Shauri Na. 36/2022 la Halima Mdee na wenzake 18 dhidi ya CHADEMA, Spika wa Bunge la JMT & NEC. Ni nini madai yao?

Hiyo NB ndicho kilichofanyika

Ndio sababu Mbowe aliwaita Halima Mdee na Bulaya kule.Nairobi na kuwabembeleza wajiuzulu
Ni kweli ndivyo ilivyofanyika. Kwa hilo tunakubaliana wote bila shaka...

Lakini swali ni hili: Kwa utaratibu gani?

Kumbuka, hata wewe ukitaka kuchukua pesa toka ktk benki akaunti ya JokaKuu, unaweza kuchukua tu...

Utakuwa umepata pesa lakini si kwa njia halali. Utakuwa umeiba..

Hawa nao wameapishwa na kuwa wabunge, sawa. Lakini kwa utaratibu upi..?

Bila shaka kwa kughushi nyaraka zilizowapa uhalali wa kuwa wabunge sawa na wewe johnthebaptist uliyejifanya JokaKuu ukamwibia pesa zake benki..

Swali lingine muhimu ni hili:

Kina nani ndani ya CHADEMA, NEC na Bungeni walisaidiana na hawa kina mama kughushi nyaraka za kuwapa uhalali wa kuwa wabunge...??

NB:

✓ Freeman Mbowe kukutana na Mdee na Bulaya Nairobi Kenya na kuwaomba waachie nafasi hizo haiwezi kuwa na maana hiyo udhaniayo wewe ingalau kwa 95%..

✓ Bali inaweza kuwa ilikuwa kwa manufaa yao hawa kina mama i.e kulinda political reputation yao na pia kukiepusha chama kuingia kwenye purukushani na mgogoro kama unavyoendelea sasa ambao kwa kweli ndiyo wajibu mkuu wa kiongozi mkuu kama m/kiti. Na hii ndiyo yaweza kuwa sababu hasa ingalau kwa 95%...
 
Katiba ya JMT haijataja utaratibu maalumu wa kuwapata wabunge Wanawake wa viti maalumu

Hivyo kila chama kina utaratibu wake

Kwahiyo swala la akina Halima Mdee na wenzake ni la Chadema zaidi kuliko Bunge na NEC
 
Kesi hii ina masilahi kitaifa. Kuingia kwao bungeni ni maelewano kati ya serikali na viongozi wa juu wa chadema kuinusuru serikali na misaada ya wafadhili. Ni case endelevu mpaka uchaguzi 2025.
 
Kesi hii ina masilahi kitaifa. Kuingia kwao bungeni ni maelewano kati ya serikali na viongozi wa juu wa chadema kuinusuru serikali na misaada ya wafadhili. Ni case endelevu mpaka uchaguzi 2025.

..Ni maelewano kati ya serikali na wahusika 19 waliokwenda bungeni.

..kamati kuu ya Chadema haikuhusika, Katibu haku-forward majina, na Nec haikuhusika.
 

..kwenye utawala usiojali sheria kama wa awamu ya 5 jambo hilo linawezekana.
 
Mnyika amekania wapi?

Kumbuka Mahera anayo fomu iliyoasainiwa na J J Mnyika!

..Kamati kuu haikuwahi kupitisha majina ya kina Halima.

..Mnyika amehojiwa na wanahabari na ameeleza kuwa hajawahi kupeleka fomu za kina Halima Nec.

..Mahera angekuwa na hizo fomu kina Halima na Nec wangezitoa hadharani na mchezo ungekuwa umekwisha.
 
..Halima na wenzake waliapishwa na kuwa wabunge kwa maagizo kutoka juu.Chama chao hakikuwateua, na Nec haikuwathibitisha kuwa wabunge.
Nakazia hapa...

Kimsingi hakuna kesi,
 
Halima alishabainisha "anafuga mbwa", sasa mbwa wanaofugwa watamhangaisha vipi?

Kiufupi ni kwamba hawa watu hawana lolote wanalolitegemea mbali ya wafadhiri wao CCM, ambao watatumia vyombo kama mahakama na bunge kulazimisha wanayoyataka wao.
 
..Halima na wenzake waliapishwa na kuwa wabunge kwa maagizo kutoka juu.Chama chao hakikuwateua, na Nec haikuwathibitisha kuwa wabunge.
Hapa ndipo huwa nasema, yule bwana alikuwa na akili za kishetani kwelikweli.
Hakuna jambo ambalo alilionea aibu kulifanya, hata liwe la kipumbavu kiasi gani!

Na wakati akipanga haya, tayari alishaanda mtego wa kumwondoa njiani Mbowe kwa kumbambikizia "ugaidi."

Kwa mipango yote hii, tayari alishajua CHADEMA imekwisha, maanake hatua ambayo ingefuata ni kumkabidhi Halima chama.
 
CHADEMA haijasema imewafukuza ubunge isipokuwa imewafuta uanachama
Na wao wamefungua kesi kupinga kufukuzwa kwao ndani ya chama; ambako wanasema kumekiuka taratibu za chama!

Kama uanachama wao utarejeshwa na mahakama, basi swala la ubunge litakuwa swala jingine ambalo CHADEMA, kama bado watakuwa na nguvu itabidi walishughulikie kama jambo jipya kabisa.
 
HATA kama Chadema haikufuata taratibu za kuwafukuza Je Uteuzi wao wa kuomba Ubunge Ulifuata Sheria na Taratibu kwa Mujibu wa Sheria mpaka Kuapishwa?
Kuapishwa gereji(nilipenda umalizie hoja yako nzuri ivo)
 
HATA kama Chadema haikufuata taratibu za kuwafukuza Je Uteuzi wao wa kuomba Ubunge Ulifuata Sheria na Taratibu kwa Mujibu wa Sheria mpaka Kuapishwa?
Hiyo ni kesi nyengine tofauti ambayo nayo chadema wanaweza kufungua. Infact walitakiwa wafungue kitambo lkn kutokana na siasa za mihemko hawajaliona hilo.
 
Utapoteza muda wako bure na huyu.
 
Waende CCM huko
 
Daktari Mahera atazitoa hizo fomu mahakamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…