Shehe Ponda: Kwanini Spika anaendesha Vikao vya Bunge Siku ya Ijumaa? Au ni kiburi?!

Shehe Ponda: Kwanini Spika anaendesha Vikao vya Bunge Siku ya Ijumaa? Au ni kiburi?!

Kila tatizo linatatulika, ni Mafuvu yetu magumu tu.
 
Kwahiyo sasa mnataka kutuongezea urefu wa weekend,Ijumaa mpaka J.pili,tuhurumieni jamani,hapo bado hujaweka na sikukuu.Ila msianze kupiga kelele mkianza kuambiwa tozo zile kubwa kubwa zinarudi tena maana si kwa kulala huko...
 
Mbona Waislam kila siku kwetu ni siku ya Ibada?

Asituletee mambo yake huyu mtu hana uislam wowote bali vurugu tu, kila ikifika muda wa ibada hiyo Ijumaa naamin maofisini kote huwa tuko guru kwenda ibadani, labda aseme kufanyakazi hakufai basi!

Siku ya J.pili baadhi yetu Waislam huwa tunafunga maduka yetu tukiamini ni siku ya mapumziko..hivyo tuendelee hivyo hivyo na sisi msituchokoze kwenye kuchinja
 
Yeye anazungumzia bungeni
 
Shehe Ponda amehoji kupitia ukurasa wake wa Twitter kwanini Ijumaa isiheshimiwe kwa bunge kama ilivyo Jumamosi na Jumapili?

Ponda anasema Jumamosi ni Siku ya Ibada
Jumapili ni Siku ya Ibada
Na Ijumaa ni Siku ya Ibada, sasa kwanini Jumaa kareem isiheshimiwe au ni kiburi tu!

Sabato njema
Kwa nini jmosi na jpili hatuendi kazini ila jtatu hadi ijumaa tunaenda?
 
Kwahiyo sasa mnataka kutuongezea urefu wa weekend,Ijumaa mpaka J.pili,tuhurumieni jamani,hapo bado hujaweka na sikukuu.Ila msianze kupiga kelele mkianza kuambiwa tozo zile kubwa kubwa zinarudi tena maana si kwa kulala huko...
Anachotaka muda wa swala ijumaa pasiwe na bunge
 
Shehe Ponda.
Unaona mbali! Huu ndio ukweli. Watu wanafanyia kazi za kujipendekeza na Wala sio kufuata taratibu. Tuheshimu Dini zetu. Tulia wajibika.
Je, Ijumaa kwa Waislamu ni siku ya mapumziko kama ilivyo Jumamosi Kwa Wasabato au ni siku ya Ibada na kazi zinaendelea?
 
tukifuata ivyo bas siku za kazi pia zitapungua zibaki nne, kwanin ijumaa Kareem msingeisogeza ikawa jmos au ilishaandikwa na mudi hainaga correction?
 
Shehe Ponda amehoji kupitia ukurasa wake wa Twitter kwanini Ijumaa isiheshimiwe kwa bunge kama ilivyo Jumamosi na Jumapili?

Ponda anasema Jumamosi ni Siku ya Ibada
Jumapili ni Siku ya Ibada
Na Ijumaa ni Siku ya Ibada, sasa kwanini Jumaa kareem isiheshimiwe au ni kiburi tu!

Sabato njema
Bwashee, vipi kule Zenji, ijumaa hakunaga vikao vya Bunge a.k.a Baraza la Wawakilishi?
 
Jumamos na jumapil watu hawafanyi kazi kwasababu ni mapumziko ya mwisho wa wiki sio kwasababu ya kwenda kusali.Kalenda tunayoitumia inatambua kupumzika weekend sio kwasababu tunatakiwa kusali.swala la kusali ilo ni kila mtu na imani yake kulingana na tafsiri yake ndo maana hata kwa wakristo pamoja ya kwamba wanatumia biblia moja bado wanasali siku tofauti kati ya dhehebu na dhehebu wakati biblia imetambulisha siku ya saba kwa maana ya jumamosi.Shehe hapo kateleza.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Huo mfumo tumerithi kutoka kwa wakoloni na kila Mtanzania anajua hivyo hata Marais kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Samia wote wameukuta na watauacha kama ulivyo kama yeye anapenda kupumzika apumzike tu mbona hajazuiliwa au anadhani kwa kuwa Rais Samia ni Mwislamu basi atakubaliana na malalamiko yake Ijumaa kuwa siku ya mapumziko hapana hilo haliwezekani kama ni nafasi ya kuswali Ijumaa hiyo nafasi hutolewa kila mahali serikalini na sekta binafsi na analijua hilo aache Uchochezi kama ni njaa akamwone Mkuu wa mkoa atamsaidia.
 
Back
Top Bottom