‘Shark loans’ namna taasisi za fedha za nchi tajiri wanavyowalewesha mikopo nchi maskini na kuweka mazingira ya kufubaza uchumi

Mwaka huu unaokuja nataka kuongeza mazungumzo yanayokwenda kwa hoja za kiunazuoni na vitabu, data, research.

Hata kama ni kwa kutaja waandishi na kuweka vitabu tu watu tusome tujue zaidi.

Na pia na sisi tuandike zaidi.

Ukitaka kuanza kuyaelewa vizuri mambo haya, kama hujamsoma, mfuatilie muandishi anaitwa John Perkins.

Nikisoma vitabu vyake vinavyoelezea economic espionage katika geopolitics, halafu nikiangalia uongozi wetu na uwezo wake, naona tumepwaya sana, sana tu.

John Perkins ameandika au kuhariri vitabu hivi.

The Secret History of the American Empire: The Truth About Economic Hitmen, Jackals, and How to Change the World

A Game as Old as Empire: The Secret World of Economic Hit Men and the Web of Global Corruption

Confessions of An Economic Hitman

Hoodwinked. An Economic Hit Man Reveals Why the World Financial Markets Imploded--and What We Need to Do to Remake Them

Not One Drop: Betrayal and Courage in the Wake of the Exxon Valdez Oil Spill

The New Confessions of an Economic Hit Man


Vitabu hivi, kasoro kimoja ambacho kipo katika epub format, nimeviweka katika attachments.
 

Attachments

Economical model ya TZ ndiyo ina attract loans appetite.
 
Na ukiona nchi inakopa kulipa mishahara ambayo ni operating expenses na sio capital expenditure... hapo ndo unajua kwamba hii ni house or cards inatengenezwa
 
Mambo magumu kama haya huwa hawataki yaongelewe utaanza onekana adui wa serikali badala ya mzalendo.

Kwao mzalendo ni kuwa Chawa na kumsifia sifia Rais Kila ndio mzalendo.

Mambo ya kijinga kabjsa.

"Tatizo hapa hatuna akili kabisa..." -Dr Godwin Mollel.
 
Asante sana mkuu.. na mimi ni mdau mkubwa wa kufuatilia Geopolitics.. ni somo pana sana maana linaenda pia kwneye mbinu za kiuchumi ...

Sidhani kama mataifa mengi ya nchi masikini kwenye idara zao za usalama wa taifa, huwa kuna ma analyst kwenye issue nzima ya Geopolitics na economics.. maana haya ni mambo ambayo yanaweza kuweka taifa kwenye risk kubwa sana ..

Asante kwa vitabu
 
Anytime.

Nakubaliana na wewe sana. Nimeanza kusoma tu "A Game As Old As Empire". Kinaanza tu na mi data ya kufa mtu kuonesha how the game is stacked against us, halafu nikiangalia tulivyokuwa addicted na mikopo, naona kabisa "this is a train wreck waiting to happen".

Ukisoma "Confessions of An Economic Hitman" unaona kabisa tunapitishwa mulemule.
 
Economical model ya TZ ndiyo ina attract loans appetite.
Wanatukopesha kwa sababu walifanya assessment zao wakaona Tanzania ni kama vile msitu wa miti mizuri ya mkaa, ambayo kwao kwasababu wao ni wachoma mkaa wanahitaji miti hiyo kuchoma mkaa.

Lakini jiulize, kuna pori la miti ya kuchoma mkaa ambalo limedumu daima?

Maana yake ukiona wanakimbilia kuikopesha Tanzania ni kwa sababu wanaona bado hii nchi haijaelemewa na madeni na kwamba zerikali yao bado inahitaji kukopa zaidi na zaidi.

Kwahiyo na wao wanafurahi kwasababu wanapata wakuwashikisha hela zao za moto.
 
Powa powa mkuu naahidi kuvifuatilia kwa undani.. hiyo title ya 'Confessions of an economic hitman' imenishawishi
 
Ni shida sana mkuu... na hawataki tuhoji pia
 
Nasikitika sana mada kama hizi zina wachangiaji wachache na wafuatiliaji wachache sana, kinyume na mada zisizo na maana zinavyo kimbikiliwa.
Tunaweza tusiwe na mchango wa maana kwenye mada kama hizi kutokana na kiwango cheti cha ufahamu kwenye mambo ya uchumi na fedha lakini hatutakosa mengi ya kujifunza kutokana na maoni ya wataalamu na walio pitia vitu hivyo.
Hongereni sana wadau mlio changia uzi huu pamoja na mleta mada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…