Shehe Ponda: Kwanini Spika anaendesha Vikao vya Bunge Siku ya Ijumaa? Au ni kiburi?!

Subhanallah!Hatujafijia huko ndugu.
 
Hajateleza ni kujifanya mtetezi wa Waislamu kumbe ana maslahi yake binafsi.
 
Kuna aya kwenye Quran inayoyema: Mnaposikia adhana acheni kazi zenu mwende kumwabudu Allah, Kisha tawanyikeni katika ardhi kutafuta riziki. Siikumbuki aya hiyo lakini ipo inayoonyesha Ijumaa siyo siku ya kupumzika, ni siku ya kuabudu, na baada ya ibada watu waendelee na kazi za kutafuta riziki. Sasa Sheikh Ponda analazimisha iwe siku ya mapumziko. Ikumbukwe Sheikh Ponda alifaulu kuleta ubaguzi wa mavazi mashuleni kwa Waislamu, Ila hakufanikiwa kubadili mavazi katika majeshi kwa Askari wa kike.
 
Huyu Ponda mjinga sana.....kwa jinsi nchi ilivyo na changamoto zote hizi kaona hili ndio la muhimu...
Nimemdharau sana...kumbe kichwani hakuna kitu
 
Pweinti!

Halafu Islam swala ni kila Siku 5times
Mimi ni muislamu na nakubali hakuna sababu ya kuacha kufanya kazi sababu ya ibada na najuwa hata kama kuna mkutano wa bunge hata shule au ofisini ziku za ijumaa kazi zinafanyika lakini wanapata break ya kutosha ila kwenda kufanya ibada ya ijumaa na swala zingine maana sisi tunaswali mara tano daily. Hakuna haja ya kuanzia mjadala usiokuwa na tija
 
Huyu bila shaka ni shehe wa kichina!! Ina maana hajui kuwa koran haimzuii mwislam kufanya kazi ijumaa? Hata waajiriwa huenda kazini kama kawaida isipokuwa muda wa ibada ukifika wanaruhusiwa kwenda kusali na kisha kurudi kazini kuendelea na kazi!! Hata wanaofanya kazi zao binafsi huamkia kwenye kazi zao siku ya ijumaa na ikifika muda wa ibada huondoka kwenye shughuli zao na kwenda kusali. Wafanya biashara waislam wa maduka kariakoo hali kadhalika hufungua maduka yao kama kawaida siku ya ijumaa na huyafunga muda wa ibada ukifika na kisha hurejea tena baada ya ibada. Hata mlalamikaji mwenyewe hufanya kazi siku ya ijumaa na muda wa ibada huenda zake ibadani na akarejea tena!

Huyu shehe wa kichina naona anataka kulazimisha vuruga isiyokuwepo na lazima adhibitiwe mapema kwa nguvu zote!! Inaelekea anahamu tu ya kupewa airtime asiyoistahili kwenye jamii!!
 
Pweinti ni kwamba Muda wa Ibada Siku ya Ijumaa Bunge liahirishwe

Isiwe wengine wako Msikitini wengine wako bungeni wanajadili hoja mbalimbali
 
Yawezekana wewe ndio islam chinese!
 
Wapagani juma tano.

Wahindu alhamisi.

Waislamu ijumaa.

Wasabato jumamosi.

Wakristo jumapili.

Kazi tutakua tunafanya jumatatu na jumanne tu.
 
Huyu Shehe toka alambe asali kipindi kile cha Lowassa na Ukawa alitulia tulii sasa naona asali imeisha kaamua kuliamsha dude mbona mwenzake Shehe Imam Baswale toka achapwe bakora na kunyang'anywa Msikiti wa Idrissa katulia?
 
Kweli wa j2 na j1 wameheshimiwa siku yao wa ijumaa nao iheshimiwe. Na sisi wa j5 pia tutambulike..
Nakazia mkuu. J5 nayo ipewe nafasi.
Kuna ibada kanisani kwetu
 
Muda wa Ibada uheshimiwe
Kwani aligoma kuheshimu muda wa ibada? Je kuna mbunge yeyote alizuiliwa na spika kwenda kusali ijumaa muda wa ibada ulipofika? Tulikuwa na Spika nguli Adam Sapi na mwislam lakini alikuwa anaendesha vikao siku ya ijumaa na muda wa ibada ukifika anaenda zake kusali pamoja na waislam wenzake. Pia tulikuwa na naibu spika mwislam aitwaye Juma Akukweti. Kadhalika aliendesha vikao vya bunge siku ya ijumaa na muda wa ibada ukifika huenda kusali.

Tatizo la Ponda ni kuwa hajasoma hivyo matatizo yake ya kutokwenda shule yasiitie matope dini yake ya kiislam. Nawaomba waislam mwambieni ukweli huyu mtu wenu vinginevyo anawaaibisha na kuwapaka matope sana!!
 
Moja ya vipindi sheikh ponda kajamba na kuharisha ni hiyo point, watu tunatamani hata jumapili kazi zifanyike kama kawaida ili tukimbizane na uchumi wa dunia yeye anawaza kuongeza siku za mapumziko
 
Ushauri wangu kwa ndugu yetu Ponda ni kuwa hajachelewa maana elimu haina mwisho!! Mzee nenda shule!! Ujinga unakuaibisha wewe pamoja na wafuasi wako!!
 
Mleta mada angeandika kama ambavyo Shehe Ponda ameandika ingeleta uelewa mzuri.
Bei Elekezi hapo mwanzo umenena vyema kwamba waislam hawahitaji wapumzike siku ya Ijumaa na wanapaswa baada tu ya kutekeleza swala ya Ijumaa watawanyike wakatafute rizki. Ila hakukua na ulazima sana wa kutumia lugha ya matusi mwishoni mwa maelezo Yako.
Ponda anaeleza hisia zake kwamba hicho kikao Spika amepanga kifanyike muda wa saa Saba ambao Waislam muda huo ni wa kutekeleza ibada.
Amehoji kwanini apange kikao muda huo wakati hata vikao rasmi vya Bunge siku ya Ijumaa ikifika saa Saba vinaahirishwa?

Hicho ndicho alichokimaanisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…