Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Mwaka huu unaokuja nataka kuongeza mazungumzo yanayokwenda kwa hoja za kiunazuoni na vitabu, data, research.Biashara ya kutoa mikopo ni biashara kama biashara nyingine. Unavyouza mikopo Zaidi ndivyo unavyopata faida Zaidi.
Kwa nchi zilizoendelea kama Marekani, mataifa ya Ulaya, Japan, na hata China, hizi ni nchi ambazo zimefanikiwa kuwa na efficiency kubwa sana kwenye mabenki, na pia benki kuu katika nchi hizo kwa ndani ya miaka 15 iliyopita, walikuwa na sera ambazo zilipelekea interest rates (au kiwango cha riba) kwenye hizo nchi, kuwa chini sana.
Matokeo yake ni kwamba, benki na wakopeshaji wengie sana wa hizi nchi tajiri, wamekuwa ni kama wana struggle kwenye kutengeneza faida, hususani kwasababu, cost of funds ni ndogo lakini pia lending costs ni ndogo, kwahiyo wamekuwa wakitengeneza ‘a very thin margin’ kwenye mikopo yao, kitu ambacho kwa investors huwa hakifurahishi.
Kwahiyo trick ikawa ni kwamba, hizi nchi tajiri ikabidi wa dizaini namna ya kuwabambika mikopo nchi maskini the likes of Zambia, Tanzania, Kenya nk. Kwasababu kama nilivosema kwenye utangulizi wangu, biashara ya mikopo, ni kama biashara nyingine, unavyouza mikopo Zaidi ndo unavyozidi kutengeneza pesa.
Na kwa kutumia taasisi zao zao kwenye assessment ya credit ratings, imejikuta kwamba kumejengek mfumo wa kuhakikisha kwamba risk profile ya mataifa mengi maskini inakuwa juu sana, ili basi hata riba ya mikopo ambayo watapewa pia itakuwa ni kubwa.
Mikopo inayofubaza uchumi – mikopo isiyoelekezwa kwenye matumizi yenye tija
Kikubwa ni kwamba, hizi taasisi za kifedha za nchi tajiri, wanataka kuhakisha kwamba, mikopo mingi ambayo nchi masikini watakopa, basi isiweze kulipika daima, ili kwamba iwe ni kama vile Ng’ombe unayemkamua maziwa kila siku.
Kwa hivo basi, nchi maskini zimekuwa zikijikuta zina finance miradi ambayo ‘payoff’ yake ni ndogo iki maanisha kwamba, mradi husika unaweza kuwa na impact ndogo kwenye uchumi kitu ambacho kitapelekea kukosekana kwa cash flow ya kulipa hiyo mikopo husika.
Lakini ni kama pia kuna agenda ambayo huwa inajificha kwenye hii mikopo ya kimataifa. Ni kwanini mikopo ambayo huwa inalenga mambo ya kipuuzi huwa inakuwa inatolewa haraka haraka sana? Na ile ambayo ina maslahi mapana nay a muda mrefu huwa inapigwa danadana?
Ukijijibu hayo maswali ni kwamba, hizi taasisi ni kwamba, huwa hazina malengo ya kuona kwamba uchumi wa hizi nchi unaboreka, ndio maana kuna mikopo serikali inapata kwa haraka haraka na ukiangalia matumizi yake unaona ni matumizi ya kipumbavu.
Zaidi Zaidi nadhani hii ni form mpya ya ukoloni mamboleo kwa kutumia taasisi za kifedha za kimataifa kuhakikisha kwamba wanawalesha na kufubaza maendeleo ya hizi nchi kupitia mikopo. Kwasababu ni mikopo isiyolipika, yenye riba kubwa, na ambayo inabeba systemic risks za kuangusha hata mfumo mzima wa uchumi wa nchi – ukiangalia kinachowakuta Ghana kwa sasahivi.
Inavoonekana ni kwamba pia Tanzania, hatuwezi kujikwepa na huu mtego, tayari tupo kwenye ile debt trap, maana kwa miaka saba iliyopita nchi imeongeza deni kwa karibu USD 12 billion (TZS 27 Trillioni) ambazo mimi binafsi ukiniuliza zilipokwenda, bado ntachelea kukupa majibu.
External debt stock as per BOT
December 2015 – USD 15,408 millions
October 2022 – USD 27,482 millions
Changes between Dec 2015 to Oct 2022 = USD 12,074 millions
Watu wengi wanasema ‘Tanzania bado haipo kwenye high risk category na deni ni stahimilivu kwa just kuangalia tu upande wa debt to GDP ratio’ lakini ukiangalia kwenye upande wa ‘cash flow’ iliyopo na projected cash flow ya hivi vilivyoombewa mikopo, huwezi kuona huo ustahimilivu ulipo.
Nawaachia swali serikali, ‘pesa unayokopa unaifanyia nini?’ hilo swali nadhani ndio tungependa kuskia bunge likijadili kabla ya serikali kwenda kukopa, vinginevyo naona hizi deal zinafanyia kimya kimya na wizara ya fedha, naona kila kukicha kwa miaka 7 iliyopita wakisaidi mikataba ya kukopeshwa mabilioni lakini hawataki kutujibu hilo swali.
Ni hayo tu.
N.Mushi
Hata kama ni kwa kutaja waandishi na kuweka vitabu tu watu tusome tujue zaidi.
Na pia na sisi tuandike zaidi.
Ukitaka kuanza kuyaelewa vizuri mambo haya, kama hujamsoma, mfuatilie muandishi anaitwa John Perkins.
Nikisoma vitabu vyake vinavyoelezea economic espionage katika geopolitics, halafu nikiangalia uongozi wetu na uwezo wake, naona tumepwaya sana, sana tu.
John Perkins ameandika au kuhariri vitabu hivi.
The Secret History of the American Empire: The Truth About Economic Hitmen, Jackals, and How to Change the World
A Game as Old as Empire: The Secret World of Economic Hit Men and the Web of Global Corruption
Confessions of An Economic Hitman
Hoodwinked. An Economic Hit Man Reveals Why the World Financial Markets Imploded--and What We Need to Do to Remake Them
Not One Drop: Betrayal and Courage in the Wake of the Exxon Valdez Oil Spill
The New Confessions of an Economic Hit Man
Vitabu hivi, kasoro kimoja ambacho kipo katika epub format, nimeviweka katika attachments.
Attachments
-
Riki Ott, John Perkins - Not One Drop_ Betrayal and Courage in the Wake of the Exxon Valdez Oi...pdf33.3 MB · Views: 3
-
John Perkins - The New Confessions of an Economic Hit Man-Berrett-Koehler Publishers, Inc..pdf3 MB · Views: 5
-
Steven Hiatt, John Perkins - A Game as Old as Empire_ The Secret World of Economic Hit Men and...pdf1.9 MB · Views: 5
-
Catherine Eagleton, Harcourt Fuller, John Perkins - Money in Africa (British Museum Research P...pdf1.8 MB · Views: 5
-
John Perkins - Confessions of an economic hit man-Berrett-Koehler Publishers (2004).pdf1.6 MB · Views: 5
-
John Perkins - The secret history of the American empire_ the truth about economic hit men, ja...pdf980 KB · Views: 6