Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Kwahiyo dereva ndio aliondoa CCTV na askari wanaolinda? Lissu alishasema Nissan patrol inamfuatilia na plate number alizitaja, badala ya kuikamata mko busy na dereva as if ndio ana mamlaka ya kuondoa walinzi!
Katika mission iliyochezwa kizembe na kufeli kibudu ni hii ya Assassination ya Lisu.

Suala la wao kutoa SISITIVI ili wahusika wasijulikane ni aibu kubwa kwao
 
Huyu mtu jamaa aliwahi kusoma na Lisu shule moja! Lakini ana chuki na Lisu ya hali ya juu sana! Nadhani siku akisikia Lisu hayupo tena duniani, atafurahi sana! Sasa kwa elimu yako ya uwanahabari ngumi, kwanini hautaki kujiuliza tu, nani aliondoa walizi wa serikali wa getini?, Nani kalificha picha cha CCTV? Kwanini bunge lilizuia stahiki zake za matibabu?

Badala yake unatulazimisha tufikirie vitu vya kijinga kijinga? Kwanini serikali haichunguZi? Serikali yenyewe ipo kimya, wewe ndio unahangaika na maelezo yako marefu yasiyo na maana!
 
Wanabodi

Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
"Shambulizi la Lissu, wanaomdhania dereva anahusika, sio wajinga!, wana hoja za msingi!" Swali ni Jee Dereva Anahusika?

ums
1. Hata wanaomdhania kuwa Magufuli akimtumia Paul Makonda anahusika, sio wajinga bali wanaoelewa na wanaona.!

2. Lakini pia wanaodhania kuwa dereva hahusiki kwa 100% sio wajinga, wanaelewa kuwa hahusiki !

3. Lakini kikubwa zaidi ni kuwa, wanaodhania kuwa dereva huyu ndiye "kihitimisho"cha mkakati mzima wa shambulio hilo dhidi ya Tundu Lissu Ili kuficha aibu ya serikali kwenye ishu hii, sio wajinga na uwe unaelewa Pascal Mayalla!

4. Lakini pia, na hii ikiwa ni jumuisho la majibu ya maswali yako yote uliyojiuliza kwenye bandiko lako refu ni kuwa, CHADEMA kamwe sio wajinga wala wapumbavu kumshauri dereva Adamu akae huko nje kwa usalama wake Ili muda mwafaka ukifika aje hapa nchini.

5. Na mwisho kabisa, mtuhumiwa namba Moja (serikali) kupitia jeshi la polisi wala sio wajinga wala wapumbavu kudhania kuwa hawawezi kumfuata dereva Adamu hukohuko aliko Ili kuchukua maelezo yake kutumika kama ushahidi wa kesi watakayoi - establish kwa sababu wanajua taratibu na hatua zote za sheria kupata ushahidi wa kijinai wa mtu aliyeko nchi nyingine.

Tatizo lao ni moja. THEY WANT ADAM DEAD before anything else. Kwanini? Usijifanye hujui, wewe unajua nini?
 
Kwahiyo dereva ndio aliondoa CCTV na askari wanaolinda? Lissu alishasema Nissan patrol inamfuatilia na plate number alizitaja, badala ya kuikamata mko busy na dereva as if ndio ana mamlaka ya kuondoa walinzi!
Walioondoa camera hawajulikani,
waliopiga risasi hawajulikani,
wasiojulikana hawajulikani
ila dereva anajulikana hvy hii case ingeanza kwa dereva.

Sasa tuje kwenye kauli zenu Chadema, mnasema JPM ndie mhusika wa yote haya sawa, JPM ni mwaka wa tatu sasa ni mfu lakini bado hamna ushahidi kuhusu tukio la Lissu, wewe huoni hapo kuwa tatizo lipo kwenu nyie Chadema pamoja na huyo dereva.?
Huyo dereva anaogopa nn wakati ule utawala umeisha.? Sasa ndio ujue huyo dereva kuna mtu mwingine anayemuogopa na huyo mtu yupo chademani.

Watu wengi mpaka leo hawajawahi kumuelewa Yuda, kwanini alimuua Yesu. Watu wanadhani Yuda alikuwa na shida ya vipande 30 vya fedha,La hasha hasha Yuda hakua na njaa hiyo hata kidogo. Yuda alikuwa na mipango mingine kabisa zaidi ya vipande Thelathini vya fedha.
Mipango mingine ilikuwa ni yapi.?

Ni katika shambulio la TL

Huyu mtu akibanwa vizuri ataweza maliza maswali mengi sana .
Anasubiri mpaka mbowe atoke kwenye kiti mana ndie anayemuogopa mana ndie alikuwa mchonga ramani wa tukio
 
Walioondoa camera hawajulikani,
waliopiga risasi hawajulikani,
wasiojulikana hawajulikani
ila dereva anajulikana hvy hii case ingeanza kwa dereva.

Sasa tuje kwenye kauli zenu Chadema, mnasema JPM ndie mhusika wa yote haya sawa, JPM ni mwaka wa tatu sasa ni mfu lakini bado hamna ushahidi kuhusu tukio la Lissu, wewe huoni hapo kuwa tatizo lipo kwenu nyie Chadema pamoja na huyo dereva.?
Huyo dereva anaogopa nn wakati ule utawala umeisha.? Sasa ndio ujue huyo dereva kuna mtu mwingine anayemuogopa na huyo mtu yupo chademani.

Mipango mingine ilikuwa ni yapi.?

Anasubiri mpaka mbowe atoke kwenye kiti mana ndie anayemuogopa mana ndie alikuwa mchonga ramani wa tukio

..Na nini kiliwazuia Magufuli, na Sirro, kumkamata, na kumshitaki, Mbowe, kama kweli amehusika?
 
Wanabodi

Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
"Shambulizi la Lissu, wanaomdhania dereva anahusika, sio wajinga!, wana hoja za msingi!" Swali ni Jee Dereva Anahusika?
Shambulio la Lisu si ulishasemaga ni dereva wake? Huo ndio uchunguzi wa kiuandishi unaousema? Au ilikuwa ni chuki binafsi na Lisu ambaye unasema uliwahi kusoma KTM shule moja ingawa madarasa tofauti?
Hili ni bandiko la swali na sio la statement!。
P
 
Wanabodi

Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
"Shambulizi la Lissu, wanaomdhania dereva anahusika, sio wajinga!, wana hoja za msingi!" Swali ni Jee Dereva Anahusika?

Si maanishi kuwa dereva wa Lissu anahusika, bali mazingira ya tukio, yanahalalisha watu wenye udadisi kujiuliza maswali kihusu tukio lenyewe, hivyo kuhisi uhusika wa dereva wa Lissu, sio jambo la ajabu, tena uhusika wenyewe sio lazima uwe expressly but impliedly kwa negligence iliyopelekea Lissu kuwa reached na watu wasiojulikana na kushambuliwa, wakati alikuwa na uwezo wa kumuepusha na shambulizi hili.
Maswali haya ni kufuatia hoja za Lissu kwenye bandiko hili.
Mhe. Tundu Lissu,
Kwanza pole sana kwa yaliyokusibu.
Umezungumza mengi kuhusu kilichotokea mwaka mmoja uliopita, ila watu wanaohoji kuhusu dereva wako, nakuomba sana usiwaite wajinga, au wametumwa, kwa sababu mashaka yao ni very valid.

Kwa vile mashuhuda ni nyinyi wawili tuu, wewe na dereva wako, then kuna mambo tungependa kujua kutoka kwa Lissu mwemyewe na dereva wake.

Hoja kuwa tumetoka naye mbali hivyo tunaaminiana, hazina mashiko mbele ya watu na kazi zao. Lissu alipotoka na dereva wake, anaweza kujilinganisha Dr. Slaa na mlinzi wake Kagenzi walipotoka?, halafu what happened?!. Kwenye mambo ya assignment, anaweza hata akatumika mke wako aliyekuzalia wanao, sembuse itakuwa dereva tuu mliotoka nae mbali!.
Baadhi ya maswali ni haya...
  1. Kwa vile Lissu aliwahi kuripoti kufuatiliwa, kupitia press conference, kwa nini hakuripoti polisi?!.
  2. Baada ya Chadema kupokea taarifa ya Mnadhimu wake kufuatiliwa, walichukua hatua gani?.
  3. Baada kuona kuna gari linawafuatilia, mlichukua hatua gani?.
  4. The common sense ya kufuatiliwa inaelekeza, uki note you're followed, hatua ya kwanza ni kumpote anaye kufollow kwa makusudi, ili kwanza kujiridhisha kuwa anakufollow.
  5. Ukiisha jiridhisha you are followed, una change direction kumpoteza maboya.
  6. Ukimuona bado yupo, then kama uko fit, unamlengesha mahali kwenye kona ambapo hawezi kuchomoka, mnamalizana!.
  7. Kama hauko fit, unamlengesha kwenye safe area ,usually sehemu open kwenye makundi ya watu na kumripoti kunakohusika.
  8. Baada ya kuona mnafuatwa, kwa nini mliendelea kuelekea nyumbani?.
  9. Mlipofika mkasimama, mkawaona watu wawili wanashuka na AK 47, kitendo tuu cha kujua tuu bunduki zile ni AK 47, hii maana yake ni close proximity, kwenye shooting that close!, risasi 38!, dereva huyu amesalimikaje asipitiwe hata na moja?.
  10. (Mimi niliwahi kuwa mwanajeshi wa JWTZ hivyo kuna kitu nakijua kuhusu hizi AK47 ndani ya jeshi letu, lakini vitu vingine ni siri za usalama wa taifa letu, sina uhakika mtu asiyepitia JWTZ, ana uwezo gani kuijua AK 47!.)
  11. Ametokaje kwenye gari na kujificha chini ya gari ya jirani bila kugundulika?!.
  12. Anafichwa nini kuhojiwa?, kuna nini kinafichwa?.
  13. Maswali haya yameendelea kwa msaada wa mwana jf huyu

  14. Bunduki iliyotumika waliiona ni AK 47 iliyokuwa na full magazine (risasi 40) ambayo ilimimina risasi zote 40 at close range. Kati ya hizo 17 zilizama kwenye miguu, mikono na kiuno cha Tundu Lissu.
  15. Risasi zilimiminwa kutoka upande wa kulia wa gari ambao ni upande wa dreva lakini dreva hakupatwa na risasi hata moja na alipata hata fursa ya kuteremka kwenye gari na kwenda ku take cover kwenye magari yaliyokuwa yamepaki eneo hilo. Assailants walikuwa upande wa kulia wa gari, hivyo risasi zilizama zaidi kwenye mguu wa kulia, paja la kulia, mkono wa kulia, kiuno upande wa kulia na kutokea tumboni na mkono wa kushoto. These are the documented medical forensic clues.
  16. Majeshi yetu hayana bunduki za AK 47, yana SMG badala yake ambayzo full magazine zake ni risasi 30. Bunduki za AK47 zinamilikiwa na majambazi yanazozipata kutoka kwa wanajeshi wa Burundi wanaokimbilia Tanzania ambao huwa wanaziuza kwa bei ya shillingi 20,000 tu!! Silaha hizi ndizo zilitikisa huko Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
  17. Hakuna mwanajeshi ye yote (aliyepata mafunzo ya kijeshi) ambaye ampige mtu (adui) risasi 38 from an AK 47 gun at a close range halafu mtu huyo asalimike!! Never on earth. Kwanza atahitaji risasi moja tu na atafumua kichwa au moyo. Hivyo it is so obvious kwamba assailants wa Tundu Lissu walikuwa ni wahuni tu wa mitaani wasiojua kutumia bunduki. Yaani risasi 38 zote zinakosa target (kichwa au moyo) zinaishia kupiga makalio na hewa!! Hili halihitaji askari wa Scotland yard kulitambua. Swali ni nani aliwakodi hawa wahuni wasiojua shabaha? Kwa nini dreva wa Lissu akawa mkimbizi nchi za nje? Nini kakimbia? Kwani hata polisi wetu wakienda kumhoji huko kwani atasema lo lote la maana? Huko hawawezi kumu arrest. Alipaswa kuwa behind bars ili aeleze vizuri. Tundu Lissu alipaswa kujua hili. Mara nyingi kikulacho unacho nguoni mwako. Eti ninamuamini sana. Mbele ya pesa kunakuamini mtu? Yaani apewe shillingi million 500 aache kukumaliza? Yaani Tundu Lissu hajui kwamba "Money is the source of all evils in this world?"
  18. Hospitali ya serikali ya Dodoma na madaktari wa serikali wa Dodoma hospital ndiyo waliookoa maisha yake. Kama serikali ilikuwa na mpango wa kumuua, ingalishindwaje kumumalizia hapo hapo kwenye hospitali yake ya Dodoma humo humo operation theatre? It was so simple eg hiyo damu aliyopewa hangeipata au angalipewa incompatible blood ambayo ingalimumaliza hapo kwa hapo! Lazima aishukuru serikali kwa kuokoa maisha yake badala ya kuilaumu. Upinzani haupaswi kuwa wa aina hii. Tujifunze kwenye nchi zilizotutangulia.
  19. Bunduki kama AK 47 au SMG ikiunguruma si mchezo. Kwa askari yo yote trained, hata kama naye ana bunduki ya aina hiyo hiyo lakini kashutikizwa, reaction ya kwanza ni ku take cover. Atalala chini na ku craw hadi mahala salama. Hapo ndipo atatafuta kuona adui/ maadui walipo na kutafakari kama anao uwezo wa kupambana nao au kuomba reinfocement au kutokomea kabisa kwenye eneo hilo. Trained soldier hakurupuki tu kuanza kurusha risasi ovyo ovyo anapositukizwa na milio ya risasi. Hivyo kwa jinsi tukio lilivyotokea hapo usingalitarajia askari waliokuwa karibu na eneo hilo kuwa wangaliweza kuanza kujibu mapigo kwa muda huo mfupi uliotumika kabla ya majambazi hayo kutokomea kusikojulikana. Dreva wa Lissu aliyaona live na alitaja hata aina ya gari yalilotumia na plate namba zake. Polisi walikamata magari kadhaa ya aina hiyo lakini dreva huyo alikataa kwenda kuyatambua na hivyo yakabidi yaachiwe kwani hakuna shahidi aliyejitokeza. Shahidi muhimu alikuwa Nairobi akidaiwa anapata tiba ya kisaikolojia. Sasa hivi Lissu anasema dreva huyo yuko masomoni Ubeligiji. Sijui anasoma digrii gani hapo Leuven University teaching hospital anapotibiwa boss wake. Jamani aacheni kutufanya wajinga. Pascal yuko sahihi kabisa.
  20. Huko nyuma niliisha wahi kuzungumza haya kuhusu dereva wa Lissu.

Mpaka sasa the situation ya shambulio la Lissu as it is, limefanywa na watu wasiojulikana. Serikali yetu imeshindwa kuwabaini, lakini sisi watu wa media, tunaweza kusaidia kama nilivyosema hapa.
WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
Hitimisho.
The only defence ya Dereva wa Lissu has nothing to do na hiyo shooting, ni uzito tuu wa serikali yetu kufanya upelelezi wa tukio hili na kugoma kuita wachunguzi wa nje. Ingekuwa ni inside job ya Chadema, tungeshuhudia serikali fasta ingechunguza!.

Lakini kwa vile wasiojulikana ni hawa
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums

Tusitegemee lolote jipya hapa.
Tundu Lissu, just get well soon, na sasa inakubidi uchangue kati ya kuendelea na uanaharakati na kuishi kwa mashaka, au uamue kupunguza makali na kuishi kwa amani.

Pole Sana Mhe. Tundu Lissu, Get Well Soon.
P.
Rejea

  1. Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums
  2. Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?! - JamiiForums
  3. Tundu Lissu: Polisi wa Tanzania hawana mamlaka ya kunihoji nikiwa Kenya au kwingineko nje ya mipaka ya Tanzania - JamiiForums
  4. Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli! - JamiiForums
    TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe! - JamiiForums
  5. Bandiko la 5 Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?! - JamiiForums
  6. Bandiko la 6 Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums
  7. Bandiko la 7 https://www.jamiiforums.com/threads...je-tukahukumiwa-karma-ndio-pekee-hutoa-hukumu
  8. Bandiko la 8 Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums
  9. Bandiko la 9 Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija - JamiiForums
  10. Bandiko la 10 WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
  11. Bandiko la 11 Siku ya Sheria: No mention of Tundu Lissu!, Je ni amesahaulika tu kutajwa, amepuuzwa au ameepukwa?!. - JamiiForums
  12. Bandiko la 12 Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi! Je, anahusika? - JamiiForums
  13. Bandiko la 13 Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela! - JamiiForums
  14. Bandiko la 14 Je, Tundu Lissu anaichafua nchi yetu au anasema ukweli wa kilichomtokea? Je, Serikali yetu iwe Proactive kusema ukweli au Reactive kumjibu? - JamiiForums
Anaehisi dereva wa Lissu anahusika ni mpumbavu sana!
 
Walioondoa camera hawajulikani,
waliopiga risasi hawajulikani,
wasiojulikana hawajulikani
ila dereva anajulikana hvy hii case ingeanza kwa dereva.

Sasa tuje kwenye kauli zenu Chadema, mnasema JPM ndie mhusika wa yote haya sawa, JPM ni mwaka wa tatu sasa ni mfu lakini bado hamna ushahidi kuhusu tukio la Lissu, wewe huoni hapo kuwa tatizo lipo kwenu nyie Chadema pamoja na huyo dereva.?
Huyo dereva anaogopa nn wakati ule utawala umeisha.? Sasa ndio ujue huyo dereva kuna mtu mwingine anayemuogopa na huyo mtu yupo chademani.

Mipango mingine ilikuwa ni yapi.?

Anasubiri mpaka mbowe atoke kwenye kiti mana ndie anayemuogopa mana ndie alikuwa mchonga ramani wa tukio
Hawa walichukua kitendo cha dereva kupona na kusaidia kuokoa maisha ya boss wake hivyo wanatamani kumkamata na kunyesha ili kumaliza hasira yao!
Kwanini wadianze na walio ondoa Lindi, walielekezwa na nani?
Waliingia CCTV camera walitumwa na nani? Ni Chadema walifanya yote hayo?
 
Wanabodi

Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
"Shambulizi la Lissu, wanaomdhania dereva anahusika, sio wajinga!, wana hoja za msingi!" Swali ni Jee Dereva Anahusika?

Si maanishi kuwa dereva wa Lissu anahusika, bali mazingira ya tukio, yanahalalisha watu wenye udadisi kujiuliza maswali kihusu tukio lenyewe, hivyo kuhisi uhusika wa dereva wa Lissu, sio jambo la ajabu, tena uhusika wenyewe sio lazima uwe expressly but impliedly kwa negligence iliyopelekea Lissu kuwa reached na watu wasiojulikana na kushambuliwa, wakati alikuwa na uwezo wa kumuepusha na shambulizi hili.
Maswali haya ni kufuatia hoja za Lissu kwenye bandiko hili.
Mhe. Tundu Lissu,
Kwanza pole sana kwa yaliyokusibu.
Umezungumza mengi kuhusu kilichotokea mwaka mmoja uliopita, ila watu wanaohoji kuhusu dereva wako, nakuomba sana usiwaite wajinga, au wametumwa, kwa sababu mashaka yao ni very valid.

Kwa vile mashuhuda ni nyinyi wawili tuu, wewe na dereva wako, then kuna mambo tungependa kujua kutoka kwa Lissu mwemyewe na dereva wake.

Hoja kuwa tumetoka naye mbali hivyo tunaaminiana, hazina mashiko mbele ya watu na kazi zao. Lissu alipotoka na dereva wake, anaweza kujilinganisha Dr. Slaa na mlinzi wake Kagenzi walipotoka?, halafu what happened?!. Kwenye mambo ya assignment, anaweza hata akatumika mke wako aliyekuzalia wanao, sembuse itakuwa dereva tuu mliotoka nae mbali!.

View: https://youtu.be/Yo4zV7MKv1U?si=XKFRTGRYCDNDzzGZ
Nimemsikiliza huyu jamaa, kiukweli uchawa ukizidi sana, mtu unakuwa kama taahira fulani1. Nao puuzeni hoja zake za uchawa, ila msikilize anapomzungumzia dereva wa Lissu, ulinganishe na nilichouliza kwenye bandiko hili.
P
 
..wamechomoa na memory ya camera zilizokuwa kwenye gari ya Lissu!!
Sijui kuhusu camera za Toyota, camera za Range Rover latest models ni ip cameras, storage ni kwenye clouds, na hata ukiiba ni kazi bure,tracker zao zinatumia live satelite view wanaiona gari ilipo with 360 degrees, wanawaona walio ndani, but you can disable inside cameras for privacy but you can't disable tracking!.
P
 
Back
Top Bottom