Sheikh apinga Urais kwa mwanamke

Sheikh apinga Urais kwa mwanamke

Huyo shekhe ni Nani katika Nchi ambayo ina mchanganyiko wa dini mbalimbali? Alidhani Tanzania ni Nchi ya Kislamu?!!! Kama mnasheria zenu za kislamu nchi za kwenda mnazijua nendeni Uarabuni. Tanzania Tunaongozwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania fullstop. Hizo kelele zenu za chura pelekeni mahali sahihi..Mnajifanya mnajua dini mbona watoto wenu wanasoma shule mchanganyiko sio kama Pakistan?? Hii nchi haiongozwi na SHARIA.. waafrika ushamba umetuzidi kwa kupenda tu kubeba mambo ya watu na kujifanya tunajua sana. Dini hizi zimeletwa na wazungu na waarabu lakini kabla ya hapo tulikuwa na mambo yetu mila zetu,tamaduni zetu, dawa zetu, style zetu za maisha ziko wapi??? Tazama wahindi na wachina walivyobakia na mambo yao hata baada ya ukoloni. Hivyo mkitaka hayo fuateni nchi zinazoishi kwa kutumia Sharia hayo mambo msituletee Tanzania.
Sheikh aliongea mapema kabisa kabla hata ya Samia kuwa Rais.
 
Marekani walivyoona mwanamke anataka kuwa Rais wakapiga kura za hasira!!

Nilishangaa sana haha wakati wao ndio walioleta hii ishu ya Feminist sijui 50/50 afu hawataki kuongozwa na mwanamke!
 
sheik ana elimu gani?


Itabidi wenye ilmu ya dini toka vyuo vinavyo tambulikana, kuheshimiwa na kusifiwa duniani waje waseme, mfano wale wenye ilmu ngazi ya juu kuhusu Uislamu, tamaduni mithili ya kina Sheikh Abdallah Seif waje watoe fatwa juu ya matamshi mazito ya kubagua viumbe wake mola kisa ni jinsia :

Simulizi za wazee wetu : Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini Tanzania

(NZIMA)-SIMULIZI YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SEIF (1939 -2020) - HISTORIA YETU part 1









KIU YA ILMU, SHEIKH ABDALLAH SEIF ILIMPELEKEA KUSOMA KWA MIAKA 11 MFULILIZO KATIKA NCHI ZA IRAQ, LEBANON NA IRAN (1968-1979)



Sheikh Abdallah Seif Linganaweka anatujuza kuwa Wenyeji wa Lindi jina Lao la asili ni Wakudewe kwa sasa almaaruf wanafahamika kama waMachinga wa pwani ya Lindi.



Babu yake Babu Abdallah Seif alikuwa mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga mwenye watumwa baada ya kuwazidi wanyonge majirani kuja kuwatumikisha kujaza vyakula. Mfalme Alei(Ali)waLunga.. wa Lindi. Baada ya kuja mkoloni Muingereza nchini Tanganyika, aliua ufalme na kubakiza uchifu. Sehemu za pwani ziliathirika kwanza kwa kupoteza ufalme mapema kabla ya watu wa bara.. Pwani wakabakia na usheikh na uchifu... usiokuwa na nguvu kama falme za asili za maeneo yao Lindi / Kilwa kabla ya kuja ukoloni...



Sheikh MbogaBure mjuzi wa lugha ya Kiarabu, dini pia mmoja wa waanzilishi wa madhehebu ya Shia Tanzania amuunganisha Mzee Abdallah Seif kupata scholarship kwenda Baghdad, Iraq mwaka 1968 kusoma zaidi dini...



Kijana Abdallah Seif mwaka 1968 alipokwenda Kijijini ashutumiwa kupotea kwa kuukumbatia u-Shia mojawapo ya madhehebu ya dini ya KiIslamu, wakati wengine wote ni Sunni. Lakini babu yake msomi wa dini madhehebu wa Sunni anayetambulika Lindi na Kilwa hakuwa anatoa shutma zozote alikuwa msikivu na kumtia moyo Abdallah Seif asome zaidi na ili kuifahamu dini vizuri zaidi.



Kilichomsukuma Sheikh Abdallah Seif kuvutiwa na u-Shia ni namna masheikh wa ki-Shia walivyokuwa wazi (tabligh) kukaribisha maswali tofauti na madhehebu mengine ya KiIslam ambapo kijana hakuruhusiwa kuhoji na pia kuuliza maswali ilikuwa inachukuliwa ni utovu wa nidhamu kwa waalimu au masheikh wake.



Safari ya Sheikh Abdallah Seif wenzie vijana wakiwemo kina Sheikh Isihaka Pingili kwenda Iraq kwa meli iliwachukua mwezi mzima kupitia bandari mbalimbali za Zanzibar, Tanga, Mogadishu, Bahrain na kuishia Basra nchini Iraq na kutua katika chuo cha Hawza mji wa Najaf Iraq



Ujio wao Basra, Iraq ulileta tafrani kwa mwenyeji wao Mpakistani mfanyabiashara mkubwa nchini Iraq enzi hizo na kupelekea Saadam Hussein kumshutumu mfanyabiashara huyo tajwa kuleta majasusi wa kiAfrika ikumbukwe ndiyo kwanza Saddam Hussein na chama chake cha Baath walikuwa wanajaribu kushika hatamu za kuongoza nchi baada ya mapinduzi nchini Iraq. Mpakistani huyo alinyongwa mwaka 1969 pamoja na wafadhili wengine kama kuna Bakri Sadr waliowezesha ujio wa vijana wa kiAfrika
kuingia Iraq kwa dhumuni la kusoma dini.



Kutokana na hilo ikabidi Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine wa kiAfrika waondoke Iraq mwaka 1970 kwenda Lebanon kwenda kuendelea na azma yao ya kusoma dini.



Sheikh Abdallah Seif wakakaa Lebanon kuanzia mwaka 1970 mpaka 1978 ambapo mara nyingine masomo ya dini yakaingia changamoto baada ya vita baina ya Wapaletina waliokuwa kambi za ukimbizi Lebanon na waLebanon wenye nchi na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe.



Mwaka 1978 Ikabidi Sheikh Abdallah Seif na wenzie wahamie nchi ya jirani ya Iran kwenda katika mji wa Qom city kuendelea na masomo yao ya dini. Iran ilikuwa imetulia nchi ya amani chini ya utawala wa mfalme (Shah) Mohammed Reza Pahlavi Historic Personalities of Iran: Mohammad Reza Shah Pahlavi miaka 7 waliakaa Iran wakiendelea kusomeshwa.



Wakati wa likizo Iran wengine wenda Ufaransa kuchuma zabibu mashambani au kufanya kazi sehemu za utalii wa ndani wa Iran au kuchukua mabusati ya kushona ya Iran yanayosifika Uarabuni kote kwenda kuyauza ktk nchi mbalimbali za Arabuni ndivyo mwanafunzi kama Sheikh Abdallah Seif na wenzie vijana walivyojiongezea fedha za kujikimu na kupeleka kiasi cha pesa nyumbani Tanzania.



Hatimaye mwaka 1980 baada ya ukisoma kwa miaka 11 nje ya Tanzania ,walitunikiwa shahada ya baccalauréat ya masomo ya dini na kurejea Tanzania. Kwa miaka hiyo 11 ughaibuni pia waliweza kusoma elimu ya secular kiwango cha sekondari kwa njia ya posta masomo ya nchi ya Uingereza kwa msaada mkubwa wa swahiba wa kiongozi wa kijeshi wa Nigeria Jenerali Yakubu Gowon. Swahiba huyo alikuwa mfanyabishara wa vituo vya mafuta na makazi yake Uingereza.



Mahojiano haya yanakuja kwa hisani kubwa ya Ammar Dachi yaliyemshawishi Mzee Abdallah Seif kufunguka historia ya mapito yake, ukoo , ilmu na utafiti wa mafuta 1955 na pia ujio wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania


HISTORIA YA ABDALLAH SEIF (1939 -2020) Part - 2







Sheikh Alhaj Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Mnan’gole sehemu za Dimba mkoa Lindi Tanzania anaendelea kusimulia kazi kubwa aliyofanya ya kujitolea ya kueneza dini.



Sheikh Abdallah Seif anasisitiza umuhimu wa ilmu na elimu kwa wanazuoni wote wa KiIslamu.



Anasema ili sheikh awe mwanazuoni aliyekamilika kufundisha chuoni lazima kusoma ilmu ya dini kwa angalau miaka 15.



Anakumbuka alivyokuwa mjini Qom Iran akisoma chuoni alionana na wazee wa miaka 70 wakijiendeleza na kuwaambia wao vijana kuwa inahitajika walau miaka 35 ili kuielewa dini nje ndani kwa ufasaha. Wazee hao walicheka waliposikia vijana Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine toka Afrika wakisema wanataka kusoma dini kwa miaka 5 mpaka 10 tu ilihali wametoka Afrika na kuwaambia bila kupepesa macho kuwa ili wawe wabobevu wafikirie miaka angalau 15 ya ilmu ya dini ngazi ya chuo.



Hivyo akiwa amepikika kwa elimu tosha ya kidini baada ya kufanya kazi kwa takriban miaka 11 nchini Tanzania, mwaka 1990 sheikh Abdallah Seifu alikwenda Nampula jimbo la Cabo Delgado nchini Mozambique kufanya kazi ya dini.



Kisha sheikh Abdallah Seif alishuka mpaka mji mkuu wa Maputo Mozambique na alisaidia kufungua taasisi rasmi inayotambulika na serikali na kupewa leseni iliyosajiliwa Maputo Mozambique kwa ajili ya taasisi ya Shia Ithna-Asheri Muzdalifah . Sheikh Abdallah Seif anazungumza lugha za Kiswahili, Kiarabu, Kiingereza na Kireno.

Source : Asadiqmedia
 
Ningepata anyejua vizuri anieleweshe hiyo ni maoni ya Sheikh au ni kwa mujibu wa Dini na unaandika yake? Ingenisaidia sana.
Sheikh amenukuu Qur'an...

Na hajaongea leo au jana, hiyo ni clip ya zamani.
 
Sheikh amenukuu Qur'an...

Na hajaongea leo au jana, hiyo ni clip ya zamani.
Naijua kuwa ni zamani ila leo nikiwa naitafakar na kwa bahati nzuri Uzi bado juu. Sasa kama ni hivo wakuu wa Dini yake wanaogopa kumwambia kwamba si sawa au ndo uoga wa viongozi wa Dini nyingi uliowakumba tangu awamu ya 5
 
Naijua kuwa ni zamani ila leo nikiwa naitafakar na kwa bahati nzuri Uzi bado juu. Sasa kama ni hivo wakuu wa Dini yake wanaogopa kumwambia kwamba si sawa au ndo uoga wa viongozi wa Dini nyingi uliowakumba tangu awamu ya 5
Unafiki ni mbaya sana mkuu!
 
Back
Top Bottom