Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Sijui kuhusu camera za Toyota, camera za Range Rover latest models ni ip cameras, storage ni kwenye clouds, na hata ukiiba ni kazi bure,tracker zao zinatumia live satelite view wanaiona gari ilipo with 360 degrees, wanawaona walio ndani, but you can disable inside cameras for privacy but you can't disable tracking!.
P
Pascal unafikiri kwanini hasa polisi hili suala waliachana nalo mapema mno na hata hawataki kulizungumzia

Lissu ametumia miaka mingapi kupewa lile gari kutoka kituoni?

Unafikiri tuhuma za Tigo ni "fabricated"?

Dereva alihojiwa na DW akiwa Ubelgiji na alieleza kwa kina kilichotokea kwa shambulizi lile dereva lazima alipitia PTSD na sehemu pekee ambayo angekuwa sawa na walau kupata ahueni ni nje ya Tanzania.

Polisi wa Tanzania kama kweli walikuwa na nia ya kuandika maelezo yake wangeshirikiana na Interpol akiwa huko huko na sio kurudi Tanzania maana usalama wake ungekuwa mdogo sana.


View: https://youtu.be/6Ysrl-iFNJM?si=rHb478ZhBO6NAQjF
 
Sijui kuhusu camera za Toyota, camera za Range Rover latest models ni ip cameras, storage ni kwenye clouds, na hata ukiiba ni kazi bure,tracker zao zinatumia live satelite view wanaiona gari ilipo with 360 degrees, wanawaona walio ndani, but you can disable inside cameras for privacy but you can't disable tracking!.
P

..hili tukio kukiwa na nia ya dhati sio kazi kubwa kuujua ukweli, na kuwanasa waliohusika.
 
..hili tukio kukiwa na nia ya dhati sio kazi kubwa kuujua ukweli, na kuwanasa waliohusika.
Ukweli wanajua ila haiwezekani jambazi achunguze masuala ya ujambazi.

Samia tangu apige askari ambao ndio hao hao watekaji na wauaji wa mzee Kibao leo ni siku ya 36 tangu kaomba ripoti na kuko kimya.

Yaani watu wafunge barabara mchana kweupe na wamchukue mtu ndani ya gari na kutokomea nae kusikojulikana na tuambiwe eti ni raia tu wa kawaida?

Deusdedith Soka alipigiwa simu na askari hao hao aelekee kituoni leo ni siku ya 58 hajulikani alipo.

Nani mjinga hapo ataendelea kudanganywa kuhusu wahusika wa hayo matukio?
 
Pascal unafikiri kwanini hasa polisi hili suala waliachana nalo mapema mno na hata hawataki kulizungumzia

Lissu ametumia miaka mingapi kupewa lile gari kutoka kituoni?

Unafikiri tuhuma za Tigo ni "fabricated"?

Dereva alihojiwa na DW akiwa Ubelgiji na alieleza kwa kina kilichotokea kwa shambulizi lile dereva lazima alipitia PTSD na sehemu pekee ambayo angekuwa sawa na walau kupata ahueni ni nje ya Tanzania.

Polisi wa Tanzania kama kweli walikuwa na nia ya kuandika maelezo yake wangeshirikiana na Interpol akiwa huko huko na sio kurudi Tanzania maana usalama wake ungekuwa mdogo sana.


View: https://youtu.be/6Ysrl-iFNJM?si=rHb478ZhBO6NAQjF

Thanks for this, Tanzania hatuhitaji kibali kumhoji Mtanzania yoyote popote just notification. Tanzania na Kenya tuna extradition treaty hivyo polisi wetu wangekuwa wana nia kumhoji, wangemhoji akiwa jijini Nairobi. Tanzania na Belgium hatuna extradition treaty, hivyo mhalifu wa Belgium Tanzania ni safe heaven, na mhalifu wa Tanzania, Belgium ni safe heaven.

Issue ya dereva wa Lissu sio issue ya interpol na dereva huyo sio mhalifu, hivyo interpol has nothing to do with this.
P
 
Ni kweli, hata sisi waandishi wa IJ, hili tunaliweza liko ndani ya uwezo wetu
P
Mimi nilifutilia kwa kutumia codes zangu nikajipa moyo kunasiku litambumbuluka tena hao ambao hawatakiwi wajulikane ipo siku watajulikana tu, (it is never too late in life) niliongeza codes nyingine baada ya kumsikiliza dereva akihojiwa DW
 
Ukweli wanajua ila haiwezekani jambazi achunguze masuala ya ujambazi.

Samia tangu apige askari ambao ndio hao hao watekaji na wauaji wa mzee Kibao leo ni siku ya 36 tangu kaomba ripoti na kuko kimya.

Yaani watu wafunge barabara mchana kweupe na wamchukue mtu ndani ya gari na kutokomea nae kusikojulikana na tuambiwe eti ni raia tu wa kawaida?

Deusdedith Soka alipigiwa simu na askari hao hao aelekee kituoni leo ni siku ya 58 hajulikani alipo.

Nani mjinga hapo ataendelea kudanganywa kuhusu wahusika wa hayo matukio?
Kama ni kushauri tumemshauri sana tuu kwa mtu wetu, awatose tuu hawa jamaa, na tukaeleza kuwa mchelea mwana kulia, hulia yeye! Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe
P
 
Kama ni kushauri tumemshauri sana tuu kwa mtu wetu, awatose tuu hawa jamaa, na tukaeleza kuwa mchelea mwana kulia, hulia yeye!.
P
Una nikumbusha wimbo wa MR Blue wa mapozi nami mapozi nawee, kwakifupi ni wapumbavu hata tukio liliratibiwa na wapumbavu.

The evils, (wicked), left with a lot of question marks ???????????? Without closing the marks
 
Mimi nilifutilia kwa kutumia codes zangu nikajipa moyo kunasiku litambumbuluka tena hao ambao hawatakiwi wajulikane ipo siku watajulikana tu, (it is never too late in life) niliongeza codes nyingine baada ya kumsikiliza dereva akihojiwa DW

..kwanini Wamarekani walimuweka Makonda ktk listi ya watu wasiotakiwa nchini kwao? Wanamtuhumu Makonda kwa kosa gani? Pia tukio hili halichunguzwi kwa maslahi ya nani?
 
..kwanini Wamarekani walimuweka Makonda ktk listi ya watu wasiotakiwa nchini kwao? Wanamtuhumu Makonda kwa kosa gani? Pia tukio hili halichunguzwi kwa maslahi ya nani?
Hilo swali la kutuhumiwa kwa makonda linaweza jibiwa vizuri na walio mtuhumu lakini kwa faida yako unaweza soma kuhusu the use of orbiting satellites, (artificial satellites)

Halichunguzwi kwa masilahi ya waliokuwa, (wame ratibu), ondoa na kupanga zamu za walinzi, walinzi ambao, (walikuwa hawatumii bunduki),hawana bunduki na wale wenye bunduki wa area D, pia kwa masililahi ya wale walioziondoa CCTV, zilizokuwa zimefungwa karibu na nyumba ya mh. Tundulisu aliekuwa amemiminiwa risasi zote zille, akiwa ndani ya gari lake, pale pale karibu na CCTV

Similarly to, (vile vile), tume huundwa nyuma ya mikamera, majibu ya tume nyuma ya pazia
 
Wanabodi

Hili ni bandiko la maswali kwa Tundu Lissu na dereva wake, kufuatia shambulio la Lissu,
"Shambulizi la Lissu, wanaomdhania dereva anahusika, sio wajinga!, wana hoja za msingi!" Swali ni Jee Dereva Anahusika?

Si maanishi kuwa dereva wa Lissu anahusika, bali mazingira ya tukio, yanahalalisha watu wenye udadisi kujiuliza maswali kihusu tukio lenyewe, hivyo kuhisi uhusika wa dereva wa Lissu, sio jambo la ajabu, tena uhusika wenyewe sio lazima uwe expressly but impliedly kwa negligence iliyopelekea Lissu kuwa reached na watu wasiojulikana na kushambuliwa, wakati alikuwa na uwezo wa kumuepusha na shambulizi hili.
Maswali haya ni kufuatia hoja za Lissu kwenye bandiko hili.
Mhe. Tundu Lissu,
Kwanza pole sana kwa yaliyokusibu.
Umezungumza mengi kuhusu kilichotokea mwaka mmoja uliopita, ila watu wanaohoji kuhusu dereva wako, nakuomba sana usiwaite wajinga, au wametumwa, kwa sababu mashaka yao ni very valid.

Kwa vile mashuhuda ni nyinyi wawili tuu, wewe na dereva wako, then kuna mambo tungependa kujua kutoka kwa Lissu mwemyewe na dereva wake.

Hoja kuwa tumetoka naye mbali hivyo tunaaminiana, hazina mashiko mbele ya watu na kazi zao. Lissu alipotoka na dereva wake, anaweza kujilinganisha Dr. Slaa na mlinzi wake Kagenzi walipotoka?, halafu what happened?!. Kwenye mambo ya assignment, anaweza hata akatumika mke wako aliyekuzalia wanao, sembuse itakuwa dereva tuu mliotoka nae mbali!.
Baadhi ya maswali ni haya...
  1. Kwa vile Lissu aliwahi kuripoti kufuatiliwa, kupitia press conference, kwa nini hakuripoti polisi?!.
  2. Baada ya Chadema kupokea taarifa ya Mnadhimu wake kufuatiliwa, walichukua hatua gani?.
  3. Baada kuona kuna gari linawafuatilia, mlichukua hatua gani?.
  4. The common sense ya kufuatiliwa inaelekeza, uki note you're followed, hatua ya kwanza ni kumpote anaye kufollow kwa makusudi, ili kwanza kujiridhisha kuwa anakufollow.
  5. Ukiisha jiridhisha you are followed, una change direction kumpoteza maboya.
  6. Ukimuona bado yupo, then kama uko fit, unamlengesha mahali kwenye kona ambapo hawezi kuchomoka, mnamalizana!.
  7. Kama hauko fit, unamlengesha kwenye safe area ,usually sehemu open kwenye makundi ya watu na kumripoti kunakohusika.
  8. Baada ya kuona mnafuatwa, kwa nini mliendelea kuelekea nyumbani?.
  9. Mlipofika mkasimama, mkawaona watu wawili wanashuka na AK 47, kitendo tuu cha kujua tuu bunduki zile ni AK 47, hii maana yake ni close proximity, kwenye shooting that close!, risasi 38!, dereva huyu amesalimikaje asipitiwe hata na moja?.
  10. (Mimi niliwahi kuwa mwanajeshi wa JWTZ hivyo kuna kitu nakijua kuhusu hizi AK47 ndani ya jeshi letu, lakini vitu vingine ni siri za usalama wa taifa letu, sina uhakika mtu asiyepitia JWTZ, ana uwezo gani kuijua AK 47!.)
  11. Ametokaje kwenye gari na kujificha chini ya gari ya jirani bila kugundulika?!.
  12. Anafichwa nini kuhojiwa?, kuna nini kinafichwa?.
  13. Maswali haya yameendelea kwa msaada wa mwana jf huyu

  14. Bunduki iliyotumika waliiona ni AK 47 iliyokuwa na full magazine (risasi 40) ambayo ilimimina risasi zote 40 at close range. Kati ya hizo 17 zilizama kwenye miguu, mikono na kiuno cha Tundu Lissu.
  15. Risasi zilimiminwa kutoka upande wa kulia wa gari ambao ni upande wa dreva lakini dreva hakupatwa na risasi hata moja na alipata hata fursa ya kuteremka kwenye gari na kwenda ku take cover kwenye magari yaliyokuwa yamepaki eneo hilo. Assailants walikuwa upande wa kulia wa gari, hivyo risasi zilizama zaidi kwenye mguu wa kulia, paja la kulia, mkono wa kulia, kiuno upande wa kulia na kutokea tumboni na mkono wa kushoto. These are the documented medical forensic clues.
  16. Majeshi yetu hayana bunduki za AK 47, yana SMG badala yake ambayzo full magazine zake ni risasi 30. Bunduki za AK47 zinamilikiwa na majambazi yanazozipata kutoka kwa wanajeshi wa Burundi wanaokimbilia Tanzania ambao huwa wanaziuza kwa bei ya shillingi 20,000 tu!! Silaha hizi ndizo zilitikisa huko Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
  17. Hakuna mwanajeshi ye yote (aliyepata mafunzo ya kijeshi) ambaye ampige mtu (adui) risasi 38 from an AK 47 gun at a close range halafu mtu huyo asalimike!! Never on earth. Kwanza atahitaji risasi moja tu na atafumua kichwa au moyo. Hivyo it is so obvious kwamba assailants wa Tundu Lissu walikuwa ni wahuni tu wa mitaani wasiojua kutumia bunduki. Yaani risasi 38 zote zinakosa target (kichwa au moyo) zinaishia kupiga makalio na hewa!! Hili halihitaji askari wa Scotland yard kulitambua. Swali ni nani aliwakodi hawa wahuni wasiojua shabaha? Kwa nini dreva wa Lissu akawa mkimbizi nchi za nje? Nini kakimbia? Kwani hata polisi wetu wakienda kumhoji huko kwani atasema lo lote la maana? Huko hawawezi kumu arrest. Alipaswa kuwa behind bars ili aeleze vizuri. Tundu Lissu alipaswa kujua hili. Mara nyingi kikulacho unacho nguoni mwako. Eti ninamuamini sana. Mbele ya pesa kunakuamini mtu? Yaani apewe shillingi million 500 aache kukumaliza? Yaani Tundu Lissu hajui kwamba "Money is the source of all evils in this world?"
  18. Hospitali ya serikali ya Dodoma na madaktari wa serikali wa Dodoma hospital ndiyo waliookoa maisha yake. Kama serikali ilikuwa na mpango wa kumuua, ingalishindwaje kumumalizia hapo hapo kwenye hospitali yake ya Dodoma humo humo operation theatre? It was so simple eg hiyo damu aliyopewa hangeipata au angalipewa incompatible blood ambayo ingalimumaliza hapo kwa hapo! Lazima aishukuru serikali kwa kuokoa maisha yake badala ya kuilaumu. Upinzani haupaswi kuwa wa aina hii. Tujifunze kwenye nchi zilizotutangulia.
  19. Bunduki kama AK 47 au SMG ikiunguruma si mchezo. Kwa askari yo yote trained, hata kama naye ana bunduki ya aina hiyo hiyo lakini kashutikizwa, reaction ya kwanza ni ku take cover. Atalala chini na ku craw hadi mahala salama. Hapo ndipo atatafuta kuona adui/ maadui walipo na kutafakari kama anao uwezo wa kupambana nao au kuomba reinfocement au kutokomea kabisa kwenye eneo hilo. Trained soldier hakurupuki tu kuanza kurusha risasi ovyo ovyo anapositukizwa na milio ya risasi. Hivyo kwa jinsi tukio lilivyotokea hapo usingalitarajia askari waliokuwa karibu na eneo hilo kuwa wangaliweza kuanza kujibu mapigo kwa muda huo mfupi uliotumika kabla ya majambazi hayo kutokomea kusikojulikana. Dreva wa Lissu aliyaona live na alitaja hata aina ya gari yalilotumia na plate namba zake. Polisi walikamata magari kadhaa ya aina hiyo lakini dreva huyo alikataa kwenda kuyatambua na hivyo yakabidi yaachiwe kwani hakuna shahidi aliyejitokeza. Shahidi muhimu alikuwa Nairobi akidaiwa anapata tiba ya kisaikolojia. Sasa hivi Lissu anasema dreva huyo yuko masomoni Ubeligiji. Sijui anasoma digrii gani hapo Leuven University teaching hospital anapotibiwa boss wake. Jamani aacheni kutufanya wajinga. Pascal yuko sahihi kabisa.
  20. Huko nyuma niliisha wahi kuzungumza haya kuhusu dereva wa Lissu.

Mpaka sasa the situation ya shambulio la Lissu as it is, limefanywa na watu wasiojulikana. Serikali yetu imeshindwa kuwabaini, lakini sisi watu wa media, tunaweza kusaidia kama nilivyosema hapa.
WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
Hitimisho.
The only defence ya Dereva wa Lissu has nothing to do na hiyo shooting, ni uzito tuu wa serikali yetu kufanya upelelezi wa tukio hili na kugoma kuita wachunguzi wa nje. Ingekuwa ni inside job ya Chadema, tungeshuhudia serikali fasta ingechunguza!.

Lakini kwa vile wasiojulikana ni hawa
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums

Tusitegemee lolote jipya hapa.
Tundu Lissu, just get well soon, na sasa inakubidi uchangue kati ya kuendelea na uanaharakati na kuishi kwa mashaka, au uamue kupunguza makali na kuishi kwa amani.

Pole Sana Mhe. Tundu Lissu, Get Well Soon.
P.
Rejea

  1. Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums
  2. Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?! - JamiiForums
  3. Tundu Lissu: Polisi wa Tanzania hawana mamlaka ya kunihoji nikiwa Kenya au kwingineko nje ya mipaka ya Tanzania - JamiiForums
  4. Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli! - JamiiForums
    TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe! - JamiiForums
  5. Bandiko la 5 Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?! - JamiiForums
  6. Bandiko la 6 Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums
  7. Bandiko la 7 https://www.jamiiforums.com/threads...je-tukahukumiwa-karma-ndio-pekee-hutoa-hukumu
  8. Bandiko la 8 Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums
  9. Bandiko la 9 Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija - JamiiForums
  10. Bandiko la 10 WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
  11. Bandiko la 11 Siku ya Sheria: No mention of Tundu Lissu!, Je ni amesahaulika tu kutajwa, amepuuzwa au ameepukwa?!. - JamiiForums
  12. Bandiko la 12 Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi! Je, anahusika? - JamiiForums
  13. Bandiko la 13 Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela! - JamiiForums
  14. Bandiko la 14 Je, Tundu Lissu anaichafua nchi yetu au anasema ukweli wa kilichomtokea? Je, Serikali yetu iwe Proactive kusema ukweli au Reactive kumjibu? - JamiiForums
Interesting…
 
Upuuzi mtupu ,mbona uchunguzi haukufanywa ,acheni mtoto wa watu ,Mungu alimepusha basi,Mbona wahusika munawajua ?bas useme ni ww ivo unaweweseka na bado utasema mengi

Tigo munahusika mumekimbila kubadili jina eti bayasi ? Jamani@ ilimukwepe kesi sasa wazungu wana akili sana suɓiri muda tu utasema
 
Si mlishaambiwa Tigo walitoa code zote ili mwamba apotezwe,vipi na zile Camera za usalama kwenye yale makazi ya wagonga meza nani aliziondoa.

Yote kwa yote Mungu ni Mwema Mwamba anapumua mpaka sasa.
 
Back
Top Bottom