu nakijua kuhusu hizi AK47 ndani ya jeshi letu, lakini vitu vingine ni siri za usalama wa taifa letu, sina uhakika mtu asiyepitia JWTZ, ana uwezo gani kuijua AK 47!.)
  11. Ametokaje kwenye gari na kujificha chini ya gari ya jirani bila kugundulika?!.
  12. Anafichwa nini kuhojiwa?, kuna nini kinafichwa?.
  13. Maswali haya yameendelea kwa msaada wa mwana jf huyu
  14. Bunduki iliyotumika waliiona ni AK 47 iliyokuwa na full magazine (risasi 40) ambayo ilimimina risasi zote 40 at close range. Kati ya hizo 17 zilizama kwenye miguu, mikono na kiuno cha Tundu Lissu.
  15. Risasi zilimiminwa kutoka upande wa kulia wa gari ambao ni upande wa dreva lakini dreva hakupatwa na risasi hata moja na alipata hata fursa ya kuteremka kwenye gari na kwenda ku take cover kwenye magari yaliyokuwa yamepaki eneo hilo. Assailants walikuwa upande wa kulia wa gari, hivyo risasi zilizama zaidi kwenye mguu wa kulia, paja la kulia, mkono wa kulia, kiuno upande wa kulia na kutokea tumboni na mkono wa kushoto. These are the documented medical forensic clues.
  16. Majeshi yetu hayana bunduki za AK 47, yana SMG badala yake ambayzo full magazine zake ni risasi 30. Bunduki za AK47 zinamilikiwa na majambazi yanazozipata kutoka kwa wanajeshi wa Burundi wanaokimbilia Tanzania ambao huwa wanaziuza kwa bei ya shillingi 20,000 tu!! Silaha hizi ndizo zilitikisa huko Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
  17. Hakuna mwanajeshi ye yote (aliyepata mafunzo ya kijeshi) ambaye ampige mtu (adui) risasi 38 from an AK 47 gun at a close range halafu mtu huyo asalimike!! Never on earth. Kwanza atahitaji risasi moja tu na atafumua kichwa au moyo. Hivyo it is so obvious kwamba assailants wa Tundu Lissu walikuwa ni wahuni tu wa mitaani wasiojua kutumia bunduki. Yaani risasi 38 zote zinakosa target (kichwa au moyo) zinaishia kupiga makalio na hewa!! Hili halihitaji askari wa Scotland yard kulitambua. Swali ni nani aliwakodi hawa wahuni wasiojua shabaha? Kwa nini dreva wa Lissu akawa mkimbizi nchi za nje? Nini kakimbia? Kwani hata polisi wetu wakienda kumhoji huko kwani atasema lo lote la maana? Huko hawawezi kumu arrest. Alipaswa kuwa behind bars ili aeleze vizuri. Tundu Lissu alipaswa kujua hili. Mara nyingi kikulacho unacho nguoni mwako. Eti ninamuamini sana. Mbele ya pesa kunakuamini mtu? Yaani apewe shillingi million 500 aache kukumaliza? Yaani Tundu Lissu hajui kwamba "Money is the source of all evils in this world?"
  18. Hospitali ya serikali ya Dodoma na madaktari wa serikali wa Dodoma hospital ndiyo waliookoa maisha yake. Kama serikali ilikuwa na mpango wa kumuua, ingalishindwaje kumumalizia hapo hapo kwenye hospitali yake ya Dodoma humo humo operation theatre? It was so simple eg hiyo damu aliyopewa hangeipata au angalipewa incompatible blood ambayo ingalimumaliza hapo kwa hapo! Lazima aishukuru serikali kwa kuokoa maisha yake badala ya kuilaumu. Upinzani haupaswi kuwa wa aina hii. Tujifunze kwenye nchi zilizotutangulia.
  19. Bunduki kama AK 47 au SMG ikiunguruma si mchezo. Kwa askari yo yote trained, hata kama naye ana bunduki ya aina hiyo hiyo lakini kashutikizwa, reaction ya kwanza ni ku take cover. Atalala chini na ku craw hadi mahala salama. Hapo ndipo atatafuta kuona adui/ maadui walipo na kutafakari kama anao uwezo wa kupambana nao au kuomba reinfocement au kutokomea kabisa kwenye eneo hilo. Trained soldier hakurupuki tu kuanza kurusha risasi ovyo ovyo anapositukizwa na milio ya risasi. Hivyo kwa jinsi tukio lilivyotokea hapo usingalitarajia askari waliokuwa karibu na eneo hilo kuwa wangaliweza kuanza kujibu mapigo kwa muda huo mfupi uliotumika kabla ya majambazi hayo kutokomea kusikojulikana. Dreva wa Lissu aliyaona live na alitaja hata aina ya gari yalilotumia na plate namba zake. Polisi walikamata magari kadhaa ya aina hiyo lakini dreva huyo alikataa kwenda kuyatambua na hivyo yakabidi yaachiwe kwani hakuna shahidi aliyejitokeza. Shahidi muhimu alikuwa Nairobi akidaiwa anapata tiba ya kisaikolojia. Sasa hivi Lissu anasema dreva huyo yuko masomoni Ubeligiji. Sijui anasoma digrii gani hapo Leuven University teaching hospital anapotibiwa boss wake. Jamani aacheni kutufanya wajinga. Pascal yuko sahihi kabisa.
  20. Huko nyuma niliisha wahi kuzungumza haya kuhusu dereva wa Lissu.

Mpaka sasa the situation ya shambulio la Lissu as it is, limefanywa na watu wasiojulikana. Serikali yetu imeshindwa kuwabaini, lakini sisi watu wa media, tunaweza kusaidia kama nilivyosema hapa.
WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
Hitimisho.
The only defence ya Dereva wa Lissu has nothing to do na hiyo shooting, ni uzito tuu wa serikali yetu kufanya upelelezi wa tukio hili na kugoma kuita wachunguzi wa nje. Ingekuwa ni inside job ya Chadema, tungeshuhudia serikali fasta ingechunguza!.

Lakini kwa vile wasiojulikana ni hawa
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums

Tusitegemee lolote jipya hapa.
Tundu Lissu, just get well soon, na sasa inakubidi uchangue kati ya kuendelea na uanaharakati na kuishi kwa mashaka, au uamue kupunguza makali na kuishi kwa amani.

Pole Sana Mhe. Tundu Lissu, Get Well Soon.
P.
Rejea

  1. Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums
  2. Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?! - JamiiForums
  3. Tundu Lissu: Polisi wa Tanzania hawana mamlaka ya kunihoji nikiwa Kenya au kwingineko nje ya mipaka ya Tanzania - JamiiForums
  4. Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli! - JamiiForums
    TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe! - JamiiForums
  5. Bandiko la 5 Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?! - JamiiForums
  6. Bandiko la 6 Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums
  7. Bandiko la 7 https://www.jamiiforums.com/threads...je-tukahukumiwa-karma-ndio-pekee-hutoa-hukumu
  8. Bandiko la 8 Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums
  9. Bandiko la 9 Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija - JamiiForums
  10. Bandiko la 10 WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
  11. Bandiko la 11 Siku ya Sheria: No mention of Tundu Lissu!, Je ni amesahaulika tu kutajwa, amepuuzwa au ameepukwa?!. - JamiiForums
  12. Bandiko la 12 Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi! Je, anahusika? - JamiiForums
  13. Bandiko la 13 Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela! - JamiiForums
  14. Bandiko la 14 Je, Tundu Lissu anaichafua nchi yetu au anasema ukweli wa kilichomtokea? Je, Serikali yetu iwe Proactive kusema ukweli au Reactive kumjibu? - JamiiForums

Advocate Pascal Mayala
 
Hii nchi idadi ya wajinga inaongezeka kwa kasi kubwa sana. Kweli vyombo well trained kwa Kodi zetu wameshindwa kukamata waliompiga risasi Lisu? Instead narrative ya dereva kumpiga Lissu inakuwa celebrated? Narrative ya kushindwa kupeleleza sababu Lisu hayupo nchini inakuwa ndio Hoka? Hebu tuwe sober na tuwe more professional la sivyo tujihesabu hatuna weledi wa kazi zetu
 
Wanabodi, maadam Tundu Lissu sasa karejea nchini na ameanza kufanya mahojiano mbalimbali, LIVE: Mahojiano na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu katika Clouds 360
Basi nami nitamtafuta na maswali haya yatapatiwa majibu
Asante Lissu kurejea, nitakutafuta ili ujibu maswali ya bandiko hili
P
Lisu alianza kufuatwa na hawa watu tangu DSM na aliwai kuwashout kwa kumfuata fuata ,pia Tundu Lisu alifahamishwa mapema na Gwajima kuwa usiende Dodoma kama nilivyomnukuu Lema ,kwa hiyo swala la kufuatwa fuatwa nyuma halikuwa jambo geni kwake na vyombo vyote vya ulinzi na usalama vilikuwa vinafahamu jambo la Lisu kufuatwa na watu wasiyo julikana, lakini wakasema awafanyii kazi maswala ya mtandaoni ingawa kila siku tunnaona watu wanafungwa kwa mambo ya mtandaoni itoshe tu kusema yote ni mapenzi ya Mungu ata Yuda kumuuza Yesu kwa vipande Thelathini haikuwa akili yake.
 
Hii nchi idadi ya wajinga inaongezeka kwa kasi kubwa sana. Kweli vyombo well trained kwa Kodi zetu wameshindwa kukamata waliompiga risasi Lisu? Instead narrative ya dereva kumpiga Lissu inakuwa celebrated? Narrative ya kushindwa kupeleleza sababu Lisu hayupo nchini inakuwa ndio Hoka? Hebu tuwe sober na tuwe more professional la sivyo tujihesabu hatuna weledi wa kazi zetu
Katika majeshi bora ya POLISI duniani jeshi letu linashika namba tano kwa uwezo wa hali ya juu wakuchunguza na kuwabaini wahalifu.Itoshe tu kusema yote kwa yote kuna mambo mengine si yakumlaumu mtu ila ni yakukaa kimya tu.
 
Ni katika shambulio la TL

Huyu mtu akibanwa vizuri ataweza maliza maswali mengi sana .
 
Ni katika shambulio la TL

Huyu mtu akibanwa vizuri ataweza maliza maswali mengi sana .
Kwahiyo dereva ndio aliondoa CCTV na askari wanaolinda? Lissu alishasema Nissan patrol inamfuatilia na plate number alizitaja, badala ya kuikamata mko busy na dereva as if ndio ana mamlaka ya kuondoa walinzi!
 
Back
Top Bottom