The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
- Thread starter
- #41
Ni kweli ndivyo ilivyofanyika. Kwa hilo tunakubaliana wote bila shaka...Hiyo NB ndicho kilichofanyika
Ndio sababu Mbowe aliwaita Halima Mdee na Bulaya kule.Nairobi na kuwabembeleza wajiuzulu
Lakini swali ni hili: Kwa utaratibu gani?
Kumbuka, hata wewe ukitaka kuchukua pesa toka ktk benki akaunti ya JokaKuu, unaweza kuchukua tu...
Utakuwa umepata pesa lakini si kwa njia halali. Utakuwa umeiba..
Hawa nao wameapishwa na kuwa wabunge, sawa. Lakini kwa utaratibu upi..?
Bila shaka kwa kughushi nyaraka zilizowapa uhalali wa kuwa wabunge sawa na wewe johnthebaptist uliyejifanya JokaKuu ukamwibia pesa zake benki..
Swali lingine muhimu ni hili:
Kina nani ndani ya CHADEMA, NEC na Bungeni walisaidiana na hawa kina mama kughushi nyaraka za kuwapa uhalali wa kuwa wabunge...??
NB:
✓ Freeman Mbowe kukutana na Mdee na Bulaya Nairobi Kenya na kuwaomba waachie nafasi hizo haiwezi kuwa na maana hiyo udhaniayo wewe ingalau kwa 95%..
✓ Bali inaweza kuwa ilikuwa kwa manufaa yao hawa kina mama i.e kulinda political reputation yao na pia kukiepusha chama kuingia kwenye purukushani na mgogoro kama unavyoendelea sasa ambao kwa kweli ndiyo wajibu mkuu wa kiongozi mkuu kama m/kiti. Na hii ndiyo yaweza kuwa sababu hasa ingalau kwa 95%...