Sheikh apinga Urais kwa mwanamke

Sheikh apinga Urais kwa mwanamke

Wee huyo shetani mwenyewe alijua kabisa kuwa mwanamke ni dhaifu ndio maana akaamua kumfuata eva na sio adam.
 
Unafiki ni mbaya sana mkuu!
Nataman hata kutowaamini hawa viongozi wa Dini na madhehebu kwasababu wamegeukia Nebukadneza wamebaki wachache tu amina Daniel, Hanania,Michael na Azaria.
 
Vipi kuhusu ujerumani?

Umeulizwa vipi kuhusu Germany umeufyata ghafla!!
Viongozi wa Ujerumani siyo Waislam.

Hata hivyo, Ujerumani ina Rais wake ambaye ni mwanaume boss.

Screenshot_20220404-093641_Chrome.jpg
 
Atajikuta mabwepande huko maana ndiko mahali awamu ile yenye mahusiano na hii walikua wanapeleka watu.
Ile awamu ya Msoga ilikuwa ya laana, nchi iliongozwa na vibaka tu.....ukitoa ushauri unakamatwa na kung'olewa kucha bila ganzi na kama haulii unapelekwa Mwabepande kupotezwa. Ukimchekelea kiongozi bila hata sababu anakualika pamoja na wasanii wa bongo fleva na muvi kwenda kunywa chai na maandazi Ikulu. Yule jamaa alitulostisha sana na cha kushangaza eti sasa kapewa tena nchi na Mama kawa kaimu wake. Mama nchi inamshinda hii.
 
Wanawake katika Qur'an,wamepewa nafasi ya juu kabisa.Kuna chapter mbili,zimepewa majina ya wanawake,
1:Surat Maryam(mama wa Nabii Issa,na Mwanamke huyu kuitwa Mwanamke bora kuliko Watu wote(wanawake),duniani.
2:Suratil Annisai(Wanawake).Yaani wanawake wote,Wana Chapter yao ndani ya Qur'an,hakuna Chapter ya Rijal(wanaume wote).
3:Mwanamke katika uislamu,ukimuoa anabaki,na ubini wake ule ule wa baba yake, hakuna kuitwa Mrs Fulani.
4:Mwanamke katika uislamu,ikitokea bahati mbaya,amezaa mtoto nje ya ndoa,anahesabika ni mwanawe,na wanarithiana mali.Lakini mwanamme akizaa nje ya ndoa,huyo mtoto,hahesabiki ni wake,na hawarithiani mali.
5:Mama(Mwanamke),amepewa daraja tatu zaidi ya baba,katika kumtendea wema,yaani ukimtendea baba mara moja wema,umtendee mams,mara tatu yake.
6😛epo ,ya mtoto(hata awe ana miaka 60 au 70)madhali mama ake yuko hai,asipomtendea wema,hapati Pepo,hata awe Sheikh wa namna gani.
7:Bi Khadija(Mwanamke),mtu wa kwanza kumuamini Mtume Muhammad(S.A.W).
8:Khadithi(Hili ni neno la kiarabu,lenye maana ya kwa kiingereza tradition(miongozo)),mingi kutoka kwa Mtume,imepitia kw Bi Aisha(Mwanamke),Asma bint Abubakar(Mwanamke),Bi Khadija(Mwanamke),na wengi wengineo.
 
Ile awamu ya Msoga ilikuwa ya laana, nchi iliongozwa na vibaka tu.....ukitoa ushauri unakamatwa na kung'olewa kucha bila ganzi na kama haulii unapelekwa Mwabepande kupotezwa. Ukimchekelea kiongozi bila hata sababu anakualika pamoja na wasanii wa bongo fleva na muvi kwenda kunywa chai na maandazi Ikulu. Yule jamaa alitulostisha sana na cha kushangaza eti sasa kapewa tena nchi na Mama kawa kaimu wake. Mama nchi inamshinda hii.
Mara mia awamu ya msoga kuliko awamu ya wasukuma mikokoteni.
 
naunga mkono hoja, ni kweli kuna baadhi ya Masheikh ni Masheikh ubwabwa.
Sheikh wa ukweli ni huyu

P

Huyu sasa ndio Sheikh Ubwabwa...hata yule sheikh wa mwanzo uliyemuita sheikh ubwabwa hajapinga wanawake kushirikishwa kwenye kutoa mawazo au hata uongozi, lakini sio uongozi wa juu, hata huyo Mtume ambaye huyu sheikh ubwabwa wako anamtumia kama reference hakuwahi kuruhusu mwanamke kuwa kiongozi wa juu!
 
Wanawake katika Qur'an,wamepewa nafasi ya juu kabisa.Kuna chapter mbili,zimepewa majina ya wanawake,
1:Surat Maryam(mama wa Nabii Issa,na Mwanamke huyu kuitwa Mwanamke bora kuliko Watu wote(wanawake),duniani.
2:Suratil Annisai(Wanawake).Yaani wanawake wote,Wana Chapter yao ndani ya Qur'an,hakuna Chapter ya Rijal(wanaume wote).
Umeenda nje ya mada. Rudia kuisikiliza na kuielewa hiyo video clip.
 
Wanawake katika Qur'an,wamepewa nafasi ya juu kabisa.Kuna chapter mbili,zimepewa majina ya wanawake,
1:Surat Maryam(mama wa Nabii Issa,na Mwanamke huyu kuitwa Mwanamke bora kuliko Watu wote(wanawake),duniani.
2:Suratil Annisai(Wanawake).Yaani wanawake wote,Wana Chapter yao ndani ya Qur'an,hakuna Chapter ya Rijal(wanaume wote).
Kuwa na sura mbili kwenye Qur'an tukufu haimaanishi kuwa wamepewa nafasi za uongozi wa juu, leta dalili ya kuwa mtume Mohamad (S.A.W) alimpa mwanamke uongozi wa juu dhidi ya wanaume!
 
Huyu sasa ndio Sheikh Ubwabwa...hata yule sheikh wa mwanzo uliyemuita sheikh ubwabwa hajapinga wanawake kushirikishwa kwenye kutoa mawazo au hata uongozi, lakini sio uongozi wa juu, hata huyo Mtume ambaye huyu sheikh ubwabwa wako anamtumia kama reference hakuwahi kuruhusu mwanamke kuwa kiongozi wa juu!
Wengi wanakimbilia kutoa maoni yao bila kumsikiliza sheikh.
 
Kuwa na sura mbili kwenye Qur'an tukufu haimaanishi kuwa wamepewa nafasi za uongozi wa juu, leta dalili ya kuwa mtume Mohamad (S.A.W) alimpa mwanamke uongozi wa juu dhidi ya wanaume!
Bi Khadija,alimuajiri Mtume Muhammad (S.AW),na akawa ni kiongozi wake katika biashara za huyu Bibi.Na mpaka anapata Utume,alikuwa kwa Bi Khadijah,na mwisho akawa mkewe.Na ndio mtu wa kwanza(Mwanamke)kumuamini kuwa Muhammad(S A W),ni Mtume.Na Mtume mpaka anafariki,alikuwa akimsifia Bi.Khadija.
 
Huyu Sheikh ni male chauvinist, analeta mambo ya male chauvinism ya kuwabagua Wanawake.

Hapa aitwe Sheikh Mkuu, kulifafanua hili na ikibidi huyu Sheikh avuliwe usheikh.

Mafundisho ya kweli ya Uislamu kuhusu mwanamke wa Kiislamu na uongozi ni haya

P
Ushekh unavuliwa na Mufti?acha ushamba ndugu yangu.Uislamu kupitia Quran unasema Wanaume ndio viongozi wa wanawake Sasa Mufti hajui hiyo Aya?Na pia kwa mujibu wa Mtume mkiongozwa na mwanamke mnakuwa mnapata laana ndio maana hakuna immam mwanamke Wala nabii mwanamke kwa Wala khalifa mwanamke kwa mujibu wa uislam.
Swala la uongozi Kama itakuwa ni kuongozna wanawake kwa wanawake hapo sawa au awe kiongozi wa chini na sio kiongozi mwenye mamlaka ya mwisho .Wewe mwenyewe unajua hilo Ila njaa na tamaa ya madaraka na unafiki vinakufanya utete ujinga.Mke wako nyumbani anakuongoza au unamuungoza?
 
Back
Top Bottom