carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Mwenyekiti wa Taasisi ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) Sheikh Alhad amevitaka vyama vya siasa nchini kuweka mbele maslahi ya taifa na kukubali maridhiano kwa ajili ya kulinda amani, umoja na maisha ya Watanzania.
Amesema maridhiano yanahitaji busara, hekima na utayari wa kila upande kusameheana na kuvumiliana, badala ya kila mmoja kushikilia maslahi yake bila kuzingatia hali ya nchi.
Amesisitiza kuwa si kila aina ya uanaharakati inafaa, akionya dhidi ya vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani na maisha ya Watanzania. Ameongeza kuwa maridhiano ya kweli yanahitaji pande zote kuthamini utu, kuheshimiana na kuwa tayari kufanya maamuzi magumu kwa manufaa ya taifa.
Chanzo: Nijuze news
Amesema maridhiano yanahitaji busara, hekima na utayari wa kila upande kusameheana na kuvumiliana, badala ya kila mmoja kushikilia maslahi yake bila kuzingatia hali ya nchi.
Kuhusu mchakato wa maridhiano Tanzania Bara, amesema JMAT haiwezi kueleza hatua zilizofikiwa kwa kuwa suala hilo liko mikononi mwa wanasiasa, akibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeonesha utayari wa kufanya maridhiano na vyama mbalimbali vya siasa.Amesisitiza kuwa si kila aina ya uanaharakati inafaa, akionya dhidi ya vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani na maisha ya Watanzania. Ameongeza kuwa maridhiano ya kweli yanahitaji pande zote kuthamini utu, kuheshimiana na kuwa tayari kufanya maamuzi magumu kwa manufaa ya taifa.
Chanzo: Nijuze news