Shareholder mkubwa wa NMB ameondoka – Rabobank Nederland

Nahisi kitu kama hicho ukiangalia yule CEO wao mzungu mmama naskia kuna fitna fulani ilifanywa.
Punguzu negative outlook ya all commercial or economic decisions made by either Government or Parastatals.

Katika maisha ukiangalia chini tuu, utafikiria kuchimba na kwenda chini mnoo bila kuona kizuri .
Na ukifikiri na kuona mamba with pessimistic mind itakusaidia kuona ya juu na mema, na pia mabaya ya chini in the same vain.
 
It's sad now days kila kitu kinajadiliwa kisiasa, kihisia na mihemko bila kuchimba kutafta ukweli wa habari husika...very few people wame dig kupata ukweli wa habari husika the rest ni mapovu tu. Hata mleta mada kaleta habari nusu nusu ili mradi tu ku provoke watu wanaopenda kudandia treni kwa mbele wadandie vzuri.

Hii tarifa ni public notice, na ipo kwenye website ya nmb wenyewe Rabobank has lodged a share transfer request for its stake in NMB Bank Plc - NMB Bank Plc.

kuna share transfer itafanyika due to a emerger btn Robobank, Dutch development bank na Norwegian state owned development fund, and for now wame lodge their request kwa mamlaka husika for the approval.

Heb tujifunze ku dig taarifa ili angalau tuwe na wider understanding ya topic husika kabla hatujaanza kuchangia kwa mihemko.
 
Serikali inaweza kuwa inataka kuzirejesha benki zake, NMB+NBC, makaburu bado wanaweza kufungua benki yao na kujenga mtando kadri wanavyotaka, siyo kujimwambafy kwenye benki ambayo ilikuwa imeshaanzishwa na serikali.
Hali halipo kabisa katika será za uchumi na fedha wa Tanzania 2015 to 2050.

Ila kutakuwa na Benki zitakazo pewa capital injection ili zifanye shughuli za Marchantile Banking, Construction Banking na Industrial Development Banking. Kuna muono hasi ambao haupo kiuchumi kabisa.

Kwa muda mrefu Watanzania tumekuwa na makundi mawili makubwa katika biashara na wote tunaowaita wafanya biashara kimakosa.
WACHUUZI AMBALO NI 91% NA WAFANYABIASHARA AMBAO NI 9%.

Small retailer and distributors VS Business people/ Investors and Industrialist.

Hii topic inataka muda wa kutosha na ijitegemee.
 
Shukran sana Mkuu. kwa sababu me siyo mtaalamu wa haya mambo, eti nilidhani capital leakage ni pale ambapo bank yenyewe imeamua kuzinunua hizo hisa kwa kuwalipa Rabobank hayo madolars halafu izitafutie mwekezaji mwingine ? Lakini ikiwa zimenunuliwa na investor mwingine na Rabobank akavuta huo mpunga si fresh tu kwamba Mtaji wa NMB haujatikiswa? (Hapo zaidi zaidi ni maswala ya forex ndiyo yaliyoathirika kwamba kutatakiwa kuwe na midolars ya kuwalipa hao wadachi kutoka Tz.Ila kama aliyenunua ni mgeni (foreigner) hapo hakuna effect at all. Issue inayobaki ni kama aliyenunua ni serikali,na akawa ndiyo majority shareholder,kwamba serikali itakuwa inafanya biashara ya bank,kitu ambacho wengi humu wanaonekana kutokiafiki.

Labda wenye taarifa watusaidie

Nani amenunua hizo hisa za dolars milion183 Kutoka Rabobank?
 
Walicho fanya hawa Rabo bank ni kupunguza share za umiliki kutoka 35% mpaka 25% kwa kuanzishwa kampuni mpya iitwayo Arise ambayo itakuwa sasa ina stake katika benki ya mozambique ambayo wameona ni emerging market pamoja na benki nyingine nchini Ghana. Na kampuni hiyo sasa kuongozwa na ceo mpya aitwaye Deepak Malik. Ni moja ya strategy za kampuni ku-diversify portfolio ili kupunguza risk at the same time taking advantage of new emerging markets. Hii transfer haina effect yoyote katika inflow/outflow of cash. Please refer to Mergers and acquisitions, P4, P7 ACCA course)
 
Serikali ndio mwanahisa mkubwa kwa sasa.

Ni jambo jema!
Mkuu John hili unaloongea ni kweli au tusubiri maelekezo mengine? Na Kama yatatoka maelezo tofauti na unachokikubali wewe hapa je taarifa zako zitakuwa na credibility hapa jukwaani?
 
Nadhani umemaliza maswali yangu mkuu.thanks

By the way nadhani mada kama hizi ni mhimu kujadiliwa watu ili wenye uelewa mdogo kwenye mambo mhimu kama haya tunapata mwanga kupitia jukwaa hili
 
Utasemaje hakutakuwa na economic impact kwa Tanzania wakati amepunguza capital na kudiversify Ghana mkuu? Kama hiyo kampuni mpya ingekuwa inafanya kazi hapahapa nchini kungekuwa na hakuna kushake kwa inflow/outflow of cash.
Tueleweshane tafadhali
 
Nadhani umemaliza maswali yangu mkuu.thanks

By the way nadhani mada kama hizi ni mhimu kujadiliwa watu ili wenye uelewa mdogo kwenye mambo mhimu kama haya tunapata mwanga kupitia jukwaa hili
Kuna mambo mengine hata hayahitaji kua na uelewa mkubwa. Ni issue ya kua na tarifa sahihi na iliyokamilika, na km huna hio taarifa kua willing kuitafta.
Jamii tuliyonayo haitaki kutafta taarifa sahihi na iliyokamilika..unaweza kubuni taarifa yoyote fake au iliyo nusu kamili, ukaipost kwenye mitandao ya kijamii then ukakaa pembeni ukajionea ni jinsi gani watu wanaijadili kwa mihemko ukabaki unashangaa hapa ndo jamii yetu ilipofikia.

A simple google search ya hii tariifa ingemfikisha mtoa mada kwenye official website ya nmb ambayo inge clear all his/her doubt na yy kutuletea kitu kilichokamilika tukijadili km Great Thinkers and not otherwise.
 
Now days jiwe agawa Hela barabarani ni ujinga wa Hali ya juu

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Huu ni ujinga serikali haiwezi kufanya biashara na ikafanikiwa, kazi ya serikali ni kuwa regulator.
Huwezi kufanya regulation kwenye eneo ambalo wewe mwenyewe siyo mshiriki, haya mambo yameifanya serikali ipigwe kwenye kila sehemu na watu wanaoitwa wafanyabiashara na wawekezaji. Serikali inaweza ikawa na kampuni zake kwenye kila sekta na bado ikawa na wawekezaji binafsi kwenye maeneo hayo hayo.
 
Utasemaje hakutakuwa na economic impact kwa Tanzania wakati amepunguza capital na kudiversify Ghana mkuu? Kama hiyo kampuni mpya ingekuwa inafanya kazi hapahapa nchini kungekuwa na hakuna kushake kwa inflow/outflow of cash.
Tueleweshane tafadhali
Kuna muwekezaji mpya ameingia ambaye ata inject additional capital, na sasa kwenye mgao huu mpya Rabo bank atapata gawio la 25% ya kampuni hiyo mpya. Additional capital haihusiani na market ya Tanzania. Wanataka kufanya expansion kwenye hizo market nilizotaja (Ghana & Mozambique)
 
Rabo bank, FMO (Dutch Entrepreneurial Development Bank) na Norfund (Norwegian Investment Fund) waliunganisha assets zao kutengeneza “Arise”. Kwahiyo Arise ndo atakuwa mmiliki mpya wa NMB.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…